Diamond Platnumz aburuzwa Mahakama ya watoto na Hamisa Mobetto!

Diamond Platnumz aburuzwa Mahakama ya watoto na Hamisa Mobetto!

Pia Domo ajifunze kukaa kimya. Yeye ni brand tofauti na Gold Digger
 
Kutembea na NgUMbARU nuksi kweli aisee. Binti anaponea humo humo kwenye child support. 5m? Domo sio hawez bali bora apigwe kuliko kutoa huo mzigo.
**Kojoa Upigwe kama Dayamondi Karanga.
 

Attachments

  • 20171001_151753.jpg
    20171001_151753.jpg
    259.5 KB · Views: 27
DADA ZETU WAJINGA SANA,SASA HAKIMU ATAMWAMBIA ATOE ELFU ISHIRINI KWAMWEZI.HATA UKIWA NA AKILI NANI ATAMUOA HUYU MCHWA SI NI AFADHARI ZARI.MIMBA SIO MTAJI DADA ZETU MJIONGEZE NI AIBU
 
Hamisa anazitafuta milioni tano kwa mwezi. Ila haya mambo ya kulazimisha vitu mwisho wake huwa si mnzuri hata kidogo. Pamoja na kwamba matunzo ni haki ya mtoto ila nachokiona Hamisa anazidi kujidhalilisha tu.

..................................................................
Katika pitapita mitandaoni nimekutana na haya::

SHERIA HAILAZIMISHI KUTOA MATUNZO YA MTOTO KULIKO UWEZO WAKO.

Na Bashir Yakub.


Suala la matunzo ya watoto/mtoto lim ekuwa ni suala ambalo wasomaji wengi wamekuwa wakiniuliza sana. Wengi wao wanaouliza ni wale ambao wamezaa nje ya ndoa na hivyo kuna utata wa matunzo ya watoto na wale ambao wamekuwa wana ndoa lakini sasa tayari wametengana aidha kwa talaka au bila talaka. Niseme tu kwa ufupi kuwa suala la matunzo ya watoto linajumuisha mambo mengi nami nitaeleza baadhi tu. 1.

HUWEZI KUMLAZIMISHA MTOA MATUNZO KUTOA AMBACHO HANA. Kumekuwepo na tabia ya wazazi hasa upande wa wazazi wa kike kuwalazimisha wanaume ambao wamezaa nao na kutengana nao kutoa matunzo ya watoto kwa kiwango cha juu kabisa ambacho pengine kinazidi hata kipato cha mtoaji.

Hili si sawa. Ni kweli sheria inamlazimisha mwanaume kutoa matunzo ya mtoto lakini haimlazimishi kutoa kuliko anachopata. Sheria haiseme kwakuwa mwanamke anaishi na mtoto wa mtu basi mwanaume ndio sasa afanywe kitega uchumi.

Inafikia hatua mwanamke hafanyi kazi yoyote isipokuwa anategemea ile pesa ya matunzo ya mtoto ndio iwe kila kitu katika maisha yake. Hii ndio sababu hata akipewa kiasi kinachotosha haoni kama kinatosha kwakuwa kinakuwa na njia nyingi kama saluni, nguo za kuvaa, pesa ya upatu, michango ya harusi na kitchen party na kila kitu kinachohusu maisha yake binafsi.

Ieleweke wazi kuwa kwa mujibu wa sheria pesa ya matunzo ya mtoto haihusiki na haya. Pesa ya matunzo ya mtoto ni pesa ya matunzo ya mtoto kama neno lenyewe lilivyo na linavyojieleza si vinginevyo.

2.INARUHUSIWA KUKATAA IKIWA UNALAZIMISHWA KUTOA MATUNZO YANAYOZIDI UWEZO WAKO. Ikiwa mwanaume analazimishwa kutoa kuliko kipato chake basi anaruhusiwa kukataa hata kama amri hiyo imetolewa na mahakama. Wengine huandikishana polisi lakini bado haibadili maana kwakuwa mtu anatakiwa kutoa kulingana na uwezo wake au kipato chake. Wapo wazazi hasa wa kike ambao huwalazimisha wanaume kutoa matunzo ya kuwasomesha watoto international schools wakati kipato cha mwanume ni shule ya kata.

Sheria inachokataza ni kukataa kabisa kutoa matunzo ya mtoto lakini haimlazimishi mtu kutoa kilichomzidi. Au wengine hulazimisha kuwekewa mpaka wafanykazi wa ndani( house girl) wakati kipato cha mwanaume hakiruhusu jambo hilo. Huu nao ni unayanyasaji kwa upande wa wanaume na haukubaliwi na sheria.

La msingi ni kuwa iwapo utalazimishwa kutoa kuliko uwezo wako we kataa. Na kama uamuzi huo umetolewa na mahakama basi kataa kwa kukata rufaa kupinga kabisa jambo hilo. Sheria inaposema matunzo ya watoto haisemi kuwa watu watoe kuliko uwezo wao hapana. Sheria ni haki na haki huzingatia ukweli na hali halisi ya jambo.

3. UMRI WA WATOTO KUISHI NA MAMA AU BABA. Mara nyingi sheria imeelekeza watoto walio chini ya umri wa miaka kumi yaani kuanzia miaka tisa kushuka chini kuishi na mama. Aidha kuanzia miaka kumi kwenda mbele mtoto anaweza kuchagua aishi na nani kati ya baba au mama.

Kwahiyo iwapo mtoto amefikisha umri wa miaka kumi au zaidi basi baba anaweza kumchukua mtoto wake iwapo pia mtoto atapenda kukaa na baba yake. Wapo wazazi ambao wamekuwa wakiwagangania watoto hata baada ya watoto kuvuka umri huo ili waendelee kuwafanya vitega uchumi kupitia kudai matunzo. Hili si sawa hasa iwapo mtoto yuko tayari kukaa na baba yake.

4. BABA ANAWEZA KUOMBA KUKAA NA WATOTO HATA KAMA NI WADOGO SANA. Hapo juu tumeona kuwa ni lazima mtoto kukaa na mama iwapo ana umri chini ya miaka kumi. Msimamo huu unaweza kubadilika iwapo baba atatoa sababu za msingi za kuomba mama asikae na watoto. Hii haijalishi watoto wana umri gani iwapo tu ana sababu za msingi basi ataomba kukaa na watoto/mtoto wake. Sababu kubwa za kuomba watoto ni iwapo mama ana ugonjwa wa akili na hivyo kuwa hatari kwa ustawi wa mtoto/watoto.

Pia iwapo mama anakaa na watoto katika mazingira hatarishi kama danguro, baa, sehemu za madisco, au mama anajihusisha na vitendo vya ukahaba ambavyo si vyema kabisa kwa makuzi ya mtoto. Hii inajumuisha matendo yote maovu ambayo kukaa na watoto/mtoto yanaweza kuleta athari mbaya kwake na ni hapo baba atakapoomba kuchukua mtoto/watoto na atakubaliwa bila kujali umri wa watoto.

5. HAKI YA KWENDA KUWAONA WATOTO. Wapo watu ambao huzuiwa kuwaona watoto. Wengine huruhusiwa lakini kwa masharti maalum na kwa kupewa muda wa kuzungumza. Hii haikubaliki kisheria mzazi anapaswa kuwaona watoto kwa uhuru na bila masharti yanayolenga kumwondolea haki hiyo.

0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com. | sheriayakub.blogspot.com
nakupa kesi huyu mjinga akafanye kazi huyu dada mjinga sana
 
Stress inayofuata ni kupigwa chini na mkewe. Yule mwanamke ana exposure, kaishi mbele kidogo, South Africa, haelewi mambo ya ku chiti halafu unasema "shetani alipita." Hatokei Tandale. Eti unafumwa kwenye infidelity kwa kuzalisha pembeni halafu unasema "kwa mwanamme haya yanatokea, shetani amepita." Ungetafuta mke Tandale angekuelewa na akavumilia hayo...!
 
Timu Dai embu fikirieni,

hii hela inaweza ku cover vitu basic vya mtoto tu,

haitoshi,kumpa na mama yake matunzo,

yes,na yeye alipwe,

Muda anaoshinda na mtoto,angeweza kwenda kazini au kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo...........

hii sheria itazamwe upya.....
 
Ok,tumekuskia tutamuongezea coz kale kajamaa kingine kumbe si ka kwetu so gharama za yule tutazihamishia huku.....team Lion oyeeeeee!!!!!
 
Hivi nyie watu mnajua mnachoongea hapa!!!

Hamna kitu cha maana hapo!!! Diamond keshasema wazi kwamba kwavile mambo yenyewe yanaenda kisheria, ameshamalizana na mwanasheria wake na matunzo ni Sh.200K kwa mwezi kwa sababu ndivyo sheria inavyosema!!

Hamisa anataka 5M kwa mwezi! Ni mpumbavu tu ndie anaweza kutoa hukumu in favor of Hamisa manake lazima aseme hizo 5M zinakujaje kujaje! Na kwavile alizalishwa na Majizo, aoneshe hizo 5M alizokuwa analipwa kila mwezi or else, ataonekana ni opportunist anaezaa na watu wenye uwezo ili kuendesha maisha yake binafsi!!!!
 
DADA ZETU WAJINGA SANA,SASA HAKIMU ATAMWAMBIA ATOE ELFU ISHIRINI KWAMWEZI.HATA UKIWA NA AKILI NANI ATAMUOA HUYU MCHWA SI NI AFADHARI ZARI.MIMBA SIO MTAJI DADA ZETU MJIONGEZE NI AIBU
Yaani huyu demu ndo anazidi kulivurunda! Endapo angefahamu sheria zinasemaje kuhusu child support, wala asingefanya huu upuuzi manake yeye ndo anakuwa loser zaidi kuliko huyo Diamond!!! Mbaya zaidi, ataonekana ni gold digger!!
 
Ajiandae kutoa breakdown ya 5m mahakamani. Mtoto anatumiaje 5m kwa mwezi?
Maana ni matunzo ya mtoto. Yeye hayumo?
Zipo pia sehemu za kutunza watoto asisahau !!
 
Timu Dai embu fikirieni,

hii hela inaweza ku cover vitu basic vya mtoto tu,

haitoshi,kumpa na mama yake matunzo,

yes,na yeye alipwe,

Muda anaoshinda na mtoto,angeweza kwenda kazini au kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo...........

hii sheria itazamwe upya.....
Wakati mnapobeba mimba hua hamsemi mtahitaji kulipwa, uzae useme unataka kulipwa? Kwani kua na mtoto ni ulemavu? Au kua na mtoto ni ajira? Kwa hiyo alipwe 30,000 kama beki tatu ? Maana ndo mshahara wa beki tatu mlea mtoto.
 
Timu Dai embu fikirieni,

hii hela inaweza ku cover vitu basic vya mtoto tu,

haitoshi,kumpa na mama yake matunzo,

yes,na yeye alipwe,

Muda anaoshinda na mtoto,angeweza kwenda kazini au kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo...........

hii sheria itazamwe upya.....
Mchangie
 
Hakuna kiwango cha kumlea mtoto wako ni ukosefu wa akili na ustaarabu kusubiri serikali ikupangie kiwango kwa nyama na damu yako mwenyewe,ugomvi wake na mzazi mwenzie usimtoe kwenye mstari wa kua baba bora kwa kua anamudu kufanya kitu ni heri afanye kwa manufaa ya mwanae hizi saga zitamgharimu akumbuke hata yeye yuko mbali na baba ake kisa tu vurumai kati ya baba na mama ake na baba kutomlea ipasavyo kwa nafasi yake bora amlee mtoto wake kama anavyowalea wengine ikitokea mama akaamua kutumia vibaya anachopewa yeye anakua salama inawezekana hata baba ake Diamond alikua anatiwa ujinga na masela zake kua alete usela ila leo anajutia.
Kumbe ungekuwa wewe ndo Diamond ungefanyaje?! Wakati wa ujauzito alikuwa anahudumia above many men would do; 70K per day! Diamond alipotaja hicho kiasi watu waliamini anatafuta kiki. Majuzi baada ya Idris Sultan kumzingua Hamisa, povu la Hamisa kwa Idris likathibitisha ukweli wa 70K.
Hamisa.png


Hizo sehemu nilizo-underline zinathibitisha kwamba ni kweli Hamisa alikuwa anazilamba 70K daily na usafiri juu! Hapo ilikuwa hata mtoto hajazaliwa!!

Sasa kama mtu aliweza kuhudumia mimba kiasi hicho, ndo angeshindwa mtoto?!!

Matokeo yake, Hamisa akakutana na wajinga wenzake akaanza kuwasikiliza badala ya kuendelea kula na kipofu bila kumgusa mkono!!! Kwavile walishatibuana, Chibu akasema okay, you're issue now will be handled na mwanasheria wangu manake sihitaji hata kuonana na wewe!!! Sheria inasema 70K kwa mwezi or probably less; Chibu akasema nitatoa 200K; above legal limit!!!

Hamisa na tamaa zake anataka 5M kwa mwezi! Milioni tano kwa mwezi huyo mtoto anakunywa maziwa ya almasi na dhahabu, au?! Au anavaa pampers zilizotengenezwa kwa madini?!!!

Mjini kuna wanawake kibao, tena wengine na status zao kuliko Hamisa lakini wamezaa na committed men na wanazitandika pesa za hao wanaume kimya kimya bila upande wa pili kufahamu!!!

Kinyume chake, Hamisa akadhani akiweka public atakuwa anamkomoa Zari na matokeo yake, hivi sasa anadhihirisha msemo kwamba, "mtaka yote kwa pupa, hukosa yote kwa pupa!" kwa sababu hakuna mahakama itakayokubali eti alipwe Sh 5/mwezi wala 2 Million!!!

In short, huyu demu ni mjinga kama sio mpumbavu!!! Na utakavyojua huyu demu ni mjinga ni pale anapodai amedhalilishwa na kutaka aombwe radhi wakati ni yeye ndie alikuwa anavujisha picha za chumbani!!!
 
Back
Top Bottom