Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 33,643
- 36,090
Ukiwa huna kitu,Katika hali isiyokuwa ya kawaida, msanii wa muziki na mmiliki wa biashara, ikiwemo WASAFIBET, ameamua kuwatukana vijana wa kitanzania kwa makusudi kwa kuchapisha tangazo lenye nia ovu ya kudhalilisha, kutweza na kubagaza utu wa vijana wa Tanzania. Ni dhahiri shahiri kuwa amewalenga vijana kwa kuwa wengi wao hawana ajira, hivyo wanategemea kubet ili wapate fedha za kujikimu.View attachment 3206254
MAONI YANGU
Diamond amefanya kitendo kinachopaswa kulaaniwa na kila mtanzania mwenye utu, mpenda amani na anayezingatia na kujali maisha ya wengine, bila kujali hali zao za kiuchumi. Haikuwa na haja kuchapisha tangazo hili la kidhalilishaji, kibaguzi, kichochezi na kibagazaji. Kuna namna nyingi za kutangaza lakini sio kwa udhalilishaji wa kiasi hiki. Naomba serikali iingilie kati kwa kumuonya huyu kijana aache dharau kwa vijana wenzake na pia aondoe hilo tangazo, kuwaomba radhi vijana wenzake na kuapa kutorudia kosa kama hili wakati mwingine.
Nawasilisha.
1. Hata mtu akicheka tu unaona anakucheka wewe.
2. Hata mtu akikuangalia tu unaona anakuangalia kwa dharau.
3. Hata mtu akipita kasi na IST yake, unaona anakunyanyasa kisa huna gari.
4. Hata mtu akiwa anapiga stori na mwingine, lakini mkakutanisha macho, utaona anakuangalia jicho la madharau.
etc etc...!!
By the way, hakuna asiyejua kuwa Januari almost zote, kwa wengi kunakuwa na njaa kali sana. Sijaona tusi kwenye tangazo lake, isipokuwa ni INFERIORITY COMPLEX tu ya mtoa mada..!! Au chuki tu zisizo na kichwa wala miguu.