Katika hali isiyokuwa ya kawaida, msanii wa muziki na mmiliki wa biashara, ikiwemo WASAFIBET, ameamua kuwatukana vijana wa kitanzania kwa makusudi kwa kuchapisha tangazo lenye nia ovu ya kudhalilisha, kutweza na kubagaza utu wa vijana wa Tanzania. Ni dhahiri shahiri kuwa amewalenga vijana kwa kuwa wengi wao hawana ajira, hivyo wanategemea kubet ili wapate fedha za kujikimu.
View attachment 3206254
MAONI YANGU
Diamond amefanya kitendo kinachopaswa kulaaniwa na kila mtanzania mwenye utu, mpenda amani na anayezingatia na kujali maisha ya wengine, bila kujali hali zao za kiuchumi. Haikuwa na haja kuchapisha tangazo hili la kidhalilishaji, kibaguzi, kichochezi na kibagazaji. Kuna namna nyingi za kutangaza lakini sio kwa udhalilishaji wa kiasi hiki. Naomba serikali iingilie kati kwa kumuonya huyu kijana aache dharau kwa vijana wenzake na pia aondoe hilo tangazo, kuwaomba radhi vijana wenzake na kuapa kutorudia kosa kama hili wakati mwingine.
Nawasilisha.