Kwan Clouds unadhan Joseph anamilik peke yake?? Kuna kina KUSAGA 5 wako pale wote na share
Anae onekana mbele siku zote FOUNDER, ambae anakua ni sura ya kampun
Mfano Jack Ma wa Alibaba, sina kumbukumbu vizuri ila umilik wake ndani ya kampuni ni chini ya 30%, mshindan wake huko kwao Tancent ( Pony Ma=mmilik) nae hvyo hvyo
UBER unaijua, kaangalie mwanzilishi n nani na aliekaa pale juu saiv n nani,
Wenzetu hua mambo yao yanapiga hatua kwakua na STRONG INSTITUTIONS , unakuja na wazo, likimake sense kwa watu (wawekezaji/Investors) wanatia pesa wanamilik hisa ndani ya kampun, wewe mwanzilish unabak kama Face of the company, na utatambulika kama founder, ila humo ndan kuna mtu anaweza kua na share nying kuliko wewe hata voting power vile vile
Nenda kasome samsun ilivyo
Steve Jobs anasifika kama mwanzilishi wa Apple, je wajua kuna wakati alifukuzwa kabisa kwenye board?? ikambidi akaanzishe kitu kingine ambacho baadae kilikuja mrudisha kwenye board of directors ??
Wenzetu wanafanya hvyo, leo mkurugenzi/mwanzilish/mmilik akafa, company hua zinabak zinaendeleza operations
Sasa hili sie kinamadange tunapata nafasi ya kulijua, badala tupate cha kujifunza tunaona NONGWA, sijui wivu, tukabatizwe kwa maji mangi walai