Diamond awatukana vijana wa Tanzania; 'wana njaa'!

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, msanii wa muziki na mmiliki wa biashara, ikiwemo WASAFIBET, ameamua kuwatukana vijana wa kitanzania kwa makusudi kwa kuchapisha tangazo lenye nia ovu ya kudhalilisha, kutweza na kubagaza utu wa vijana wa Tanzania. Ni dhahiri shahiri kuwa amewalenga vijana kwa kuwa wengi wao hawana ajira, hivyo wanategemea kubet ili wapate fedha za kujikimu.
1737285612479.png

MAONI YANGU
Diamond amefanya kitendo kinachopaswa kulaaniwa na kila mtanzania mwenye utu, mpenda amani na anayezingatia na kujali maisha ya wengine, bila kujali hali zao za kiuchumi. Haikuwa na haja kuchapisha tangazo hili la kidhalilishaji, kibaguzi, kichochezi na kibagazaji. Kuna namna nyingi za kutangaza lakini sio kwa udhalilishaji wa kiasi hiki. Naomba serikali iingilie kati kwa kumuonya huyu kijana aache dharau kwa vijana wenzake na pia aondoe hilo tangazo, kuwaomba radhi vijana wenzake na kuapa kutorudia kosa kama hili wakati mwingine.

Nawasilisha.
 
View attachment 3206254

Vijana poleni kwa kubagazwa!
 
Pole kakugusa

Ila neno hilo nalo kiroho kulikubali ni kujitafuatia shida..

Nje ya Mada kidogo poo.. ☺️
Diamond nimempenda kwa juhudi ya kujifunza kimombo na sasa anamwagika haswaaaaa

Hongera kubwa kwake..
Mkuu kumwagika kimombo kwa Diamond kunahalalisha matusi anayowatukana vijana wenzake?
 
Back
Top Bottom