Diamond Platnumz afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kuharibu nyumba aliyokuwa amepanga

Diamond Platnumz afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kuharibu nyumba aliyokuwa amepanga

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mwanamuziki Nassibu Abdul 'Diamond Plutnumz' amepelekwa mahakamani kwa tuhuma za uharibifu wa mali ndani ya nyumba aliyokuwa amepanga kwa ajili ya studio maeneo ya Sinza Kijitonyama kabla ya kuhamia Mbezi, jijini Dar es Salaam huku akidaiwa kodi ya mwezi mmoja.

Mali hiyo yenye thamani ya zaidi ya Sh337 milioni kwa mujibu wa wasanifu majengo waliifanya uchunguzi wa vitu vilivyoharibika vya Maulidi Wandwe ambazo Diamond Plutnumz anatakiwa kulipa.

Diamond amepelekwa Mahakama ya Ardhi Mwananyamala Dar es Salaam jana Jumatatu na mmiliki wa nyumba hiyo Wandwe ambapo msanii huyo hakutokea mahamani huku wakili wake Gerald Hamisi alitoa taarifa kwamba mteja wake yupo nje ya nchi hivyo kutokana na ugonjwa wa Corona atarudi nchini baada ya wiki tatu.

Aidha wakili huyo wa Diamond aliieleza mahakama kuwa kutokana na muda kwenda amefanya mawasiliano na Meneja wake Babu Tale na kwamba watalifanyia kazi suala hilo na kuliweka sawa.

Kwa upande wa wakili wa Wandwe, Felix Buruda ameielezea Mahakama kuwa, wakili wa mlalamikiwaji Diamond maelezo yake ni mbinu ya kupoteza muda wangeweza kuwasiliana naye kwa njia ya barua pepe ili aweke mambo sawa.

Wakili wa Diamond kutokana na kuendelea kuieleza Mahakama kuhusu kesi hiyo, alikuwa anaeleza vitu tofauti na alichoandika kwenye maelezo ya utetezi wa mlalamikiwaji hadi kufikia Hakimu Laurent Wambili ambaye alikuwa muendesha mashitaka kutoa saa mbili pande zote mbili zijadiliane ili Mahakama iweze kuendesha kesi kwa urahisi.

Lakini Wakili wa Diamond aliomba wapewe muda wa siku moja kwani muda huo wa saa hayo anahitajika kwenda kwenye kesi nyingine Mahakama ya Kisutu ambapo
Hakimu Wambili ameahirisha keshi hiyo hadi keshokutwa Jumatano.

"Kesi ya kwanza ilisomwa Septemba 19, 2019, ikaja kusomwa Septemba 24, 2019, ikasomwa Oktoba 24, 2019 Novemba 18 zote mwaka jana, ilisomwa tena Januari 6, ikasomwa Februari 26 na leo Machi 16 mwaka huu," amesema Wandwe.

Kwa upande wa Babu Tale Mwanaspoti limempigia simu juu ya kesi hiyo alijibu kwa ufupi: "Siwezi kuongelea kitu ambacho kipo mahakamani."
 
Diamond anahusishwa vipi na kampuni(wcb), au na yeye anataka kuwa kama raisi mwenzie?
mr everything
 
miaka michache iliyopita iliekezwa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari kwamba ile nyumba thamani yake ni billions na kwamba kuna baadhi ya thamani ni za dhahabu


Sent using Jamii Forums mobile app
Acha masihala wewe yaani kuwe na nakshi za dhahabu watu waziache?

Hiyo copper tu wazee wakazi wanaweza wakatinga vilevile.
 
Watu na mbwembweee zinawatokea puani,ofisi katimuliwa na kesi juu. Bado ile anayoishi kwa sasa ,kodi ikiisha muziki mnene utatimka
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] uwiiiiiih shostie khaaaaaa navunjika mbavu huku lol

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom