SeliSelina
JF-Expert Member
- Jun 27, 2014
- 289
- 710
kwanza kabisaa diamond ni mtoto ambae mama ake aliolewa bila ya kuwa na mimba yake au laa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika mkuulabda wazungu
Hakika mkuu
Wanaume wengi tunajiona wajanja sana wakati wa kutongoza wanawake na kutia mimba, linafika suala la kulea tunaruka futi sita na kukimbia majukumu yetu ya msingi. Wengi hatujui maana ya baba... Baba ni majukumu
Sasa ikifika muda mtoto uliyemtekeleza ana maisha tunaanza kutafuta huruma ya jamii. Tunasahau wale watoto wana mioyo kama yetu.
Nasisitiza hapa kwa wanaume wenzangu, kama huna uwezo wa kulea tafadhali vaa kondomu, kama tayari umeshasababisha mtoto jiandae kulea, kwa namna yoyote usitekeleze mtoto maana karma won't let you free. Ubaba ni majukumu
Ndugu mwacheni baba mondi awe fundisho kwa watia mimba wengine.....Mondi katika upande huu mi namuona boya Sanaa.......kitachomtoa machozi ni nn siku ikitokea mzee huyu akafariki?
Duu!! Aisee!!Usilojua ni kwamba Mama Diamond ndio kila kitu kwa Diamond. Ndio anampangia kila kitu. Nimewahi kufanya kazi na WCB kwa vipindi Fulani kipindi Makao makuu ya WCB yalipokuwa pale sinza.
Diamond sio kwamba hataki kumsaidia mama Yale ila Mama Diamond ndio hataki kabisa kusikia masuala ya Baba diamond. Nyie muoneni vile vile yule mama ni noma.
Nadhani mnajua kuwa Diamond na QUEEN DARLIN kuwa wanashea Baba. Siku moja Queen Darlin kamuita Kaka Yake Diamond chumbani akamwambia kuwa waangalie namna ya kumsaidia Baba yao. Mama Diamond alikuwa anawasikiliza dirishani, mpaka leo Huyo mama haziungi kabisa na Queen Darlin. Kuna wapuuzi watakuja kuleta ushabiki ila ndio hivyo.
Yule mama ana roho mbaya sana akikukataa jua huna chako kwa Diamond.
We jamaa lazima uende peponi
God Bless You ,akuongezee mara dufu ulipo punguza.
You guys mnaongelea msamha it’s all b’coz hamjui how it feels that situation na bad enough hamtakuja kui-experience at all. The best thing you can do it’s just to thank your God that shit had never happened to you.
In reality hakuna that feeling ya so called eti baba wala bond yake. Trust me akifa @mshanajr au member mwingine humu unaweza kusikitika kwa jinsi mnavyokua mnajadili mada mbalimbali humu JF. Yani kifo cha huyo baba au mahangaiko yake haufeel chochote yani unaona ni kama vile watu wanavyoteseka huko Syria au kufa maelfu ya watu kwenye vita lakini wala hustuki.
Personally likija suala la baba I cut it short, He’s dead. Honestly I don’t hate him at all and I am grateful kwa kuwa sehemu ya mimi kuzaliwa ila nakwepa tu maswali mengi abt him yatakayokuja mbele and I am not proud of him at all.
Lakini hii mambo imenifundisha kitu tofauti kabisa. Kuwa baba mwema, kulea familia hata kama uwezo huna.
In sha Allah I am gonna make a good dad to my future kids and to my future wife.
Lakini pia tuache hii mambo ya matumizi mabaya ya Mungu. Watu wanafanya ujinga mwingi sana tena intentionally then baadae wanakuja kusema sijui shetani, eti Mungu anasamehe sijui nini.
Nina kijana anakaribia miaka 20 Baba yake hamtaki, Kwanza hamjui hataki kujua habari zozote za mtoto nimejaribu miaka yote hii nimeshindwa mwaka Jana nikamuomba kuwa mtoto anaomba hata akujue alinijibu, anijue kama Nani? Asome afuate maisha yake na kashfa kibao LIVE kuwa afuate yake. Kimbembe kachaguliwa chuo kila nikipiga simu anakata mwezi SASA nimekopa Hadi kwenye riba mtoto aende chuo. Mwisho WA mwezi umefika nimelipa kiasi bado madeni. Kifupi MWACHENI DIAMOND AFANYE ANAVYOTAKA. Yoyote anaemtetea Mzee Abdul hajawahi kupitia shida hii. Mimi mtoto wangu Baba yake anamkashifu utafikiri sio damu yake.
Acha ninayopitia ni magumu hata siwezi kueleza yote uchungu alionao kijana kuna wakati nahisi anaweza hata kujidhuru. Huwa analia Hadi nachanganyikiwa.Hivi Diamond angekuwa anaendelea kuzunguka mjini na pea 4 za viatu Mzee Abdul angemkubali kuwa ni mwanae?. Angeshoboka kiasi hiki?Watu wasiojua mambo haya huwa wepesi kuongea
Acha ninayopitia ni magumu hata siwezi kueleza yote uchungu alionao kijana kuna wakati nahisi anaweza hata kujidhuru. Huwa analia Hadi nachanganyikiwa.Hivi Diamond angekuwa anaendelea kuzunguka mjini na pea 4 za viatu Mzee Abdul angemkubali kuwa ni mwanae?. Angeshoboka kiasi hiki?
Hilo ni somo tosha kwa wale wasioelewa, kuwa kumtelekeza mtoto Kuna madhara yake baadae, usije kutafuta lawama au mchawi,Hebu soma hiki kisa halafu niambie huyo mtoto akaja kukua na kisha baba yake akajitokeza unadhani nini kitatokea..?
2020
18 September 2020 majira ya saa 5 asubuhi,nikiwa kazini kwangu alikuja mdada wa umri wa miaka 22(sitamtaja jina) alikuja akiwa na lengo la kutoa mimba.Ukweli sikupendezwa na hiko kitendo ukitegemea niliwahi kuapa sitafanya hilo jambo katika taaluma yangu mpaka mwisho wa pumzi zangu,lakini ikabidi nimuhoji kwanini amefika hatua ile ya kutaka kutoa mimba.
Dada alianza kueleza yeye kwao ni Makambako alikuja Dar akiwa na umri wa miaka 14 kwa ajili ya kazi za ndani,baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja Boss wake alikua mkarimu sana kiasi alimchukulia kama binti yake hapo basi akamtafutia sehemu ya kujifunza ushonaji na baada ya muda kwa kua binti alikua muislam na boss ni mkristu,bint alimuomba ampeleke madrassa ili asome dini yake.
Boss alikubali na akampeleka alisoma madrassa kwa mwaka mmoja huko huko akapata Mwanaume wa kumuoa alipofikisha miaka 17 akaolewa,Boss kwa kushirikiana na ndugu zake akamuozesha.Maisha ya ndoa yalikua magumu kwa jambo moja yule bwana alikua mlevi sana japo alimjali kwa kila kituila dosari ilikua ulevi na baadae akaanza mambo ya kumpiga,..baada ya kuishi kwa miaka 2 ndani ya ndoa walipata mtoto wa kike.
Siku moja alikua ameenda mjini aliporudi alikuta mwanaume amehamisha kila kitu kwenye chumba walichokua wanakaa na mbaya zaidi alikuta talaka ikiwa imeshaandikwa na hakujua mahala yule mwanaume alipoelekea na ukizingatia hata mwenye nyumba alijua tu wanahama na mkewe japo kodi yao ilikua imebaki miezi 5 kuisha,,pigo lingine ilikua yule boss wake alihamia mwanza miezi 6 tu tangu alipoolewa hivyo kwa Dar akawa hana ndugu.
Mama mwenye nyumba akamwambia akae tu pale alimpa msaada wa kumpa godoro dogo na maisha yalianzia hapo..maisha yakawa magumu kwakua hakua na kipato na kazi hana kula yake ikawa ya tabu na baada ya muda alipata kibarua cha kuuza maji kwa mama mmoja na malipo yalikua 2500 kwa siku kazi ilikua ngumu sana kwake lakini hakua na chaguo ukizingatia alikua na mtoto mdogo baada ya kuhangaika sana kwa muda mrefu kuna kipindi mtoto wake aliugua hivyo akijikuta akitumia pesa ndogo kumtibia.Akajikuta anadaiwa kodi ya miezi 7 katika nyumba akawa na hofu kubwa ya kufukuzwa lakini Mama mwenye nyumba wala hakua akipiga kelele.
Mwaka 2020 February mama mwenye nyumba alifiwa na baba yake hivyo alisafiri kwenda kwao kigoma alikaa huko miezi 2..huku nyuma alikosa msaada siku moja wakati anatembeza maji alikutana na boda boda aliyekua amemzoea sana akamwambia shida yake kua anaumwa na hana pesa yakwenda hospital anaomba amkopeshe hela na angemlipa kidogo kidogo.Yule boda boda alikubali lakini kwa sharti moja alale nae na angempa elfu 30 bila kutaka kurejeshewa.Alikubali na wakaenda kulala lakini baada ya tendo asubuhi alipewa elfu 10 na alipohoji jamaa akamwambia kubali uwe mpenzi wangu nitakuhudumia.
Mwanamke alikubali lakini ndani ya wiki moja aligundua mwanaume alikua malaya sana hivyo akaomba waachane baada ya kumfumania mara mbili,jamaa kwa nyodo akasema sawa baada ya mwezi aliona mabadiliko na baada ya kupima akajikuta mjamzito alipomfuata jamaa alikataa akasema sina mpango wa mtoto chukua 10 ukanunue vidonge utoe.Kweli yule bint akaenda kutafuta vidonge(Misoprostal) akapata kwa elfu 15 akaweka lakini aliona damu kidogo sana akajua imetoka akendelea mambo mengine lakini baada ya miezi miwili akaona bado tumbo linakua na haelewi..alipopima tena akakuta bado mjamzito akazidi changanyikiwa akamfuata tena mwenye mimba yake.
Jamaa yule alimkana kua hamjui kwani alishampa hela ya kutoa na alishamwambia imetoka hivyo akamtafute mwenye hiyo mimba,aliendelea kumsumbua mpaka jamaa siku moja akampiga na jamaa kuhama kijiwe na mtaa.Alijatibu majaribio mengi ya kutaka kuitoa lakini ikashindikana hivyo alijichanga na ilipofika elfu 18 akaja kituoni ninapofanya kazi kujaribu.Aliponieleza hayo nikamuhurumia lakini bado sikumuamini nikamwambia mimi sitoi mimba na hapa haturuhusu kutoa mimba na kwakua umejaribu kuitoa hiyo mimba bila mafanikio usiitoe fanya uzae..alibembeleza sana ila nikasimamia msimamo wangu.Nilimpa elfu 5 kumuongezea pesa akaondoka.
Baada ya siku nne akarudi tena akiwa analia nimsaidie hana ndugu na maisha yanazidi kua magumu ana mtoto mdogo na bado mimba inamsumbua kisha hata kazi zake za kuuza maji za juani ni ngumu kuzurula ,,nikamwambia tena siwezi kufanya hilo jambo..nikamuuliza tena kipato chako kwa siku sh ngapi? Akasema 2500 ndo anayolipwa nikamwambia basi aache kutembeza maji mimi nitakua ninampa kila wiki elfu 30 kama pesa ya kujikimu.,ikiwemo na kumlipia kodi ,hapo akakubali nikaanza kumchunguza kidogo kidogo nikakuta kweli ana maisha magumu kuliko yale aliyonihadithia nikamuanzisha clinic kituoni kwetu ila jambo nina hofu nalo ameandika jina langu la kwanza kama jina la baba(na nilipohoji akanambia kwake ni kama shukrani na kwa kua mtoto hana baba basi jina langu lingefaa)..Mwezi wa kumi na moja zilinyesha mvua nyingi nyumba anayoishi iliporomoka akawa hana pa kukaa nikamshauri aende kwao akajifungulie na kipindi hiko chote mama ake na ndugu zake niliwasiliana nao wakiwa huko kijijini na wanajua yote, na sikuona busara akajifungulie huko maana najua changamoto zake,ila baada ya changamoto ya makazi ikabidi nimsafirishe hadi kwao na imebaki kumuhudumia kila ninapoweza.
Kufupisha stori .Jambo hili ndugu zangu staff wenzangu na marafiki wengine wanajua ila sijawahi mwambia mpenzi wangu kwakua yuko mbali ila akirudi nitamueleza kila kitu..nilishangaa kujikuta tu nafanya yote hayo lakini nina furaha nimeokoa maisha ya yule mtoto na tunatarajia mwezi huu ajifungue salama.Sijui ni kwa vipi itakuaje kuhusu baba yake mtoto lakini mimi kwa kiasi fulani najisikia amani nimetimiza majukumu yangu na huko alipo nadhani baada ya kujifungua atamlea vyema na nitatoa msaada kadri ninavyoweza japo sina kipato kikubwa.
Yapo mambo mengi yaliyotokea kwa mwaka 2020 lakini hili ndo jambo la kwanza nimelipa uzito mkubwa sana.
Nb:Sijasimulia kisa hiki kujisifu ila nimeona nishee nanyi ndugu zangu wa humu ili kama kuna mahala nimekosea nielezwe na pia kutoa angalizo kwa wanaume wanaokataa mimba zao ni wanasababisha matatizo makubwa sana kwa wasichana.
#Ndefu ila tuvumiliane
Una roho nzuri we Doc...God bless u[emoji848]Hebu soma hiki kisa halafu niambie huyo mtoto akaja kukua na kisha baba yake akajitokeza unadhani nini kitatokea..?