Diamond Platnumz achaguliwa na FIFA kushiriki wimbo wa Kombe la Dunia 2018

Diamond Platnumz achaguliwa na FIFA kushiriki wimbo wa Kombe la Dunia 2018

Huyu Jamaa kila Siku anapigwa ' majungu ' na ' Wazawa ' kabisa ila nilichogundua wenye ' akili ' zao kubwa huko nje ya mipaka ya Tanzania wanatambua sana Kipaji chake na uwezo wako kama Mwanamuziki. Kwa hili sasa nadhani ni wakati muafaka kwa ' haters ' wake wote kuungana na wanaompenda ili kumuunga mkono azidi kufanikiwa zaidi na kuipeperusha vyema Bendera yetu ya Tanzania.

Hongera sana Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na namuomba Mwenyezi Mungu azidi Kukubariki.

Za kunyapianyapia kutoka Huku kwetu mji kasoro meli zinasema eti Hili fagio lako ulilolitoa kwa huyu dogo ni tu kwa kuwa unatafuta ajira wasafi TV and redio ukizingatia wewe ni Guru talented kabisa katika tasnia ya Habari hapa nchini
 
Hongera DP kwa mafanikio makubwa sana. Tunga wimbo ambao utaitikisa dunia nzima na kukuongezea umaarufu wako kila kona ya dunia.
Ni kazi kubwa sana...maana lazima atafute vionjo vya Asia, Amerika zote, ulaya, australia, na wale wa visiwani! Kwenye wimbo utakao pigwa ndani ya 3-5 minutes! Kwenye maneno lugha (Kiswahili, kifaransa, kiingera, latino, kirussia, china), si kazi ya kitoto hii.
 
haka kajamaa kanafanya vizuri sana kanastahili pongezi hata kama hatutaki!
fikiria elimu yake na pia sio mtoto wa kishure ila anatubuluza kwa mkwanja ile mbaya wasomi wamebaki na bahasha za kaki na kumlalamikia Magu eti posho haipandi yeye yuleee!
mkisema mchawi na ninyi mnaroga kupita kiasi mpaka chekeche la vyeti hewa haliwaoni.
Kuna msomi mmoja hapo juu tena kwa level ya digrii ni mshabiki wake wa kutupwa.Elimu ni nyenzo tu ya kukuingiza kwenye tabaka la wanyonyaji na ukifanikiwa kuingia humo utatusua tu.Kipaji hakijawahi kulingana na usomi,kipaji kiko juu,acha tuendelee na kumshsbikia Messi
 
Za kunyapianyapia kutoka Huku kwetu mji kasoro meli zinasema eti Hili fagio lako ulilolitoa kwa huyu dogo ni tu kwa kuwa unatafuta ajira wasafi TV and redio ukizingatia wewe ni Guru talented kabisa katika tasnia ya Habari hapa nchini

Ha ha ha ha ha ha....mdogo wangu bhana! Hapana ila ninamkubali mno ' Ndomo ' kutokana na Kazi zake nzuri na za ukweli.
 
Kama nawaona Basata wakijiandaa kuifungia nyimbo yake world cup.
Ile ilikuwa wake up call akae kimaadili maana dili lilikuwa njiani. Exposure itakuwa kubwa kwenye kombe la dunia hivyo Basata wasingekaa kimya kama tunaelekea kuaibika kutokana na mienendo ya wanamuzi!
 
Uongo mtupu, hilo ni tangazo la cocacola tu. Yaani waachwe wasanii wenye akili zao duniani wanaojua tumbuiza wkamchukie Diamond aende kuimba salome , wabongo mnapenda Tanganyika kirahisi sana. Habari hiyo haipo kwenye source zozote zaidi ya viblog vyenu vya madale
 
Kuweka majina ya nchi zote washiriki katika wimbo wake pia itakuwa bomba sana. Nakubaliana nawe Mkuu ni lazima uwe dakika 5 au labda FIFA wanaweza kuruhusu hadi dakika 7.

Ni kazi kubwa sana...maana lazima atafute vionjo vya Asia, Amerika zote, ulaya, australia, na wale wa visiwani! Kwenye wimbo utakao pigwa ndani ya 3-5 minutes! Kwenye maneno lugha (Kiswahili, kifaransa, kiingera, latino, kirussia, china), si kazi ya kitoto hii.
 
KOMBE LA DUNIA.
Diamond Platnumz ameteuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa miongoni mwa wasanii watakao perform kwenye uzinduzi wa Kombe La Dunia nchini Urusi.
84c95c7c5b3f76b38c2252cfe8737e31.jpg

Vile vile,Katika kombe la dunia hilo Diamond Platnumz watakutana na wasanii kama JasonDarulo,CassperNyovest na wasanii wengine wengi kutoka nchi mbali mbali zikiwemo Uganda,Ethiopia,na Msumbiji katika wimbo uitwao [HASHTAG]#COLOR[/HASHTAG],unatarajia kutoka mapema tarehe 16 March mwezi huu.
20333f06e3fb87930a0e0ba69f86c611.jpg

Huo ni miongoni mwa uwanja uliopo nchini Urusi.

Kikubwa watanzania wenzangu Tusuport na kumuombea sana maana nchi yetu tulidharauliwa sana kila nyanja kupitia Diamond Platnumz ,Now tuko kwenye Ramani ya Dunia.
Hii inaitwa funika bovu... Dogo ni next level haters roho roho zinawavuja sumu... But waswahili wanasema usimwingilie aliyepewa kapewa
 
Shemeji yetu angeenda Urusi ila ndiyo hivyo tena,WEMA deal hilo!!!
 
wamekosa mtu wanapeleka huyo jinga,,,,,,tujiandae kuaibika linaweza kwenda kule kutafuta wanawake
 
Back
Top Bottom