Diamond awatukana vijana wa Tanzania; 'wana njaa'!

Diamond awatukana vijana wa Tanzania; 'wana njaa'!

Tatizo linaanzia pale ulipo interpret Hilo neno Kwa hisia zako zinavyokutuma
Sio hisia mkuu. Hii ni fact. Hata wewe ukisoma kwa kutulia utagundua kuna shida mahali.
 
Shida sio diamond na tangazo lake,shida ni sisi wenyewe, hatujui fasiri sahihi ya misamiati ya kiswahili. kabla hujamlaumu diamond nenda kamusi ya kiswahili sanifu ukapekue maana ya neno njaa kisha urudi hapa umpe diamond maua yake na samahani zisizo na idadi. ni hayo tu bhanandugu.
Tafsiri ya neno njaa inajulikana lakini kutumia njaa za watu kuwabagaza hairuhusiwi.
 
Naelewa hilo mkuu
Ila watu fulani wanawaaminisha
Wati betting ni ajira 😄

Ova
CCM ndio wanawaaminisha kuwa kubet ni kazi na kuwaita maofisa ubashiri.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, msanii wa muziki na mmiliki wa biashara, ikiwemo WASAFIBET, ameamua kuwatukana vijana wa kitanzania kwa makusudi kwa kuchapisha tangazo lenye nia ovu ya kudhalilisha, kutweza na kubagaza utu wa vijana wa Tanzania. Ni dhahiri shahiri kuwa amewalenga vijana kwa kuwa wengi wao hawana ajira, hivyo wanategemea kubet ili wapate fedha za kujikimu.
View attachment 3206254
MAONI YANGU
Diamond amefanya kitendo kinachopaswa kulaaniwa na kila mtanzania mwenye utu, mpenda amani na anayezingatia na kujali maisha ya wengine, bila kujali hali zao za kiuchumi. Haikuwa na haja kuchapisha tangazo hili la kidhalilishaji, kibaguzi, kichochezi na kibagazaji. Kuna namna nyingi za kutangaza lakini sio kwa udhalilishaji wa kiasi hiki. Naomba serikali iingilie kati kwa kumuonya huyu kijana aache dharau kwa vijana wenzake na pia aondoe hilo tangazo, kuwaomba radhi vijana wenzake na kuapa kutorudia kosa kama hili wakati mwingine.

Nawasilisha.
Umeandika utumbo mtupu, bandiko limedhihirisha inferiority complex yako + low self-esteem.
Tafuta hela LAINISHA NJAANUARY YAKO.
 
Back
Top Bottom