Diamond atoa sababu za kushindwa kuhudhuria msiba wa baba yake Dully Sykes

Diamond atoa sababu za kushindwa kuhudhuria msiba wa baba yake Dully Sykes

chige kiuswazi hua wanaangalia kama ukienda kwenye misiba kula huli na kwako watakuja ila kula hawali. Kuna Jirani yangu hua anahudhuria misibani kisha anachambua mchele kisha anapika ila mida ya kula hali sasa na yeye wakamfanyia hivyo hivyo ikabidi akaite bodaboda waje kula
 
Last edited by a moderator:
We kwenye huo msiba ulikwenda? msiba ulipangwa? Dully aligawa kadi? Wewe na Dully huwa mna hudhuria kila msiba? Mbona mna promote msiba kama show? Kwani ni lazima kwenda kwenye msiba? Ange kwenda kila msiba mngekuwa wa kwanza kusema ana kwenda kuuza sura...au anapenda kuonekana kila msiba! Hata Jk alivyo kuwa ana hudhuria misiba kuna baadhi mlianza kumkejeli kuwa anapenda misiba!

Kwanza huyo mfiwa ana watia aibu wale walio kwenda maana anaonesha kuwa wao hawana maana bali kuna watu alikuwa anataka waende!

Nimegundua kwenye hili kuna swala lingine zaidi ya msiba..

"Watanzania wengi ni wachawi sema hawajijui"
Dully mwenyewe hahudhurii misiba ya watu
 
Msiba wa muhusika siku zote unategemea heshima yake binafsi na namna alivyoishi na watu wake Jirani ndugu jamaa na marafiki, tujitahidi kuishi kwa kumpendeza mungu na kufanya mazuri kwa watu wetu hivyo inatosha kuwa faraja kwa wafiwa kwa kuwa kuna mema yakukumbukwa dhidi ya marehemu na mifano ya kuigwa kwa watakaosikia Yale mazuri ya marehemu vinginevyo tutajidanganya tu hata uzikwe na mamia kwa maelfu lkn ukikosa sifa nzuri hata wahudhuriaji watakuwa kwenye kukusononekea kwa hasara utakayokuwa ukiondoka nayo.
Mungu amsamehe na amuepushie adhabu za kaburi huyo marehemu.
 
Kwani Dully amelalamika kuhusu Diamond kutoenda msibani? Wakilalamika wapambe ni wao na mtazamo wao. Maneno yakizidi watu wanaropoka hadi visivyokuepo.

Uchonganishi tu.
 
Chief ni kwamba mtu anapokua juu tunategemea awe mnyenyekevu kwa watu wengine ili maisha ya kitanzania yasonge. Kwa mfano rafiki yako mfano mbotoki kawa mke wa mfalme na wewe kuna siku unapata shida utategemea huyo bi mfalme ndo awe wa kwanza KUJA au sio
Ndo maana nikasema hivi, iwe hajaenda Diamond au yeyote yule, Dully hakutakiwa kulalamika... kama wa kulalamika, wangelalamika wengine kwa niaba yake! Si busara kumlalamikia mtu kwamba mbona hukuja kunitazama wakati naumwa au kwanini hukuja kwenye msiba wa ndugu yangu... likitokea jambo kama hilo unatakiwa kukausha huku ukifahamu kwamba kumbe niliokuwa nawadhania ni wenzangu; sio wenzangu!

Binafsi niliwahi kukutwa na misiba miwili... mmoja wa m-sure wangu na mwingine wa sister angu kipenzi! Kwa bahati mbaya, sikuwapo! Nilipofika miezi kadhaa baadae, nikamuomba my best friend, I repeat, MY BEST FRIEND! Huyu bwana nikamuomba anipeleke akanioneshe kaburi la m-sure na sister! Sikuamini hata kidogo aliponiambia hakuhudhuria mazishi ya yeyote kati ya hao kwahiyo alikuwa hajui makaburi yalipo!!!! Hii ni true story, sijawahi kumwambia yeyote na siri hiyo ndo naitoa hapa kwa mara ya kwanza! Na wala mshikaji sikumuuliza na wala sijamuuliza ni kwanini hakuhudhuria... ikabaki siri yangu ingawaje niliumia kishenzi!!!!! Sikumuuliza kwa sababu nilihisi labda aliona misiba ile haikumuhusu...! Panapo msiba ni wako peke yako na sherehe ndiyo ya wote... kwahiyo unatakiwa tu kumsubiria rafiki wa kweli aje na asiyekuja huna sababu ya kuhoji kwanini hakuja... labda aanze kueleza mwenyewe kwanini hakuja!
 
chige thanx tumeelewana kiswazi unakuta mtu kafiwa lakini anafanya SENSA
Ya waliokula au waliokuja. Pole mkuu past it touches
 
Last edited by a moderator:
Sijapata kuona nchi ya watu wa hovyo kama Tanzania yetu! Yaani mtu analaumiwa kwa sababu hajaenda msibani! Yaani Diamond kumuita Dully kaka kwa kumuheshimu tu ingawaje sio kaka ake ndo ishakuwa nongwa!!! Kuna wasanii wangapi hawajaenda... WHY ONLY DIAMOND?! Hatutashangaa tukisikia kwamba Dully ndo kamtoa Diamond, upuuzi mtupu!!! Davido kushirikishwa kwenye My Number One, anataka anyenyekewe, Dully nae kuitwa kaka (wa heshima), ndo basi tena keshajiona ana haki kumlalamikia asie ndugu yake kutokwenda msibani... upuuzi mtupu, akili za kukosa kazi hizi!

Kama ndo mnavyoishi hivyo na kwenye jamii zenu basi hongereni.

Btw; unafikiri ni kwanini Diamond ameamua kujielezea? Hivi kweli kulikuwa na ulazima wowote wa kujitolea sababu?
 
Ndo maana nikasema hivi, iwe hajaenda Diamond au yeyote yule, Dully hakutakiwa kulalamika... kama wa kulalamika, wangelalamika wengine kwa niaba yake! Si busara kumlalamikia mtu kwamba mbona hukuja kunitazama wakati naumwa au kwanini hukuja kwenye msiba wa ndugu yangu... likitokea jambo kama hilo unatakiwa kukausha huku ukifahamu kwamba kumbe niliokuwa nawadhania ni wenzangu; sio wenzangu!

Binafsi niliwahi kukutwa na misiba miwili... mmoja wa m-sure wangu na mwingine wa sister angu kipenzi! Kwa bahati mbaya, sikuwapo! Nilipofika miezi kadhaa baadae, nikamuomba my best friend, I repeat, MY BEST FRIEND! Huyu bwana nikamuomba anipeleke akanioneshe kaburi la m-sure na sister! Sikuamini hata kidogo aliponiambia hakuhudhuria mazishi ya yeyote kati ya hao kwahiyo alikuwa hajui makaburi yalipo!!!! Hii ni true story, sijawahi kumwambia yeyote na siri hiyo ndo naitoa hapa kwa mara ya kwanza! Na wala mshikaji sikumuuliza na wala sijamuuliza ni kwanini hakuhudhuria... ikabaki siri yangu ingawaje niliumia kishenzi!!!!! Sikumuuliza kwa sababu nilihisi labda aliona misiba ile haikumuhusu...! Panapo msiba ni wako peke yako na sherehe ndiyo ya wote... kwahiyo unatakiwa tu kumsubiria rafiki wa kweli aje na asiyekuja huna sababu ya kuhoji kwanini hakuja... labda aanze kueleza mwenyewe kwanini hakuja!

Hapo umenena.
Na kwa mtazamo wangu wala Diamond hakutakiwa kujieleza.
 
Ujawah kuckia msanii amepangiwa melody za kuimba itakua ujui chochote kuhusu mziki !!

Mwengine nani ?
Kwani dully amesema kua ameumia diamond kukosa kumzika baba ake ?

Dully kasema wasanii wana roho za ajabu kwa kushindwa kumpa sapoti katika safar ya mwisho ya mzee wake

Ila nyie mashabiki marboro mnayaweza

Ungesikiliza interview ya dull clouds Fm, haikuhitaji akili za chuo kikuu kugundua alikuwa anamaanisha nini! Hahhah afu dully wa ajabu nyie eti kasema imemuuma diamond kutokuja kwani anampenda sana! (Yaani dull anampenda sana diamond! ) haya ni maajabu mengine lol!
 
Hapo umenena.
Na kwa mtazamo wangu wala Diamond hakutakiwa kujieleza.

Ifikie time watu wa karibu wa diamond wamshauri maswali ya kujibu na namna ya kuyajibu, unless anawatafutia waswahili cha kuongea, hili ni la muhimu sana kwa afya ya heshima ya kipenzi chetu diamond (kwa Wale tunaompenda na kumtakia mema) mi naamini humu wapo watu wa karibu na Diamond sana Akina Romy, Esma , kifesi na managers wake, kwenye swala kama hili hakutakiwa kutoa maelezo meeeeengi lakini alitakiwa kujibu technically! Cc Ruttashobolwa chige Dinazarde Kim nana
 
Unajua Diamond aliona labda akikaa kimya watu wangefikiri yanayo sema ni kweli na ukizingatia kuna watu walianzisha campaign ya kuhakikisha anaonekana ni mbaya..kwa asingeweza kukaa kimya na inaonekana alipigiwa simu na watu wa clouds nimesoma sehemu na anasema alipo pata taarifa alimpigia Dully simu na alisema yuko katika kipindi kigumu sana sema watu hawafahamu.

Kifupi nimegundua Dully ana zaidi ya hili la msiba.
 
Last edited by a moderator:
huyo dully nae anamatatizo baadala kumuenzi baba yke msiban yeye anapiga sensa kwan shoo hyo kwamba diamond angeongeza mashabiki#wat if zile post za insta zilikuwa za mda mfupi....nchi huru hii.....# dully ni bogas
 
Majibu haya hayakuwa ya lazima na wala hayakusaidia kabisa hasa kwa vile kila mtu anajua jinsi alivyokuwa akiponda raha huko vekesheni; ijulikane kuwa Diamond hakulazimika kuwapo msibani pale hasa kwa vile ulitokea wakati yeye alishakuwa commitment nyingine. Lakini alivyojibu ni kama vile aliweza kuwapo ila alipiga chenga hivyo sasa anataka kujustfy chenga zake. Ndiyo maana ya kuwa na meneja; Diamond ana meneja anayejua sana kujibu mambo kama haya, angemwachia yeye ndiye atoe majibu kwa sababu hata kama meneja akikosea huwa lawama zinaishiea kwake hazimfikii staa mwenyewe.
 
Back
Top Bottom