Diamond hawa ndio wabongo, chukua ushauri wangu

Diamond hawa ndio wabongo, chukua ushauri wangu

Ndio ujue marafiki wa kweli na wa uongo ukipata misuko suko,huyu maatope ni shabiki namba moja wa domo lakini leo kamuhama hhhhhaaaaaaaaaaa

Naona leo sir Maatope anamruka kimanga homeboy wake waliokula wote utumbo wa kuku na supu ya mapupu.
 
Last edited by a moderator:
Poor mind set inamalza watz weng sana , mimi hv vitu huwa vinanisikitisha sana kuona jinc watz weng walivojaa negative attitude, ss cjui ni hzo dv5 au ndo vp?????? Am speechless

huu ujinga nilidhani ni kwenye siasa tu, vijana wetu wasomi wa vyuo vikuu ndio wanaongoza huu uswahiliswahili..
 
Yaani umejipinda kuandika gazeti zima wakati dangote akikuona atasema hana hadhi ya kuongea na wewe
 
Kiba aliposema alimsaidia Diamond kurekodi pale kwa Bob junior haikua shida, ila Diamond kusema atamsaidia Kiba wafanye kolabo imekua nongwa! WABONGO WASAHAULIFU SANA!
 
Kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusu Diamond haswa kipindi hiki akionyesha mafanikio makubwa kimuziki.

Wakati yeye akipambana kupiga hatua kuna wanaopambana kuakikisha hasogei na anarudi chini.

Mimi nimejitolea kumpa ushauri wa bureeee kabisa akiwa kama mdogo wangu.

Ukiangalia kelele zote na matukio ya hivi karibuni utagundua hakuna ishu ya maana sana ya kumchukia diamond ila ni roho mbaya zetu waswahili...Diamond kafanikiwa sana kuna watu linawauma ili jambo yani inawauma inawauma ata wangepata nafasi ya kumuwekea sumu wangemlisha ..Jamani hakuna mtu mbaya dunia hii kama mswahili ndio maana mimi uwa sipendi kuwa karibu na mtu mswahilimswahili,nchi haiendelei sababu ya roho mbaya za kiswahili.

Mswahili anaweza kukuchukia ata hakikosa sababu ya kukuchukia na yote hii sababu ya roho mbaya unakuta mtu ana roho mbaya mpaka akicheka kuna taswira inatokea kama analia vile.

Tukifanya leo tafiti lazima tutakuta asilimia 98 ya waswahili either ni wachawi au wana tabia zote za kichawi.mbongo yupo tayari kuchoma nauli hapa mpaka nachingwea ili akakuroge kisa umenunua gari mpya, ukimpa challenge anunue la kwake atakwambia ye hapendi makuu ila atakuchukia wewe ulieamua kupenda vya kwako

Mbongo atakuchukia ata kwa kumzidi kuvaa vizuri, awezi kujipanga nae atoke smart kukuzidi ila atataka muwe wote wachafu... We ukitaka kumpima mswahili imani mkute anakula alafu akukaribishe msosi na wewe ukaribie utaona uso unavyombadilika na roho yake mbaya.

Mtu anaibuka uko alipoibuka anakwambia dogo ana dharau siku hizi, lakini ukitafakari vizuri hapa tafsiri ya neno dharau ni mafanikio....yaani tatizo dogo ana mafanikio siku hizi.

Wabongo tuna roho za kwa nini ndio maana hatuendelei kamwe, sijui tulitoa wapi hizi roho ama ni ule ujamaa ulituaribu au vipi ! ila kama ni ujamaa wenzetu China mbona wanatumia ujamaa kumfanyia roho mbaya mtu anayerudisha nyuma maendeleo ndio maana ukilisha watu drugs wanakunyonga.....sisi wabongo ujamaa wetu tunatumia kuwafanyia roho mbaya wanaopiga hatua mbele. Yani kwetu mtu akipiga hatua anafanya makosa.

So dogo diamond mimi nakushauri utulie ufanye mambo yako kimpango wako wavumilie tu awa waswahili, ila ishi nao kiakili sana. Jiamini fanya kazi nzuri zaidi watachoka tu na watakubali matokeo.

Watu wanatengeneza maneno kisha wanayapenyeza kwenye media ili kukuharibia, leo mtu anakuja na maneno eti umedharau hotel za mbeya ukimuuliza hizi kauli ulizitoa wapi hana cha kusema, kama umelala hotel za Kigoma utadharau vipi hotel za Mbeya? majuzi hapa umepiga show Tunduma inamaana huko sio Mbeya?

Unakuta mpaka radio zinaingia kwenye ujinga huu unamuuliza mtu swali akitoa majibu, mnayarusha majibu bila swali kisha mnasema haya maneno Diamond kayasema kwa Kiba. Yote ni kufitinisha tu.

Imefikia kipindi watu wanachukia mpaka wanazomea, lakini sio ishu mtu ashushwi kwa kuzomewa ingekuwa ni hivyo Chege na Temba wangeshapotea zamani maana walishapigwa mpaka makopo stejini enzi za Wanaume family na Halisi..Leo halisi wako wapi? Ata AY anayeheshimika sana kwa sasa ameshazomewa na kupigwa makopo enzi za East coast vs Temeke.

Pia chukua tahadhari na Kiba, Kiba wa sasa anamtumia diamond kupata kurudi kimuziki kiukweli bila Diamond hakuna Kiba kwa sasa but kuna Diamond bila Kiba...Kiba kwa sasa hawezi kusimama kwa kazi zake ila kwa jina la Diamond tu.

Tangu Kiba arudi kazi yake ni kuzunguka kwenye media kueleza ubaya wa Diamond, media zote kuanzia radio mpaka Tv amezimaliza akionyesha wewe ni mbaya.

Mimi nakushauri achana na kiba wewe concentrate na muziki wako kwanza mfanye kama haexist vile.

Hakuna ataekuwa juu milele ila hatushushani kwa style ya kampeni, nature ndio uwa inaamua. Muda wa mtu ukiisha haitaitajika nguvu yoyote hatutaanza kumuona kwenye headlines, hatutaskia nyimbo nzuri n.k nature itaamua.

Siku zote ridhki anayegawa ni Mungu tu hakuna binadamu anayeweza kunyang'anya ridhki ya mtu. Mungu ndio anajua nani ampe nini ndio maana yule anapewa sauti nzuri wewe ukapewa nyota. nyota ikiwaka sio rahisi kuizima ndio maana yote yaliyotokea watu wanazungumzia Diamond tu sio nani kafunika wala nini habari bado ni wewe .

Zidane alikuwa bonge la mchezaji lakini matangazo mengi na project za hela alizibeba Beckam ndio ridhki iyo kila mtu na yake.

Nakushauri fanya kazi kwa juhudi zote wataelewa tu, tena kwa sasa ndio uzidishe mara mia hasikuvunje mtu moyo bongo fleva bado inakuhitaji mno. na mashabiki wako wamezidi kukupenda amini usiamini.

Kuna wataokupenda ukifa kama Kanumba na Amina chifupa

umesema yote salute
 
ukishakusanya hizo sababu umfikishie"tajiri Dangote" muambie aachane na mahaters hao, wana wivu na wala hawawezi kumshusha kamwe
Ahsante mkuu maatope... nalazimika kutumia zile akili za kiutu uzima! Hilo la kwamba hawawezi kumshusha wala halina shaka lakini kama wanaweza, busara ipo wapi basi??!! Yaani mnataka mtu ashuke kwa kulazimisha na sio kwa kushindwa.... aaaargh! Alipopanda wala si kwamba kuna mtu alishushwa na mashabiki na hivyo, hata atakaposhuka atafanya hivyo kwavile tu hakuna msanii anayebaki No. One milele... Hata Michael Jackson wa 1980's si yule wa 1990's and 2000's... itakuja kuwa Diamond!
 
Last edited by a moderator:
Kiba aliposema alimsaidia Diamond kurekodi pale kwa Bob junior haikua shida, ila Diamond kusema atamsaidia Kiba wafanye kolabo imekua nongwa! WABONGO WASAHAULIFU SANA!
YOte wanayakumbuka sema tu nongwa zimewazidi! Ajabu zaidi, wengi wao ni vijana tu lakini wana chuki, wivu na vijiba utafikiri vibebe vizeee!
 
Maajabu mengine ya haters wa Diamond haya hapa... hao wanaomegwa hawajalalamika unakuja kulalamika wewe.... eh!!!! Cha ajabu zaidi sijasikia Diamond kamega vitoto vya shule... sasa wakimegwa akina Wolper, Penny, Kidoti wewe kinakuuma nini? Yale yale... oh, anajitangazia kwamba amemtoa Davido... malalamika nyinyi wakati Davido mwenyewe hajalalamika!!!

Maajabu mengine haya huku.... Unapamba mtu ata hajui kama ilizaliwa au ulishushwa achukiwe,aonewe wivu,apondwe wewe kinacho kukeleketa kwa moyo ni nini... Si huishi kivyavyo... Au unataka moyo wangu ufate wa kwako... Alizomewa ndiooo... Tena saaana... Ja kuja kujibu kwa jazba kama vile umepaliwa na soda ya tangawizi... Uyo unaempenda anajua km unaexist... Kama wewe umependa ni wewe bana
 
Naona leo sir Maatope anamruka kimanga homeboy wake waliokula wote utumbo wa kuku na supu ya mapupu.
sijamruka mwana, kaniuzia sana vocha na keep change alikuwa anzipata sana toka kwangu ila naungana na wadanganyika wenye hasira wanaotaka kumrudisha dogo kwenye reality maana mabega yamezidi kichwa sasa...akishaacha dharau mbona sana tu, nyimbo zake mbona kali
 
Maajabu mengine haya huku.... Unapamba mtu ata hajui kama ilizaliwa au ulishushwa achukiwe,aonewe wivu,apondwe wewe kinacho kukeleketa kwa moyo ni nini... Si huishi kivyavyo... Au unataka moyo wangu ufate wa kwako... Alizomewa ndiooo... Tena saaana... Ja kuja kujibu kwa jazba kama vile umepaliwa na soda ya tangawizi... Uyo unaempenda anajua km unaexist... Kama wewe umependa ni wewe bana
Mapya haya... wapi nimempamba mtu?? Jibu swali, kumegwa wamegwe akina Wolper, wewe kinakusumbua nini? Eti najibu kwa jazba... jaba itoke wapi... hivi hujajishtukia kwamba ni wewe ndie uliye-panic??
 
Mapya haya... wapi nimempamba mtu?? Jibu swali, kumegwa wamegwe akina Wolper, wewe kinakusumbua nini? Eti najibu kwa jazba... jaba itoke wapi... hivi hujajishtukia kwamba ni wewe ndie uliye-panic??

Nijibu swali wewe ni mwalimu???
 
Kwanin yote haya yanakuja baada ya diamond kufunukwa show ya fiesta..

m nadhan mmepungukiwa uelewa tu,kila msanii ana mashabiki wake,inawezekan kwenye fiesta mashabik weng walikuwa wa alikiba..au walimshangilia sana kwasabab walimmis sana kwenye jukwaa la fiesta tofaut na diamond ambaye kila mwaka yupo..

CHA MSING #TEAM_DIAMOND MUANGALIE NI WAPI MLITEREZA SIKU ILE NA KUJIPANGA UPYA KULIKO HII STYLE YA KUTAKA KULAZIMISHA MASHABIKI WAMSHABIKIE DIAMOND NA WASIPOFANYA HIVYO ETI WANA WIVU NA MAENDLEO YAKE,pathetic.!!!kwanin wasimzomee MBWANA SAMATA.???au kwa ujinga wenu mnadhani diamond ni kijana pekee maarufu mwenye maendleo hapa TZ.!!

Kwanini hawakuwahi kumzomea MR.NICe.!?

Nimesikitishwa na maneno ya management ya diamond kusema eti hao watu waliandaliwa,how on earth.!!!ina maana alikiba aliuziwa tiket zote kwa jumla ili watu waingie wamzomee chibu.!!acheni hzo,angezomewa ali ndo ingekuwa halaki,.??

Kama hamjajua watu wamechoshwa na vituko vya diamond nje ya mziki,refer to JUSTIN BEIBER..
 
Back
Top Bottom