Diamond Platinumz tunakushukuru, Umeamsha vijana wengi walioridhika na mafanikio

Diamond Platinumz tunakushukuru, Umeamsha vijana wengi walioridhika na mafanikio

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
1626431921313.png


Kijana Diamond Platnumz ni msanii ambae ni fundisho sahihi la namna halisi la jinsI ya kuwa na maendeleo one step at a time, kutumia connections za watu (networking) na kuji brand, pengine niseme wasanii wengi wapo kwenye kiwanda cha muziki ila huyu jamaa yupo kwenye kajiongeza mpaka kwenye music business.

Makubwa anayoyafanya hakika yanatuacha vinywa wazi, Kijana alietokea katika familia ya kimaskini huko tandale, ambae hata form 4 alifeli leo hii kawa na mafanikio ambayo hakuna msanii yoyote kawahi kuyapata hii nchi, mafanikio yake ni mengi sana lakini kitu alichofanya hizi wiki chache ni next levo, kijana kashusha magari ambayo hata Tanzania kuyakuta ni nadra sana na mengine hayapo kabisa, yani ni vyuma vyenye brand name kubwa na ni matoleo mapya,

Vijana wengi walisaridhika kwamba wakiwa na gari kama crown ama harrier tako la nani toleo la miaka kadhaa iliyopita basi ndio wameyapata maisha, kwa saizi haya mambo yanavyoendelea inawezekana vijana kuanza kuwa na ndoto za gari walau za milioni 50 na ziwe ni matoleo angalau ya miaka ya karibuni.

Pigo kubwa pia limewapata wasanii ambao nao hawana budi kufuata nyayo za huyu kijana ili wawe na mafanikio, muziki ni zaidi ya kipaji nikiwa na aana inabidi mtu akiamua kufanya muziki basi ahakikishe unamnufaisha pia kiuchumi, wasanii wengi wakali wenye vipaji kama kina barnaba, mwasiti, mario, n.k ni vipaji haswaa lakini wako wapi kimaendeleo?? hata Ali Kiba ambae nikiri wazi kabisa anaimba vizuri na anasauti nzuri na yupo kwenye game miaka nenda rudi, je maendeleo aliyonayo anaendana na thamani halisi??

Asante sana kijana wetu

Katika msafara huu kaiacha "BMW X6" nadhani ni kwasababu ni gari ambayo imepitwa na wakati, japo kibongo bongo bado ni ndoto ya vijana wengi sana na bado zinasumbua sana mjini.


 
Ila CCM ni noma sana.

Kodi ya uzalendo plus iletwe nayo.
 
Acha wivu na chuki mkuu, yani naona kila mkiwaza mafanikio ya kijana mnaanza kuingiza ajenda tofauti na maada ilimradi tu mpunguze maumivu
Hakika mkuu,yaani Kuna Muda Mara sanamu mixer migomo ya wavuvi ukicheki pembeni tozo ukibanja kidogo tezi dume.

Yaani bila bila.
 
Katika msafara huu kaiacha "BMW X6" nadhani ni kwasababu ni gari ambayo imepitwa na wakati[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Huyu mnyama ni kama jeans.. Haishi fasheni
Yes kibongo bongo x6 zinasumbua sana mkuu, hata harrier tako la nyani hasogei pale
 
Katengeneza ajira Ni vizuri wizara zinazohusika watambue mchango wake
 
Hadi wanaijeria na wakenya wakawa wanatushangaa, baadhi ya wabongo waliosapoti ile ishu ni viumbe wa ajabu sana, ila thawabu yao wameipata maana kila wakiona michuma ya kijana roho zinawauma mno
Kwanza nikupongeze kwa bandiko lako
Japo wapo watakao kupinga
 
Back
Top Bottom