Diamond Platinumz alivyomtembelea Balozi Kairuki alivaa kiholela. Muone 50 cent sasa!

Mond kama star hebu awe anavaa kihaiba kulingana na anakoenda. Kama ni kwenye shoo zake mivao ya huko inaeleweka. Hata zile shoo zake za ki ccm anatakiwa avae ki ccm. Ndio ni msanii, ila si kila sehemu anavaavaa kisani tu, hiyo itakuwa anavaa kihuni kama alivyoenda kwa bolozi na mavazi ya kihuni
 
Diamond ni mbana pua
Usimfananishe na chuma cha pua mzee fifiti sent
 
Soma hapa we Kiranga unayetetea upuuzi! Umeandika kwa jazba sana mpaka unachapia hata sikuelewi.

Huyu jamaa amemaliza yote!
Mkuu,

Ushamba ni kum judge Diamond kwa mavazi wakati Diamond kavaa mavazi yale ili wewe umuongelee hivi unavyomuongelea.

Hujaelewa strategy ya Diamond ni wewe umuongelee hivihivi unavyomuongelea umeingia katika reli zake vizuri sana kakuchota akili vilevile alivyotaka.

Diamond anaishi akilini kwako bila kulipa kodi wakati yeye hata hakujui.

Hapo nani mshamba sasa?
 
wenyewe wanasema kapangilia code
 
Msanii na mtu mwenye Pesa hata akivaa gunia wataona ni kawaida
Ila ww ungevaa hivyo? Au ungeshatolewa nje ya ofisi tayar?
 
Hata 50 Cent anaishi akilini hata kama simfahamu,

Ishu inakuja ni utambuzi binafsi, 50 Cent anajua ninakutana na nani katika mazingira yapi na natakiwa niwe na dress code zipi kwa ofisi nitakayoingia mda huo.

Diamond hajaenda kwenye show pale, hamna jukwaa ubalozini, hawezi leta umbagala kisa tu ana uhuru wake

Diamond mwenyewe hapo kakosa utambuzi, umbagala siyo wa kila mahali
 
Huko Bungeni kuna Mbunge ambaye amewahi hata kuanzisha Project yeyote ya kusaidia jamii na kutengeneza ajira. Diamond ni extra miles kuliko hata huyo anayevaa suti
 
Sasa hiyo ni baibui, junia au suruali?
Kwani ubolizi getini hakuna mlinzi??
 
50 Cent alikuwa na kesi pale kavaa mavazi ya kwenda mahakamani.

Diamond hakuwa na kesi. Alikuwa nyumbani. Ubalozini ni nyumbani.

Mbona mnalinganisha mambo ambayo hayana ulinganifu?
 
Hao majambazi wewe unawajua.. ?! tudokezee kwa kuwataja hapa wawili watatu

Pia elezea neno jambazi… jambazi ni nani au ni kitu gani kisha uhusishe na uliyoyasema hapo kuunda maana kamili

Zingatia/Kumbuka:- Utayoyasema uwe na uhakika nayo na ushahidi uliotukuka yasiwe magumu mbeleni au ukaja kukataa

Ahsante!
 
Hana akili kabisa.
Mimi nahisi ana akili sana ila amezielekeza kuchambua kitu kisicho na umuhimu.

Kiranga anashauri hizo akili angeelekeza kuchambua pesa zinazopotea kwenye ripoti za CAG.

Si ingeleta manufaa ama wewe unaonaje?
 
Unafuatilia ripoti za CAG za kila mwala au unapoga kabobo tu hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…