Watoto wenu mnawaadhibu kwa fimbo na matusi kila saa wataacha kudumaa kiakili! Halafu unakuta kucheza wanacheza wenyewe vichochoro! Huyu mnasema ana kitu cha ziada inaonyesha ushamba flani. Siyo kosa lenu lakini ila hamjatembelea duniani muone. Nchi zilizoendelea asilimia kubwa ya watoto ni zaidi ya huyu i.e. wadadisi, wana akili wanajiamini na wanaongea kama watu wazima! Hakuna cha ajabu hapo bali ni malezi na mazingira mazuri wanayokulia. Hata chekechea wanakosoma wanafundishwa vitu vya kukuza na kupanua akili. Huku kwetu akiingia kwenye daladala anakutana na matusi na mziki wa Bongo Flavour akifika nyumbani nako sijui kuna kanga Moko.