Mdogo wangu diamond unasifika sana na sidhani km utashuka leo wala kesho. Wewe ni celebrity unapendwa na wote wakristo kwa waislamu.
Nakushauri acha kaudini ambapo unako. Chukua ushauri wa Rayvanny jenga na makanisa ili uonekane hauna udini. Unajisifia kujenga misikiti yes ni jambo..but jenga na kanisa basi..Tanzania ni ya wote na fata mfano wa Rais anbaye anachangia both misikiti na makanisa. Na ushauri wa bure mwambie Tale apunguze udini. Wakristo wanakusapoti wewe sidhani km ni vyema ukijisifia kujenga misikiti au ukajifanya wewe ni mwislamu sana.Magufuli ni Rais anajenga kote..celebrity mzuri ni yule ambaye hajihusishi na dini.
Rayvanny na Baba levo wameshakushauri jenga na makanisa uonekane hauna udini.
Mkuu kwa post yako hii wewe ndiye mdini, kumbuka kuwa suala la imani ni jambo binafsi la mtu na wala haifai kumuingilia.
Katika uislamu ibada zipo nyingi, swala ndiyo inaongoza na zingine zinafuata kama kufunga ramadhani, kwenda kuhiji makka, nk, kutoa sadaka nayo ni ibada, sasa katika mafundisho ya uislamu kuna sadaka za aina 2, ya kwanza ni sadaka isiyoendelea na pili sadaka inayoendelea kwa kadiri sadaka hiyo inapozidi kutumika, (sadaqatul jarriyah), sadaka za aina hiyo ni kama kujenga msikiti, kujenga kisima, kutoa elimu inayowafaidisha watu nk, sasa Diamond anapojenga msikiti anatekeleza moja ya fundisho la dini yake kwa jambo hilo nasema lipo chini ya nafsi yake wala hapaswi kuingiliwa na hata kama atashauriwa lakini hiyo itabaki chini ya uamuzi wake na asilaumiwe kwa hilo.
Katika kujenga misikiti ikumbukwe pia kuna madhehebu kibao ya Waislamu ambao nao wanayo hamu kubwa ya kujengewa misikiti na ujue kuwa Diamond anatoka katika dhehebu la Sunni waljamaa, sasa ikitokea Diamond ajenge kanisa kwa hayo madhehebu mengine ya kiislamu itakuaje??!!, kuna Shia, Ansar sunna, Ismailia, Ahmadiyya nk. Na hata tukija kwa Wakristo itakuwa hivyohivyo kwani kuna Katoliki, Anglikana, Sabato, lutheran, Wapentekoste,nk, sasa ajenge wapi na aache wapi??!!,
Ni bora aachwe mwenyewe aamue kwani hilo ni suala binafsi na tukilifanya suala la kidini/udini ni lazima litatumbuka nyongo.