Diamond dhidi ya TRA tuko naye, ila kauli zake!

Diamond dhidi ya TRA tuko naye, ila kauli zake!

ulichokoment utoto ni wewe maana hujui chadema wameegemea mlengo gan haya tueleze huyo domo mkwepa kodi anamalengo yapi kuhusu katiba mpya ili kuleta justice and tranquility nchini maana umetolea mfano wa mainstream parties za uingereza visa viz other political or associations ambao kwa pamoja walitaka brexit ila katika modalities tofauti na kwamba labour,conservatives hawakutaka waungane nao swali ni Je huyo mkwepa kodi amewahi kupigania agenda ya katiba mpya ambayo kimsingi ndio itaondoa ujinga wote unaofanywa na mamlaka za serikali eg latra,police,tmda,tcra,nec,TRA na taasisi zingine zenye kufanya ujinga.
Leo hii huyo mkwepa kodi analalamika kufungiwa account zake na TRA huku akijua TRA wamefanya hivyo kwa mujibu wa sheria ambazo ni za hovyo au mbovu pamoja na katiba ya hovyo, unafikir kama kungewa na katiba bora huo ujinga wa TRA wa kufunga account za watu bila wao kujua ungefanyika? Maana angeweza kuwashtaki mahakaman na angewashinda lakin leo ajaribu kama atafanikiws huko mahakaman hii yote ni kwasababu ya katiba ya hovyo so chadema hawapiganii maslahi binafs bali maslahi ya kila mtanzania, huyo mkwepa kodi wamemtekenya kidogo tu ameanza kujambajamba angepigwa risasi hata moja je si angekufa kabisa.
Haya amefungiwa account zake na TRA kwa akili zake za kijinga anaandika kuwa ANAFANYIWA HIVYO KAMA PALE TRA KUNAWAPINZANI hizo ni akili au matope anafikir kuwepo kwake ccm anaimmunity au privilege kwenye kulipa kodi.
Na wewe kwa ujinga wako unafikir huyo mkwepa kodi anaprivilege ya kutokulipa kodi, nasema hivi TRA wahakikishe analipa kodi na waendelee kufunga viaccount vyake uchwara mpaka ajue kuwa KATIBA MPYA NI SASA NA YEYOTE ATAKAE PINGA NI BORA EITHER ATOWEKE AMA AUNGANE maana asipofanya hivyo lolote litakalomkuta kutokana na katiba mbovu asilalamikie mitandaoni ili kutafta huruma bali apambane mwenyewe.

Mkuu siasa hazipaswi kuchukuliwa personal. Ni muhimu kutenganisha watu na siasa. Hapa ndipo ule msemo "hakuna rafiki au adui wa kudumu bali agenda" huigia kazini.

Diamond kutendewa ndivyo sivyo si haki ila sasa haya anayosema ndipo ulipo utoto wake ulipo.

Au nasema uongo?
 
Kauli inaonyesha unaweza kuwa msanii mkubwa lakini ni empty set. Alipe tu Kodi, watu waendelee kula plau.
 
Jongwe kasema wenye akili wataelewa.

Ni upumbavu kudhani chama Cha upinzani ndio kimekukalia kooni.

LIPA KODI hio halafu tutajidiliane mambo magumu kwa mustabali wa nchii hii sio kukata mauno jukwaani na kusema "eti mumeipende wenyewe" haya Sasa " hamnywi sumu , hamjinyongi" ila maumivu mnayaoata vile vile.

Siku mkianza kutumia akili zenu barabara! Itapendeza sana

Kwasasa LIPA hizo Kodi wanachi wa kule mahezanulu wapate maji ya bomba na umeme.
 
Au kama vipi wekeni upinzani hapo TRA wote wazifuatilia Kodi vizuri[emoji1787][emoji1787]
 
TRA kama ilivyo kwa Polisi, LATRA, Takukuru, EWURA, TCRA na wengine wa namna hiyo malamiko dhidi yao yanajulikana.

Hakuwahi kusikia malalamiko ya watu wengine dhidi ya mamlaka hizi ikiwamo TRA?

Haihitaji kumiliki basi kujua ndivyo sivyo za LATRA, au kuwa na gari au kituo cha mafuta kujua fyongo za EWURA.

"Nani wamekuwa na uthubutu wa kuwaongelea wahanga wa mamlaka hizi bila kujali kulipiziwa visasi? Hii ikiwa hata bila ya wao kuwa wameguswa moja kwa moja? Wengine ninyi si imekuwa kusema hadi mkaliwe kooni wenyewe tu?"

View attachment 2465114

"Ubinafsi wenu si ndiyo unaowapa nguvu miungu watu hawa waliopaswa kukusikiliza wewe na badala yake wapo kukunywesha maji kwenye karai?"

Kwani yeye alidhani kelele za wapinzani siku zote zilikuwa kuhusiana na nini kumbe? Kwani hakujua kwanini tulishangaa na wimbo wake "baba letu?"

Tofauti yao na yeye kwenye hili analoliongea sasa si ni kuwa leo yeye ameguswa tu? Wenzake kwao sera zote za kigandamizi ni mwiba usiovumikika hata kama wao haziwagusi moja kwa moja.

Na huu sasa si ndiyo uzalendo?

Kataa wahuni kwa Tanzania ya haki.

Wahuni siyo watu wazuri!
----------

Mamlaka zinapotumika kukandamiza watu
Napenda kulipa Kodi ila TRA hawana credibility kwenye maisha yao ya kawaida na maendeleo yao mmoja mmoja tunawajua wanaojilimbikizia Mali wasizofanana nazo Kwa vipato vyao.
 
Diamond aliiamimi upendeleo wa kutolipa kodi aliopewa kutokana na yeye kutumika kuwapumbaza Watanzania kupitia fani yake ya muziki, ungeendelea milele?

TRA wafuatilie kodi zote ambazo hazikulipwa, ikiwa ni pamoja na za miaka ya nyuma ambapo alikuwa halipi.
Wafuatailie kabrasha zote

Huyu dogo atakua mkwepakodi mkubwa
 
Ndiyo maana kawambia pale TRA kuna wapinzani; na kwamba sababu za yeye kufutwa ni kwa sababu aliinga mkono CCM. Hivyo wapinzani wanamchukia, na mawakala wao kwenye serikali wanatumia nafasi zao kumkomoa. Tunajua TRA wamejaa wachagga ambao wengi ni CHADEMA NA WANAFANYA HIVYO KWA KIBURI KABISA KWA KAULI MBIU- MLIICHAGUA CCM NGOJA MUONE
Lipa KODI acha kuandika ujinga
 
Mkuu hujawahi kukutana na hao TRA wanamaneno ya shombo na wanafanya kwa kauli mbiu SI MLIICHAGUA WENYEWE CCM sasa kwa kauli hiyo wewe unaelewa nini?
Acha ukabila , huo ni upumbavu unashindwa kulipa Kodi unajishika na chama au ukabila,
Hizo akili zako Zina matatizo,
Kodi ni kwa manufaa ya taifa zima
 
Acha ukabila , huo ni upumbavu unashindwa kulipa Kodi unajishika na chama au ukabila,
Hizo akili zako Zina matatizo,
Kodi ni kwa manufaa ya taifa zima
Unajua nakuheshimu sana na sababu kubwa inayonifanya ni kuheshimu ni kuwa wewe ni mjinga sana. Ungekuwa unatakka kulika kodi usingepinga tozo?
 
Awasiliane na wakubwa wa chama chake cha akina Kanumba maana TRA wanafuata maelekezo kutoka kwa mkali Lucifer
 
Jifunzeni kupambana vita kwenye maisha kwa mikakati yenu.

Uwe individual au taasisi kufikia malengo yako ni jukumu lako.

Usilazimishe wengine wapambane kwa kufuata strategy yako.

In life mnaweza mkawa na objective moja lakini mkapishana kufikia lengo, its OK.

Nakumbuka wakati wa Brexit wanasiasa wa mainstream parties both pro and anti Brexit (Labour, Conservatives na Lib-Dem) waliunga kwenye campaign zao.

Lakini hizo team mbili za mainstream parties hawakutaka kabisa wanasiasa wa vyama vingine au taasisi zingine zenye objectives hizo hizo; ambazo wanatumia racist propaganda au nationalism idologies kuungana nao waliwaacha wapambane kivyao.

CHADEMA na viongozi wake lazima waelewe ni utoto kulazimisha watu wasio wanasiasa ku support movement zao hadharani. Jukumu lao ni kushawishi wachague wanachopigania wakipata nafasi ya kuwapigia kura, lakini uwezi kulaumu raia wakipata shida mbona ukuunga mkono jitihada za chama kwenye agenda husika acha yakukute huo ni utoto.
Mkuu mbona sijaona ubaya wowote wa chadema. Kiuhalisia hapa diamond ndo kaukosea upinzani maana kusema utafikiri pale tra kuna wapinzani inaweza kutafsiriwa vibaya
 
Kwani shidaau madai ya huyu Bwana ni yapi....TRA wana mwonea au issues za tax zomekaaje kwake,
Kiufupi asipanic akae na hao viongozi wa TRA na Wenye mamlaka ya fedha wajue namna ya kumsaidia lakini siyo kubwatuka huku mtandaoni......kama kaweka uwekezaji mkubwa wenye mabiliion ya fedha basi waangalie namna ya kulipa Kodi kwa ufasaha
Vilevile nimegundua huyu kjana Hana washauri wazuri kwenye maswala ya fedha
 
Mkuu mbona sijaona ubaya wowote wa chadema. Kiuhalisia hapa diamond ndo kaukosea upinzani maana kusema utafikiri pale tra kuna wapinzani inaweza kutafsiriwa vibaya
Kwa CDM neno “upinzani” lina connotation la vyama vya siasa; bila ya kujali limetumika katika mazingira gani.

Sometimes neno liangaliwe katika context ya argument, nadhani upinzani kwa Diamond alimaanisha kama vile wasafi inaugomvi na TRA.

It doesn’t make sense kuwahusisha upinzani wa vyama vya siasa na madai yake ya TRA. Tatizo CDM kutaka kujipachika kwenye kila mgogoro ndani ya jamii; that’s my take.
 
Kwa CDM neno “upinzani” lina connotation la vyama vya siasa; bila ya kujali limetumika katika mazingira gani.

Sometimes neno liangaliwe katika context ya argument, nadhani upinzani kwa Diamond alimaanisha kama vile wasafi inaugomvi na TRA.

It doesn’t make sense kuwahusisha upinzani na madai yake ya TRA ni CDM kutaka kujipachika kwenye kila mgogoro ndani ya jamii; that’s my take.
Asante sana mkuu hata mimi pia umenifungua akili.
 
Diamond ana maana gani kusema anajiuliza kama pale TRA kuna mtu wa chama pinzani?

Kwamba kwake wapinzani ndio wenye roho mbaya?

Kwa hiyo kauli yake, huyu mtu hata kama yanamkuta lakini ni kama bado ana mentality ya kujipendekeza kwa CCM, ameleta suala lake public ili kutafuta huruma tu kwa watanzania.
Kama hesabu zake ziko sawa ana hofu ya nini? Hajui kwamba kadhia kama hizi zinawakuta watu kila siku. Yeye analipwa hela nje ya nchi ananunua, anawekeza, lazima wamhoji vyanzo vyake na wadai Kodi zao
 
Back
Top Bottom