Watawala wakiona mambo hayaendi au hawana la maana walilolifanya au wakiona maisha magumu huwatafuta hawa kina diamond kupumbuza wananchi na kuwasahaulisha matatatizo waliyonayo. Juzi tu hapa alikuja znz kukata viuno kwa mualiko wa Mwinyi.
Sasa na wao kina diamond kwa kua ni part of conspiracy, wanajiona wana immune ya kutokufuata sheria na kua watawala watawalinda wakisahau kua watawala hawana urafiki wa kudumu.
Kila anayefanya uovu au anayeshirikiana na muovu au kuushiriki uovu, ni lazima, na ni haki kwake kuguswa kwa kiasi fulani na uovu alioshiriki kuusimika.
Wasanii kama Diamond, wanatumika na watawala/CCM kuwapumbaza wananchi badala ya kuwaelimisha.
Haya ni madogo, kuna siku atalipua zaidi ya haya malalamiko juu ya jambo dogo. Analalamikia kufungiwa bank account, na kuvamiwa kwa kituo chake. Wenzie zilifungiwa bank accounts zao, wakafungwa na wao wenyewe, na kesi za uhujumu uchumi juu yake.
Uovu ni imani isiyochagua wa kumtendea uovu. Amwulize Zakaria, aliyekuwa mfadhili mkubwa CCM kanda ya Ziwa, alilipa posho za wajumbe wa mkutano mkuu, alitoa mabasi yake kuhudumia kampeni, lakini mwisho wake, mke wake na yeye mwenyewe waliishia mahabusu kwa mwaka mzima, na pesa kutaifishwa. Uovu ni imani isiyochagua wa kumtendea uovu, na uovu kwa aliyesaidia kuusimika, ni haki na halali kwake.