Diamond kwa sasa hana Baba, ukweli mchungu

Kufuatilia pages zote za mjadala naona uvivu, ila ningependa kuuliza tu ndugu zangu! Hivi bado hakuna aliye-post ile picha ya Mzee Abdul akiwa na Mama Diamond pamoja na Diamond mwenyewe?! Nazungumzia ile picha ambayo Diamond anaonekana kakubwa kidogo ambayo wanaoi-post wanataka kutuambia "si huyo hapo Diamond na baba yake, sasa alimtelekeza wapi"!!

Diamond na Baba yake ni case study humu ila inahusu jamii nzima
 
Mimi mwenyewe sijalelewa na baba na hivyo namwelewa sana na Diamond.

Ila sasa tofauti yangu inakuja hivi, kwanini humtunzi Mzee Abdul halafu unamtunza Uncle Shamte [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Shamte anamtunzia mamaake [emoji28][emoji28][emoji28]
 
mzazi ni mzazi tuu. tatizo ni ujinga ujinga anaojazwa bwana naseeb na watu wanaomzunguka ukiwemo mtoa uzi. Diamond ni muislam,na Uislamu hauna mafunzo hayo wala hautoi fikra za namna hiyo kwa waumini wake. kama mshua alizingua kwenye malezi yako na sasa hivi anajutia, ni sawa, kwa sababu binaadamu Tumeumbiw makosa na shetani ndio kiongozi wa msafara huo wa kukosea, aidha kwa bahati mbaya ama kwa kukusudia. na kutubu piah ni sehemu ya maisha yetu, samehe saba Mara sabini... kama naseeb ni muislam na anaishi kwa misingi Ya dini hiyo(😁bt in reality hafuati misingi na taratibu za dini yake) , basi akae chini na ajitafakari juu ya mahusiano yake na Baba yake. mwenye wadhifa timilifu wa hukumu ni Mwenyezi mungu peke yake...

tenda wema kulipia ubaya ...
 
Wengi wenu hamjui ukweli kuhusu baba yake na diamond platnum ila kuna mengi anayo yaongea ni uongo na machache yanaweza kuwa na ukweli.
Kwa mimi ambae namfahamu vizuri yule mzee na alikua jirani yangu kweli ukiwa na mzazi kama yule ni shida,kwanza mzee kutwa akishapata pesa ,anashinda kwenye vibanda vya gongo.Mzee yule akikosa pesa ya kwenda kwenye hivyo viringe anajifanya anaumwa na kumlaumu mwanae kuwa hamsaidii na mguu unamsumbua lakini yote ni uongo ana matumizi mabaya ya pesa na mnywa gongo mbobezi.kwa hiyo amegundua akilalamika kwenye vyombo vya habari wake zake wa zamani wa diamondakiwepo wema,hamisa na wengineo wanamsaidia kumpa pesa kwa huruma zao lakini kipindi hicho hawajui ukweli sahihi
Diamond kwann asimchukue babaake akae nae tuone kama atanywea gongo madale
 
Baba ni baba tu! Uchagani mtoto unapata tatizo la kimila na bila baba hutoboi labda kama kafariki. Hata hivyo ndugu zake inabidi wafanye hiyo mila. Kama kweli huyo kijana ni wake huyo baba laana ipo mlangoni inasubiri kuingia ndani
 
Tunamtumia yeye kama Case Study

Mkuu unatumia kigezo gani kuuaminisha uma wa Jf kuwa Mzee Nassib ni mkosaji kwenye hili sakata? Wewe ulihusishwa vipi kwenye huo ugomvi mpaka ukang’amua huyo mzee ni mkosaji? Acha kuzungumzia tafaruku za mahusiano ya watu kama makala zako za uhamasishaji huku Jf,unakosea sana.
 
Tatizo ni uelewa wa mtu, na msimamo huwezi kukubali maisha ya mzazi kuishi na kijana mwenzio tena kwenye paa la nyumba yako. Vilevile si lazima ulipe au ukumbuke yaliyo kwisha pita, you need to be very smart yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Mwisho hakuna mtoto aliezaliwa bila Baba.
Ukinicheka shambani LAZIMA NIKUCHEKE SOKONI.
Jino kwa jino.

Aliyekuona wa afadhali mchukulie wa potelea mbali.

#YNWA
 
mzazi ni mzazi tuu. tatizo ni ujinga ujinga anaojazwa bwana naseeb na watu wanaomzunguka ukiwemo mtoa uzi. Diamond ni muislam,na Uislamu hauna mafunzo hayo wala hautoi fikra za namna hiyo kwa waumini wake. kama mshua alizingua kwenye malezi yako na sasa hivi anajutia, ni sawa, kwa sababu binaadamu Tumeumbiw makosa na shetani ndio kiongozi wa msafara huo wa kukosea, aidha kwa bahati mbaya ama kwa kukusudia. na kutubu piah ni sehemu ya maisha yetu, samehe saba Mara sabini... kama naseeb ni muislam na anaishi kwa misingi Ya dini hiyo(😁bt in reality hafuati misingi na taratibu za dini yake) , basi akae chini na ajitafakari juu ya mahusiano yake na Baba yake. mwenye wadhifa timilifu wa hukumu ni Mwenyezi mungu peke yake...

tenda wema kulipia ubaya ...
Saidia ulipo saidiwa.

Jifunze kupunguza shobo.
Aliyekuona wa afadhali basi mchukulie wa potelea mbali.

#YNWA
 
Hebu soma hiki kisa halafu niambie huyo mtoto akaja kukua na kisha baba yake akajitokeza unadhani nini kitatokea..?

2020

18 September 2020 majira ya saa 5 asubuhi,nikiwa kazini kwangu alikuja mdada wa umri wa miaka 22(sitamtaja jina) alikuja akiwa na lengo la kutoa mimba.Ukweli sikupendezwa na hiko kitendo ukitegemea niliwahi kuapa sitafanya hilo jambo katika taaluma yangu mpaka mwisho wa pumzi zangu,lakini ikabidi nimuhoji kwanini amefika hatua ile ya kutaka kutoa mimba.

Dada alianza kueleza yeye kwao ni Makambako alikuja Dar akiwa na umri wa miaka 14 kwa ajili ya kazi za ndani,baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja Boss wake alikua mkarimu sana kiasi alimchukulia kama binti yake hapo basi akamtafutia sehemu ya kujifunza ushonaji na baada ya muda kwa kua binti alikua muislam na boss ni mkristu,bint alimuomba ampeleke madrassa ili asome dini yake.

Boss alikubali na akampeleka alisoma madrassa kwa mwaka mmoja huko huko akapata Mwanaume wa kumuoa alipofikisha miaka 17 akaolewa,Boss kwa kushirikiana na ndugu zake akamuozesha.Maisha ya ndoa yalikua magumu kwa jambo moja yule bwana alikua mlevi sana japo alimjali kwa kila kituila dosari ilikua ulevi na baadae akaanza mambo ya kumpiga,..baada ya kuishi kwa miaka 2 ndani ya ndoa walipata mtoto wa kike.

Siku moja alikua ameenda mjini aliporudi alikuta mwanaume amehamisha kila kitu kwenye chumba walichokua wanakaa na mbaya zaidi alikuta talaka ikiwa imeshaandikwa na hakujua mahala yule mwanaume alipoelekea na ukizingatia hata mwenye nyumba alijua tu wanahama na mkewe japo kodi yao ilikua imebaki miezi 5 kuisha,,pigo lingine ilikua yule boss wake alihamia mwanza miezi 6 tu tangu alipoolewa hivyo kwa Dar akawa hana ndugu.

Mama mwenye nyumba akamwambia akae tu pale alimpa msaada wa kumpa godoro dogo na maisha yalianzia hapo..maisha yakawa magumu kwakua hakua na kipato na kazi hana kula yake ikawa ya tabu na baada ya muda alipata kibarua cha kuuza maji kwa mama mmoja na malipo yalikua 2500 kwa siku kazi ilikua ngumu sana kwake lakini hakua na chaguo ukizingatia alikua na mtoto mdogo baada ya kuhangaika sana kwa muda mrefu kuna kipindi mtoto wake aliugua hivyo akijikuta akitumia pesa ndogo kumtibia.Akajikuta anadaiwa kodi ya miezi 7 katika nyumba akawa na hofu kubwa ya kufukuzwa lakini Mama mwenye nyumba wala hakua akipiga kelele.

Mwaka 2020 February mama mwenye nyumba alifiwa na baba yake hivyo alisafiri kwenda kwao kigoma alikaa huko miezi 2..huku nyuma alikosa msaada siku moja wakati anatembeza maji alikutana na boda boda aliyekua amemzoea sana akamwambia shida yake kua anaumwa na hana pesa yakwenda hospital anaomba amkopeshe hela na angemlipa kidogo kidogo.Yule boda boda alikubali lakini kwa sharti moja alale nae na angempa elfu 30 bila kutaka kurejeshewa.Alikubali na wakaenda kulala lakini baada ya tendo asubuhi alipewa elfu 10 na alipohoji jamaa akamwambia kubali uwe mpenzi wangu nitakuhudumia.

Mwanamke alikubali lakini ndani ya wiki moja aligundua mwanaume alikua malaya sana hivyo akaomba waachane baada ya kumfumania mara mbili,jamaa kwa nyodo akasema sawa baada ya mwezi aliona mabadiliko na baada ya kupima akajikuta mjamzito alipomfuata jamaa alikataa akasema sina mpango wa mtoto chukua 10 ukanunue vidonge utoe.Kweli yule bint akaenda kutafuta vidonge(Misoprostal) akapata kwa elfu 15 akaweka lakini aliona damu kidogo sana akajua imetoka akendelea mambo mengine lakini baada ya miezi miwili akaona bado tumbo linakua na haelewi..alipopima tena akakuta bado mjamzito akazidi changanyikiwa akamfuata tena mwenye mimba yake.

Jamaa yule alimkana kua hamjui kwani alishampa hela ya kutoa na alishamwambia imetoka hivyo akamtafute mwenye hiyo mimba,aliendelea kumsumbua mpaka jamaa siku moja akampiga na jamaa kuhama kijiwe na mtaa.Alijatibu majaribio mengi ya kutaka kuitoa lakini ikashindikana hivyo alijichanga na ilipofika elfu 18 akaja kituoni ninapofanya kazi kujaribu.Aliponieleza hayo nikamuhurumia lakini bado sikumuamini nikamwambia mimi sitoi mimba na hapa haturuhusu kutoa mimba na kwakua umejaribu kuitoa hiyo mimba bila mafanikio usiitoe fanya uzae..alibembeleza sana ila nikasimamia msimamo wangu.Nilimpa elfu 5 kumuongezea pesa akaondoka.

Baada ya siku nne akarudi tena akiwa analia nimsaidie hana ndugu na maisha yanazidi kua magumu ana mtoto mdogo na bado mimba inamsumbua kisha hata kazi zake za kuuza maji za juani ni ngumu kuzurula ,,nikamwambia tena siwezi kufanya hilo jambo..nikamuuliza tena kipato chako kwa siku sh ngapi? Akasema 2500 ndo anayolipwa nikamwambia basi aache kutembeza maji mimi nitakua ninampa kila wiki elfu 30 kama pesa ya kujikimu.,ikiwemo na kumlipia kodi ,hapo akakubali nikaanza kumchunguza kidogo kidogo nikakuta kweli ana maisha magumu kuliko yale aliyonihadithia nikamuanzisha clinic kituoni kwetu ila jambo nina hofu nalo ameandika jina langu la kwanza kama jina la baba(na nilipohoji akanambia kwake ni kama shukrani na kwa kua mtoto hana baba basi jina langu lingefaa)..Mwezi wa kumi na moja zilinyesha mvua nyingi nyumba anayoishi iliporomoka akawa hana pa kukaa nikamshauri aende kwao akajifungulie na kipindi hiko chote mama ake na ndugu zake niliwasiliana nao wakiwa huko kijijini na wanajua yote, na sikuona busara akajifungulie huko maana najua changamoto zake,ila baada ya changamoto ya makazi ikabidi nimsafirishe hadi kwao na imebaki kumuhudumia kila ninapoweza.

Kufupisha stori .Jambo hili ndugu zangu staff wenzangu na marafiki wengine wanajua ila sijawahi mwambia mpenzi wangu kwakua yuko mbali ila akirudi nitamueleza kila kitu..nilishangaa kujikuta tu nafanya yote hayo lakini nina furaha nimeokoa maisha ya yule mtoto na tunatarajia mwezi huu ajifungue salama.Sijui ni kwa vipi itakuaje kuhusu baba yake mtoto lakini mimi kwa kiasi fulani najisikia amani nimetimiza majukumu yangu na huko alipo nadhani baada ya kujifungua atamlea vyema na nitatoa msaada kadri ninavyoweza japo sina kipato kikubwa.

Yapo mambo mengi yaliyotokea kwa mwaka 2020 lakini hili ndo jambo la kwanza nimelipa uzito mkubwa sana.

Nb:Sijasimulia kisa hiki kujisifu ila nimeona nishee nanyi ndugu zangu wa humu ili kama kuna mahala nimekosea nielezwe na pia kutoa angalizo kwa wanaume wanaokataa mimba zao ni wanasababisha matatizo makubwa sana kwa wasichana.

#Ndefu ila tuvumiliane
God Bless You ,akuongezee mara dufu ulipo punguza.
 
Kila mtu na imani yake mkuu....tumeagizwa kusamehe
Ukiweza samehe ila angalia usijegeuka mnafiki ukijifanya umesamehe wakati moyoni unakinyongo. Ni bora uonyeshe hujasamehe hata Mungu atakuelewa.
Alafu kusamehe sio lazima wala sio haki ya aliyefanya makosa, bali ukisamehewa jua ni neema tuu.
 
😊imani yako ndo inakufundisha hivyo eeeh!!?
Imani gani?
Maana hili nalo ni somo JENGINE.

Waslamu wanaamini wao ndio sahihi na wengine wotee MOTONI (wanaofanya shiriki)

Wakristo wanakwambia usipompokea Kristo (Yoh 14:1-7) Basi wewe motoni, huendi kwenye mji ule bila kupitia Kristo Yesu?

Shiah Vs Sunni nayo ni mada nyengine bila kusahau Catholic Vs Protestants na Sabath Vs Other Christian.

Ukiniambia dini fulani ndio sahihi (Mf: kristo) mi nitakuuliza ina maana Mungu alitaka nizaliwe muislamu ili niabudu dini sio halafu anichome?

IMANI GANI NI SAHIHI NA IPI ITAENDA MOTONI?

#YNWA
 
Mtoa mada anasema kusamehe sio lazima! Na mimi ninamashaka na imani yake
mzazi ni mzazi tuu. tatizo ni ujinga ujinga anaojazwa bwana naseeb na watu wanaomzunguka ukiwemo mtoa uzi. Diamond ni muislam,na Uislamu hauna mafunzo hayo wala hautoi fikra za namna hiyo kwa waumini wake. kama mshua alizingua kwenye malezi yako na sasa hivi anajutia, ni sawa, kwa sababu binaadamu Tumeumbiw makosa na shetani ndio kiongozi wa msafara huo wa kukosea, aidha kwa bahati mbaya ama kwa kukusudia. na kutubu piah ni sehemu ya maisha yetu, samehe saba Mara sabini... kama naseeb ni muislam na anaishi kwa misingi Ya dini hiyo([emoji16]bt in reality hafuati misingi na taratibu za dini yake) , basi akae chini na ajitafakari juu ya mahusiano yake na Baba yake. mwenye wadhifa timilifu wa hukumu ni Mwenyezi mungu peke yake...

tenda wema kulipia ubaya ...
 
Mkuu unatumia kigezo gani kuuaminisha uma wa Jf kuwa Mzee Nassib ni mkosaji kwenye hili sakata? Wewe ulihusishwa vipi kwenye huo ugomvi mpaka ukang’amua huyo mzee ni mkosaji? Acha kuzungumzia tafaruku za mahusiano ya watu kama makala zako za uhamasishaji huku Jf,unakosea sana.
 
Imani gani?
Maana hili nalo ni somo JENGINE.

Waslamu wanaamini wao ndio sahihi na wengine wotee MOTONI (wanaofanya shiriki)

Wakristo wanakwambia usipompokea Kristo (Yoh 14:1-7) Basi wewe motoni, huendi kwenye mji ule bila kupitia Kristo Yesu?

Shiah Vs Sunni nayo ni mada nyengine bila kusahau Catholic Vs Protestants na Sabath Vs Other Christian.

Ukiniambia dini fulani ndio sahihi (Mf: kristo) mi nitakuuliza ina maana Mungu alitaka nizaliwe muislamu ili niabudu dini sio halafu anichome?

IMANI GANI NI SAHIHI NA IPI ITAENDA MOTONI?

#YNWA
😊 huku wapi sasa!?...
 
Lakini sio lazima msamaha Mkuu.

Ukiona mtu umemuomba msamaha akakusamehe shukuru Mungu, sio haki yako kusamehewa ukikosea
Kusamehe ni lazima ila sasa itategemea kama msamaha wako umepokelewa au la ila umesamehe.

Ndo maana ya tenda wema nenda zako.
Hata kama mtu amekufanyia ubaya kumsamehe ni jukumu lako na yeye ndo anawajibu wa kukataa au kukubali msamaha wako.
 
Mimi mwenyewe sijalelewa na baba na hivyo namwelewa sana na Diamond.

Ila sasa tofauti yangu inakuja hivi, kwanini humtunzi Mzee Abdul halafu unamtunza Uncle Shamte 🤣🤣🤣🤣🤣
Uncle Shamte anamkuna vizuri ndio maana Bi Sandra kaelekeza mzigo apewe uncle
 
Hebu soma hiki kisa halafu niambie huyo mtoto akaja kukua na kisha baba yake akajitokeza unadhani nini kitatokea..?

2020

18 September 2020 majira ya saa 5 asubuhi,nikiwa kazini kwangu alikuja mdada wa umri wa miaka 22(sitamtaja jina) alikuja akiwa na lengo la kutoa mimba.Ukweli sikupendezwa na hiko kitendo ukitegemea niliwahi kuapa sitafanya hilo jambo katika taaluma yangu mpaka mwisho wa pumzi zangu,lakini ikabidi nimuhoji kwanini amefika hatua ile ya kutaka kutoa mimba.

Dada alianza kueleza yeye kwao ni Makambako alikuja Dar akiwa na umri wa miaka 14 kwa ajili ya kazi za ndani,baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja Boss wake alikua mkarimu sana kiasi alimchukulia kama binti yake hapo basi akamtafutia sehemu ya kujifunza ushonaji na baada ya muda kwa kua binti alikua muislam na boss ni mkristu,bint alimuomba ampeleke madrassa ili asome dini yake.

Boss alikubali na akampeleka alisoma madrassa kwa mwaka mmoja huko huko akapata Mwanaume wa kumuoa alipofikisha miaka 17 akaolewa,Boss kwa kushirikiana na ndugu zake akamuozesha.Maisha ya ndoa yalikua magumu kwa jambo moja yule bwana alikua mlevi sana japo alimjali kwa kila kituila dosari ilikua ulevi na baadae akaanza mambo ya kumpiga,..baada ya kuishi kwa miaka 2 ndani ya ndoa walipata mtoto wa kike.

Siku moja alikua ameenda mjini aliporudi alikuta mwanaume amehamisha kila kitu kwenye chumba walichokua wanakaa na mbaya zaidi alikuta talaka ikiwa imeshaandikwa na hakujua mahala yule mwanaume alipoelekea na ukizingatia hata mwenye nyumba alijua tu wanahama na mkewe japo kodi yao ilikua imebaki miezi 5 kuisha,,pigo lingine ilikua yule boss wake alihamia mwanza miezi 6 tu tangu alipoolewa hivyo kwa Dar akawa hana ndugu.

Mama mwenye nyumba akamwambia akae tu pale alimpa msaada wa kumpa godoro dogo na maisha yalianzia hapo..maisha yakawa magumu kwakua hakua na kipato na kazi hana kula yake ikawa ya tabu na baada ya muda alipata kibarua cha kuuza maji kwa mama mmoja na malipo yalikua 2500 kwa siku kazi ilikua ngumu sana kwake lakini hakua na chaguo ukizingatia alikua na mtoto mdogo baada ya kuhangaika sana kwa muda mrefu kuna kipindi mtoto wake aliugua hivyo akijikuta akitumia pesa ndogo kumtibia.Akajikuta anadaiwa kodi ya miezi 7 katika nyumba akawa na hofu kubwa ya kufukuzwa lakini Mama mwenye nyumba wala hakua akipiga kelele.

Mwaka 2020 February mama mwenye nyumba alifiwa na baba yake hivyo alisafiri kwenda kwao kigoma alikaa huko miezi 2..huku nyuma alikosa msaada siku moja wakati anatembeza maji alikutana na boda boda aliyekua amemzoea sana akamwambia shida yake kua anaumwa na hana pesa yakwenda hospital anaomba amkopeshe hela na angemlipa kidogo kidogo.Yule boda boda alikubali lakini kwa sharti moja alale nae na angempa elfu 30 bila kutaka kurejeshewa.Alikubali na wakaenda kulala lakini baada ya tendo asubuhi alipewa elfu 10 na alipohoji jamaa akamwambia kubali uwe mpenzi wangu nitakuhudumia.

Mwanamke alikubali lakini ndani ya wiki moja aligundua mwanaume alikua malaya sana hivyo akaomba waachane baada ya kumfumania mara mbili,jamaa kwa nyodo akasema sawa baada ya mwezi aliona mabadiliko na baada ya kupima akajikuta mjamzito alipomfuata jamaa alikataa akasema sina mpango wa mtoto chukua 10 ukanunue vidonge utoe.Kweli yule bint akaenda kutafuta vidonge(Misoprostal) akapata kwa elfu 15 akaweka lakini aliona damu kidogo sana akajua imetoka akendelea mambo mengine lakini baada ya miezi miwili akaona bado tumbo linakua na haelewi..alipopima tena akakuta bado mjamzito akazidi changanyikiwa akamfuata tena mwenye mimba yake.

Jamaa yule alimkana kua hamjui kwani alishampa hela ya kutoa na alishamwambia imetoka hivyo akamtafute mwenye hiyo mimba,aliendelea kumsumbua mpaka jamaa siku moja akampiga na jamaa kuhama kijiwe na mtaa.Alijatibu majaribio mengi ya kutaka kuitoa lakini ikashindikana hivyo alijichanga na ilipofika elfu 18 akaja kituoni ninapofanya kazi kujaribu.Aliponieleza hayo nikamuhurumia lakini bado sikumuamini nikamwambia mimi sitoi mimba na hapa haturuhusu kutoa mimba na kwakua umejaribu kuitoa hiyo mimba bila mafanikio usiitoe fanya uzae..alibembeleza sana ila nikasimamia msimamo wangu.Nilimpa elfu 5 kumuongezea pesa akaondoka.

Baada ya siku nne akarudi tena akiwa analia nimsaidie hana ndugu na maisha yanazidi kua magumu ana mtoto mdogo na bado mimba inamsumbua kisha hata kazi zake za kuuza maji za juani ni ngumu kuzurula ,,nikamwambia tena siwezi kufanya hilo jambo..nikamuuliza tena kipato chako kwa siku sh ngapi? Akasema 2500 ndo anayolipwa nikamwambia basi aache kutembeza maji mimi nitakua ninampa kila wiki elfu 30 kama pesa ya kujikimu.,ikiwemo na kumlipia kodi ,hapo akakubali nikaanza kumchunguza kidogo kidogo nikakuta kweli ana maisha magumu kuliko yale aliyonihadithia nikamuanzisha clinic kituoni kwetu ila jambo nina hofu nalo ameandika jina langu la kwanza kama jina la baba(na nilipohoji akanambia kwake ni kama shukrani na kwa kua mtoto hana baba basi jina langu lingefaa)..Mwezi wa kumi na moja zilinyesha mvua nyingi nyumba anayoishi iliporomoka akawa hana pa kukaa nikamshauri aende kwao akajifungulie na kipindi hiko chote mama ake na ndugu zake niliwasiliana nao wakiwa huko kijijini na wanajua yote, na sikuona busara akajifungulie huko maana najua changamoto zake,ila baada ya changamoto ya makazi ikabidi nimsafirishe hadi kwao na imebaki kumuhudumia kila ninapoweza.

Kufupisha stori .Jambo hili ndugu zangu staff wenzangu na marafiki wengine wanajua ila sijawahi mwambia mpenzi wangu kwakua yuko mbali ila akirudi nitamueleza kila kitu..nilishangaa kujikuta tu nafanya yote hayo lakini nina furaha nimeokoa maisha ya yule mtoto na tunatarajia mwezi huu ajifungue salama.Sijui ni kwa vipi itakuaje kuhusu baba yake mtoto lakini mimi kwa kiasi fulani najisikia amani nimetimiza majukumu yangu na huko alipo nadhani baada ya kujifungua atamlea vyema na nitatoa msaada kadri ninavyoweza japo sina kipato kikubwa.

Yapo mambo mengi yaliyotokea kwa mwaka 2020 lakini hili ndo jambo la kwanza nimelipa uzito mkubwa sana.

Nb:Sijasimulia kisa hiki kujisifu ila nimeona nishee nanyi ndugu zangu wa humu ili kama kuna mahala nimekosea nielezwe na pia kutoa angalizo kwa wanaume wanaokataa mimba zao ni wanasababisha matatizo makubwa sana kwa wasichana.

#Ndefu ila tuvumiliane
We jamaa lazima uende peponi
 
Back
Top Bottom