Ndo maana nikasema hivi, iwe hajaenda Diamond au yeyote yule, Dully hakutakiwa kulalamika... kama wa kulalamika, wangelalamika wengine kwa niaba yake! Si busara kumlalamikia mtu kwamba mbona hukuja kunitazama wakati naumwa au kwanini hukuja kwenye msiba wa ndugu yangu... likitokea jambo kama hilo unatakiwa kukausha huku ukifahamu kwamba kumbe niliokuwa nawadhania ni wenzangu; sio wenzangu!
Binafsi niliwahi kukutwa na misiba miwili... mmoja wa m-sure wangu na mwingine wa sister angu kipenzi! Kwa bahati mbaya, sikuwapo! Nilipofika miezi kadhaa baadae, nikamuomba my best friend, I repeat, MY BEST FRIEND! Huyu bwana nikamuomba anipeleke akanioneshe kaburi la m-sure na sister! Sikuamini hata kidogo aliponiambia hakuhudhuria mazishi ya yeyote kati ya hao kwahiyo alikuwa hajui makaburi yalipo!!!! Hii ni true story, sijawahi kumwambia yeyote na siri hiyo ndo naitoa hapa kwa mara ya kwanza! Na wala mshikaji sikumuuliza na wala sijamuuliza ni kwanini hakuhudhuria... ikabaki siri yangu ingawaje niliumia kishenzi!!!!! Sikumuuliza kwa sababu nilihisi labda aliona misiba ile haikumuhusu...! Panapo msiba ni wako peke yako na sherehe ndiyo ya wote... kwahiyo unatakiwa tu kumsubiria rafiki wa kweli aje na asiyekuja huna sababu ya kuhoji kwanini hakuja... labda aanze kueleza mwenyewe kwanini hakuja!