Diamond kwa sasa hana Baba, ukweli mchungu

kwanza kabisaa diamond ni mtoto ambae mama ake aliolewa bila ya kuwa na mimba yake au laa?
 
Wanaume wengi tunajiona wajanja sana wakati wa kutongoza wanawake na kutia mimba, linafika suala la kulea tunaruka futi sita na kukimbia majukumu yetu ya msingi. Wengi hatujui maana ya baba... Baba ni majukumu
Sasa ikifika muda mtoto uliyemtekeleza ana maisha tunaanza kutafuta huruma ya jamii. Tunasahau wale watoto wana mioyo kama yetu.
Nasisitiza hapa kwa wanaume wenzangu, kama huna uwezo wa kulea tafadhali vaa kondomu, kama tayari umeshasababisha mtoto jiandae kulea, kwa namna yoyote usitekeleze mtoto maana karma won't let you free. Ubaba ni majukumu
 

Kweli kabis
alafu ndio wakwanza kuita single mother
 
Mondi katika upande huu mi namuona boya Sanaa.......kitachomtoa machozi ni nn siku ikitokea mzee huyu akafariki?
Ndugu mwacheni baba mondi awe fundisho kwa watia mimba wengine.....
Mtoto anapotelekezwa na mzazi Ni mbaya na inauma sana
 
Duu!! Aisee!!
Mkuu huna haja ya kutumia nguvu sana kueleza hilo,,

Hata hii picha inajieleza,,,..

Angalia kisuruali chake .

Anaonekana wazi yaliyo moyoni mwake.
 
Nakuelewa sana mkuu,watu wanachonga tu,Diamond sio mjinga kufanya vile anavyofanya
 
You guys mnaongelea msamha it’s all b’coz hamjui how it feels that situation na bad enough hamtakuja kui-experience at all. The best thing you can do it’s just to thank your God that shit had never happened to you.

In reality hakuna that feeling ya so called eti baba wala bond yake. Trust me akifa @mshanajr au member mwingine humu unaweza kusikitika kwa jinsi mnavyokua mnajadili mada mbalimbali humu JF. Yani kifo cha huyo baba au mahangaiko yake haufeel chochote yani unaona ni kama vile watu wanavyoteseka huko Syria au kufa maelfu ya watu kwenye vita lakini wala hustuki.


Personally likija suala la baba I cut it short, He’s dead. Honestly I don’t hate him at all and I am grateful kwa kuwa sehemu ya mimi kuzaliwa ila nakwepa tu maswali mengi abt him yatakayokuja mbele and I am not proud of him at all.

Lakini hii mambo imenifundisha kitu tofauti kabisa. Kuwa baba mwema, kulea familia hata kama uwezo huna.

In sha Allah I am gonna make a good dad to my future kids and to my future wife.

Lakini pia tuache hii mambo ya matumizi mabaya ya Mungu. Watu wanafanya ujinga mwingi sana tena intentionally then baadae wanakuja kusema sijui shetani, eti Mungu anasamehe sijui nini.
 

Unajua watu wanapenda kuongea mambo yasiyowahi kuyapitia, waliopitia haya wanajua nazungumzia nini.

Kusamehe kupo lakini ukweli ni kuwa hakufanyi mtoto awe na mazoea na Baba au mama aliyemtelekeza, atabaki kumuita Baba au mama tena siku Akipigiwa simu sio mtoto apige simu
 
Nina kijana anakaribia miaka 20 Baba yake hamtaki, Kwanza hamjui hataki kujua habari zozote za mtoto nimejaribu miaka yote hii nimeshindwa mwaka Jana nikamuomba kuwa mtoto anaomba hata akujue alinijibu, anijue kama Nani? Asome afuate maisha yake na kashfa kibao LIVE kuwa afuate yake. Kimbembe kachaguliwa chuo kila nikipiga simu anakata mwezi SASA nimekopa Hadi kwenye riba mtoto aende chuo. Mwisho WA mwezi umefika nimelipa kiasi bado madeni. Kifupi MWACHENI DIAMOND AFANYE ANAVYOTAKA. Yoyote anaemtetea Mzee Abdul hajawahi kupitia shida hii. Mimi mtoto wangu Baba yake anamkashifu utafikiri sio damu yake.
 

Watu wasiojua mambo haya huwa wepesi kuongea
 
Watu wasiojua mambo haya huwa wepesi kuongea
Acha ninayopitia ni magumu hata siwezi kueleza yote uchungu alionao kijana kuna wakati nahisi anaweza hata kujidhuru. Huwa analia Hadi nachanganyikiwa.Hivi Diamond angekuwa anaendelea kuzunguka mjini na pea 4 za viatu Mzee Abdul angemkubali kuwa ni mwanae?. Angeshoboka kiasi hiki?
 

Watu wanasema mtoto kalishwa maneno wanashindwa kuelewa kuwa mtoto wa siku hizi akifikisha miaka saba tuu anaelewa na kujua mambo unayomfanyia,anajua hili ni jema na hili ni baya
 
Nasibu Shamte inabidi afikirie Mara mbili
 
Hilo ni somo tosha kwa wale wasioelewa, kuwa kumtelekeza mtoto Kuna madhara yake baadae, usije kutafuta lawama au mchawi,
 
Una roho nzuri we Doc...God bless u[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…