Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Kuhusu diamond kudaiwa na TRA.
View attachment 507134
Post aliyopost diamond leo.
maoni yangu;
Serikali kama inahitaji pesa za wasanii ainabudi kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia kazi, diamond kaongea ukweli sema anaongea kwa uoga sana.
Nadhani hili ni swala la elimu ya uraia tu.
Kuna watanzania wanaodhani kuwa kulipa kodi ya mapato serikalini (PAYE) ni asante kwa serikali kwa kuwasadia mazingira mazuri ya kufanyia kazi zao badala ya kujua kuwa hiyo ni sheria ya serikali yoyote duniani. Wanasahau kuwa kuna wafanyakazi wanaolipwa mishahara ya shilingi laki tano tu kwa mwezi na bado wanakatwa PAYE, lakini wanaona msanii anayelipwa mara elfu ya hizo za mfanya kazi hahitajiwi kulipa kodi kwa vile eti serikali haikumsaidia kuzipata.
Tatizo hili limetokana na kuwa chini ya serikali zinazotegemea misaada sana kutoka nje (ambako watu wao wanalipa kodi) na kuwaacha baadhi watanzania hasa wenye vipato visivyo rasmi wakila nchi bila kulipa kodi kwa muda mrefu. Tujifunze kuwa mastaa kama Wesley Snipes walifungwa miaka kadhaa jela kwa kutolipa kodi. Kodi ya mapato inategemea mapato yako siyo jinsi ulivyoyapata; uwe umepata mapato hayo kwa kuuza njugu, kuimba au kufanya kazi ya kuajiriwa, unatakiwa ulipe kodi.
Uganda pale kuna mwimbaji Bobi Wine alilambwa na kodi ya milioni 54 akalipa bila kulalamika.