Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

Si anasema show moja yake analipwa milioni 100?, tena naona hiyo 400M anayodaiwa ni ndogo kulinganisha na income yakeyake! Alipe tuu
Faida ya kuwa mkweli unajisifu Kwa kitu ambacho hakipo usijue unajitwisha mzigo
 
Hizo kodi 400ml ni kwa ajiri ya muzik au biashara zote anazofanya diamond? Kama ni biashara alipe tu bila kelele asitumie mgongo wa muzik kukwepa kodi
Amejitangaza Kama a successful musician
 
Dawa ya kodi ni kulipa. Kama anaona si halali alalamike TRA si bungeni. Serikali inaendeshwa kwa kodi siyo kwa uji. Kama watu tusingelipa kodi huyo Prof J mshahara mnono wa ubunge angeutoa wapi
 
Jmn vilio vya nini,sie kila mwezi tunakatwa zaidi ya 30% ya mshahara kama kodi na tumetuliaa tuliii...,
 
"unaambiwa dai amekadiliwa tu kodi, hakuna records za mapato yake anayoingiza." This implies kwamba Diamond kaonewa
Hujui sheria ya kodi ina 'presumptive rates'??.. ambazo hutumika kwa watu wanaoingiza kipato lakini hawana rekodi za kifedha
Refer Income Tax Act,section nmesahau
Ila kwa kipato cha diamond aajiri mhasibu 'amtengenezee' ishu zake za kodi,sio mtu wa kukadiriwa mapato huyu he makes a loot..
TRA sio wa kuwakimbia ni wa kuwa'manage' ili usile shoti
 
Hujui sheria ya kodi ina 'presumptive rates'??.. ambazo hutumika kwa watu wanaoingiza kipato lakini hawana rekodi za kifedha
Refer Income Tax Act,section nmesahau
Ila kwa kipato cha diamond aajiri mhasibu 'amtengenezee' ishu zake za kodi,sio mtu wa kukadiriwa mapato huyu he makes a loot..
TRA sio wa kuwakimbia ni wa kuwa'manage' ili usile shoti
Ndio nilichomwambia mleta mada kwenye post [HASHTAG]#104[/HASHTAG]. Diamond S.80 ya Income Tax Act haimuhusu.
 
Diamond ni mnafiki.... Alipe hiyo kodi aache upumbavu wake..... Si ana uraia wa S.A aende akaishi huko..... Na makaburu wenziee..... Akishindwa kulipa afilisiwe.... Ndiyo apate akili kuwa ccm siyo mama yake....
 
0ffa2e4396da87224c35c081f4f5fead.jpg


Wanajamvi salamu kwanza!

Nimekutana na mjadala mzito mtandaoni kuhusiana na msanii Diamond Platnumz kudaiwa kodi ya shilingi milioni 400 na TRA. Wengi wametoa maoni yao kwa hisia na jinsi ambavyo wanaweza na ni uhuru wao. Hata mimi nimeguswa kama alivyoguswa Profesa J na Mheshimiwa Mtolea (MB). Lakini kuna mambo nadhani kabla hatujajikita zaidi kutetea au hata kuhukumu inabidi tuyajue au tuwe informed nayo kabla hatujatetea au hata kushauri kwenye jambo kama hili.

Kwanza tujue kwamba Diamond anafanya biashara kwenye hii tasnia ya burudani hivyo ni wazi kuwa ni lazima alipe kodi kama wananchi wengine.

Swala linalobaki hapa ni kiasi cha kodi kwani kinaonekana ni kikubwa mno kwa maoni ya waliowengi humu jamvini. Lakini kabla hatujahitimisha hili ni lazima tujue Diamond anaingiza kiasi gani? Je ni aina gani hiyo ya kodi je ni income tax, entertainment tax, VAT etc.

Tukijua kiasi anachoingiza na aina ya kodi anayodaiwa, pia tulinganishe na wasanii wengine kama Ali Kiba, Lady Jaydee, Vanessa Mdee, Lina, Jux, Ben Pol, Mrisho Mpoto nk je wao wamelipa au wanadaiwa kiasi gani kutokana na pesa wanazoingiza tukijua haya tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujaji kuwa ama Diamond Platnumz anaonewa au anastahili kulipa hiyo kodi.

Mwisho nishauri serikali sasa ni wakati wa serikali kuwekeza nguvu zake kwenye kuboresha na kusaidia kukuza sanaa. Kama msanii mmoja mnaweza kumdai milioni 400 ni wazi sasa kwamba tasnia hii inaweza kuisaidia nchi kuingiza kipato kwa taifa na taifa likanufaika.

Chukulia mfano milioni 400 inaweza kujenga dispensari ngapi kule Kolomije? Je, ni shule ngapi za kata zinaweza kujengwa? Je, kama wasanii hawa walio wengi kama kumbikumbi wakitengenezewa mazingira mazuri yatayowafanya wao pia wanufaike na kazi za mikono yao lakini taifa pia likaingiza pato hatutafika tunakotaka?.

Nishauri serikali sasa kuondokana na mawazo ya kuitazama sanaa na wasanii kama watu fulani wahuni na kuwadharau bali tuwathamini na kuwawezesha tutafika mbali zaidi.

CC; Mwakyembe,
By Zawadi B. Lupelo
 
Alipe kodi aache kulia lia...si anajitangaza na kujigamba kuwa anaingiza mkwanja mrefu... au ni za ngada..basi achunguzwe nae.... HAPA KAZI TUUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Back
Top Bottom