Diamond Platnumz afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kuharibu nyumba aliyokuwa amepanga

Diamond Platnumz afikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kuharibu nyumba aliyokuwa amepanga

Nini nyumba hadi mchepuko anao na mtoto juu
Na Sisi vijana kwenye fursa kama hizo, huo tuko radhi tufie hata kifuani.. Huyu jamaa kama hana hta nyumba 2 na tubiashara tuwili tutatu hapa mjini atakua wa ajabu sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kakurupuka kujibu bila kuelewa anachojibu
Nazungumzia numbisa aliposema anapoishi kuwa amepanga na anangojea kodi iishe najua company hupanga
 
Milion 337 kabomoa nyumba nzima?

Ile nyumba yenyewe thamani yake sizani kama inavuka mil 100.
Duniani ukiwa.na.vijisenti tabu,ukiwa lofa ni tabu
Huyo.mwenye nyumba ni mpigaji tu,nina uhakika nyumba imeachwa vizuri kuliko ilivyokutwa
Halafu mkataba wa pango kama hausemi chochote kuhusu.marekebisho ya nyumba bila.kibali.cha mwenye nyumba,itakula kwa mwenye nyumba
 
Milion 337 kabomoa nyumba nzima?

Ile nyumba yenyewe thamani yake sizani kama inavuka mil 100.

Huwezi kuelewa hili kama hujui sheria.

Hapo kuna uharibifu, gharama za kesi, fidia na madai mengine ndiyo inafikia pesa hiyo. Kimsingi, mahakamani unatakiwa kudai kikubwa ili kikipunguzwa kibaki kiasi. Siyo unadai kidogo halafu kikipunguzwa unapata zero
 
Hayo madai mengine yapi? Kwa hiyo wewe unayejua sheria kwa mfano ndio ungeambiwa unatakiwa kulipa hela hiyo ungelipa tu eti kwa sababu unadaiwa.

Hiyo figure kaitaja yy na si mahakama na hata kama mahakama KAMA ikimkuta na makosa Diamond,wana watu wao kuithaminisha hiyo nyumba na wapo ndio watakao panga alipe kiasi gani.
 
Kwani nimesema kwamba hajaitaja yeye?

Hao wathaminishaji ni wataalamu. Na watakachopeleka mahakamani ni ushahidi wa vielelezo vya vipimo.
Kisheria, ushauri wa kitaalamu haiuwezi kuilzamisha mahakama katika maamuzi yake.

Mahakama hailazimiki kufuata ushauri wa kitaalamu.
Mhakama ndiyo itakayoamua ni kiasi gani kilipwe na siyo hao unaowasema.

Kama hujui uliza na siyo kujidai unajua sheria kumbe layman tu
 
"Mahakama hailazimiki kufuata ushauri wa kitaalamu."

Sasa mahakama watajilizisha vipi hizo 337mil bila kupata ushahidi wa kitalamu kwamba uharibifu huo ni sawa na 337mil?

Kwa hii kauli yako tu inaonyesha maswala ya kimahakama huyajui.

Kama hujui mara nyingi ushahidi wakitaalamu unaweza wa kuamua kesi kwa 97%.Hivi unawezaje kukataa ushahidi wa kitalaam kama DNA,hivi unawezaje kukataa ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wathaminishaji ardhi na majengo HOW hebu niambie MTAAAALAAAAM.

Kaa ukijua ushahidi wa kitalaamu una nguvu kubwa sana.

"Mhakama ndiyo itakayoamua ni kiasi gani kilipwe na siyo hao unaowasema."

Sasa hapa mahakama watatumia njia gani kujua inatakiwa ilipwe shilingi ngapi MTAAAAALAAAAAM.
 
We lucas
[/QOUTE] hakuna linaloshindikana ila n pale unapojaribu kulinganisha life ya ulaya na bongo zaidi unamtaja Michael Jackson na wasanii wetu hapa bongo.
ebu fikilia ikiwa kunakesi za wasanii wetu kuiba vtu kwenye hotels za watu ikawe studio ambapo wanaingia wasanii mbalimbali.?
afu kinachozungumziwa hapa ni kwamba alipanga nyumba kwa ajili ya studio sio nyumba ya kuishi.
 
Mwanamuziki Nassibu Abdul 'Diamond Plutnumz' amepelekwa mahakamani kwa tuhuma za uharibifu wa mali ndani ya nyumba aliyokuwa amepanga kwa ajili ya studio maeneo ya Sinza Kijitonyama kabla ya kuhamia Mbezi, jijini Dar es Salaam huku akidaiwa kodi ya mwezi mmoja.

Mali hiyo yenye thamani ya zaidi ya Sh337 milioni kwa mujibu wa wasanifu majengo waliifanya uchunguzi wa vitu vilivyoharibika vya Maulidi Wandwe ambazo Diamond Plutnumz anatakiwa kulipa.

Diamond amepelekwa Mahakama ya Ardhi Mwananyamala Dar es Salaam jana Jumatatu na mmiliki wa nyumba hiyo Wandwe ambapo msanii huyo hakutokea mahamani huku wakili wake Gerald Hamisi alitoa taarifa kwamba mteja wake yupo nje ya nchi hivyo kutokana na ugonjwa wa Corona atarudi nchini baada ya wiki tatu.

Aidha wakili huyo wa Diamond aliieleza mahakama kuwa kutokana na muda kwenda amefanya mawasiliano na Meneja wake Babu Tale na kwamba watalifanyia kazi suala hilo na kuliweka sawa.

Kwa upande wa wakili wa Wandwe, Felix Buruda ameielezea Mahakama kuwa, wakili wa mlalamikiwaji Diamond maelezo yake ni mbinu ya kupoteza muda wangeweza kuwasiliana naye kwa njia ya barua pepe ili aweke mambo sawa.

Wakili wa Diamond kutokana na kuendelea kuieleza Mahakama kuhusu kesi hiyo, alikuwa anaeleza vitu tofauti na alichoandika kwenye maelezo ya utetezi wa mlalamikiwaji hadi kufikia Hakimu Laurent Wambili ambaye alikuwa muendesha mashitaka kutoa saa mbili pande zote mbili zijadiliane ili Mahakama iweze kuendesha kesi kwa urahisi.

Lakini Wakili wa Diamond aliomba wapewe muda wa siku moja kwani muda huo wa saa hayo anahitajika kwenda kwenye kesi nyingine Mahakama ya Kisutu ambapo
Hakimu Wambili ameahirisha keshi hiyo hadi keshokutwa Jumatano.

"Kesi ya kwanza ilisomwa Septemba 19, 2019, ikaja kusomwa Septemba 24, 2019, ikasomwa Oktoba 24, 2019 Novemba 18 zote mwaka jana, ilisomwa tena Januari 6, ikasomwa Februari 26 na leo Machi 16 mwaka huu," amesema Wandwe.

Kwa upande wa Babu Tale Mwanaspoti limempigia simu juu ya kesi hiyo alijibu kwa ufupi: "Siwezi kuongelea kitu ambacho kipo mahakamani."
Weka Picha ya hiyo nyumba
 
Still Corona ndo main news now.
Habari za WCB zisubiri kwanza

Jiwe kasema kuwa maombi ndio dawa ya corona; inaelekea huyu na TRUMP baba yao mmoja, lakini mmoja akatokea mweusi na mwingine mweupe!!
 
Back
Top Bottom