Diamond awatukana vijana wa Tanzania; 'wana njaa'!

Diamond awatukana vijana wa Tanzania; 'wana njaa'!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, msanii wa muziki na mmiliki wa biashara, ikiwemo WASAFIBET, ameamua kuwatukana vijana wa kitanzania kwa makusudi kwa kuchapisha tangazo lenye nia ovu ya kudhalilisha, kutweza na kubagaza utu wa vijana wa Tanzania. Ni dhahiri shahiri kuwa amewalenga vijana kwa kuwa wengi wao hawana ajira, hivyo wanategemea kubet ili wapate fedha za kujikimu.
View attachment 3206254
MAONI YANGU
Diamond amefanya kitendo kinachopaswa kulaaniwa na kila mtanzania mwenye utu, mpenda amani na anayezingatia na kujali maisha ya wengine, bila kujali hali zao za kiuchumi. Haikuwa na haja kuchapisha tangazo hili la kidhalilishaji, kibaguzi, kichochezi na kibagazaji. Kuna namna nyingi za kutangaza lakini sio kwa udhalilishaji wa kiasi hiki. Naomba serikali iingilie kati kwa kumuonya huyu kijana aache dharau kwa vijana wenzake na pia aondoe hilo tangazo, kuwaomba radhi vijana wenzake na kuapa kutorudia kosa kama hili wakati mwingine.

Nawasilisha.
Ni perception yako tu Wala hakuna tusi apo....
 
Japokuwa mtajitetea ila wengi wenu mnanjaa mnaobet
Kubet ni mchezo wa kujifurahisha sio wa kutafuta utajiri mkuu. Kubet sio ajira rasmi inayotambulika ktk nchi hii. Ni sawa na kazi ya urefarii. Marefarii wote wanakuwa na kazi zao. The same case applies to betting mkuu.
 
Hakuna hoja mle, ni inferiority complex tupu..!!
Inferiority complex? Mm huwa sijifananishi na mtu yeyote mkuu. Naongea ukweli bila kumumunya maneno wala kumuonea mtu yeyote.
 
Mkuu umenisoma kwa mhemko. Hebu rudia kusoma kwa ufasaha utanielewa ninachomaanisha. Kutumia njaa za watu kuwabagaza ni utovu wa heshima na utu kwa binadamu wenzako.
It's just an advert, NJAANUARY is very common term in Kanairo. Wakikuyu kutamka JA it sounds NJA then like spicing up the common toughness of January you know the festival season spendings plus the January school bills so they popularized NJAANUARY.
NJAA + JANUARY = NJAANUARY.
No insults there whatsoever, just chillax dude.
Kama unalifanyia hilo tangazo 'promo in disguise' then you're doing the right thing kwa sababu publicity comes in different forms.
 
Mbona Kama wewe ndo umemwelewa vibaya maana sijaona alipotukana
Mkuu amewatukana vijana indirectly kupitia kwenye tangazo lenye nia ovu. Hebu rudia kusoma utaelewa vizuri mkuu.
 
Ninaweza kuwa nina njaa lakini kamwe mtu asitumie njaa yangu kunibagaza mkuu.
Hawa nao waliwatukana akina nani?

1737523364915.png
1737523427046.png
1737523475845.png
1737523549318.png
1737523611762.png
1737523674953.png
1737523779487.png
1737523857489.png
1737523965619.png
 
Back
Top Bottom