Wakuu, binafsi nilifuhia sana, Waziri Hamis alivyohamasisha wasanii wengi kupanda Mlima Kilimanjaro kwa Mara moja, kwa kauli mbiu Twende Zetu Kileleni...
Safari ilianza Jana Jumamosi Tarehe 28/09/2019, Ilikuwa ya siku sita.
Lakini Diamond, Steve Nyerere na Dogo Janja wamerudi leo Jumapili baada ya kuchoka sana... Walifika kituo cha kwanza Mandara wakarudia mbele kidogo ya Mandara.
Changamoto kubwa ni kupanda Mlima kwa mhemko, na pia nilishasema tena hapa kwenda gym kila siku hakukupi uwezo wa kupanda mlima Kilimanjaro. Na pia jamaa walionekana wakienda kwa kasi sana, Kosa kubwa... Kilimanjaro ni Polepole.
Bado nina wazo la kupanda Mlima Kilimanjaro na WanaJF walioko committed.
Na wote tutatoboa...
Wasanii waliobakia, wajitahidi sana ili watoboe.