Ahaa, kumbe hivyo.
Nakubaliana nawe kabisa.
Ali Kiba tatizo lake ndilo hilo. Nishawahi kusema hapa.
Na mimi siwezi kusem kwamba mtu ambaye muziki anaujua lakini tatizo hajui/hawezi/hataki kujipromote, siwezi kusema mtu huyu haujui muziki zaidi ya mtu ambaye kimuziki anamzidi, ila anazidiwa kwenye mambo ya promotion na ku hustle.
Ali Kiba mtoto wa Kigoma, ana uMwinyi Mwinyi fulani wa Kigoma wa kutegemea kudra na kipaji chake. Mambo ya "Inshallah, if it was meant to be, it will be". Kuna kipindi kirefu anaweza kujificha tu anafanya mambo yake.Husikii wimbo mpya wala collabo.
Diamond mtoto wa Tandale, kila siku kwenye magazeti, kujichanganya etc.
Kufikiri kwamba kumzidi mtu promo ni kumzidi muziki ni sawa na kusema bidhaa fulani ni nzuri zaidi ya nyingine kwa sababu inatangazwa sana.