Diamond Platnumz amewakosea nini wanaomshambulia?

Sababu kubwa ni umaarufu na mafanikio yake ndo vinavyowasumbua wengi

Umaarufu na mafanikio ya diamond yanawapa hasira sana watu ya kujiuliza kwanini wao wanashindwa kuwa km yeye? Wanachoamua kufanya ni kumchukia tu, hapo hakuna namna zaidi ya hilo la kudis kila akifanyacho

1. Wanaharakati na wanachadema watakwambia aliungana na hayati kuwakandia. Lakini ukiangalia hakuwa pekeake, wasanii karibia wote na hata viongozi walikuwepo. Sasa kwanin yeye pekeake apopolewe mawe? Unakuta sababu ni umaarufu wake wa kuweza kuishawishi hadhira ambayo hamna mtu yeyote (hata wakiungana) anayeweza kumfikia. Hapo chuki lazima izaliwe

2. Wasanii wenzake wanamchukia sababu zikiwa ni zile zile, umaarufu na mafanikio ambayo wao hata wakihangaika vipi hawayapati, Na wakienda kwake awasaidie wanataka miteremko bila kufanya kazi.. Hapo ndo utasikia jamaa mbinafsi, ana dharau, nk

Kwa sisi tuliobaki tunafata mikumbo tu ya makundi hayo mawili na ukichanganya na umackin wetu ndo boboboooh! tutamchukia hadi mishipa ya shingo itusimame
 
Mondi anachukiwa kwasababu ana hela kuwashinda hao kenge na hakuna wanachoweza kumfanya ili wao wapate nafuu mioyoni mwao lazima ashushiwe gunia la matusi na kila aina ya dhiaka. Wakijua wanamkomoa kumbe ni muda wanapoteza.
 
Naomba kujua nini kibaya diamond anakosea tofauti na wasanii wengine?

Nini afanye ili iwe sawa naonaga watu wanamshambulia ila sijawahi sikia mtu yeyote akisema makosa anayofanya tofauti na watu wengine
Mashauzi tu wakati kuimba hajui...me ndio kinaniboa
 
Uyo jamaa yenu hakuna anaemchukia eti kwa sababu amefanikiwa Kama mnavyozungumza kwani mafanikio yake sisi yanatuhusu nini mzee hata awe na hela Kama Jeff benzos atakua yeye Ila anachukiwa kwa sababu ana kelele za kijinga ,misifa ,ushamba mwingi,
Chuki zenu tuu hakuna star ambaye ana mambo yake ya ustar.ukishakuwa star kick ni kitu cha kawaida.alafu kingine hela lazima ikutofautishe mtu amenunua kigari chake imekuwa maneno angenunua kiba mngekuja kumpongeza acheni wavu watoto wakike.
 
Anatakiwa awe vipi ili asichukiwe?
Awe kama AY, Mwana FA,Proffessor Jay vile...Mziki mzuri tu na biashara zake binafsi bila makelele.

Shida ya Dimondi ni ule utandale uko damuni kilomolomo kingi makelele🤣😂🤣🤣 halafu alijiharibia toka mwanzo but ana chance ya kubadilika! Alipompataga Zari alijizolea heshima kubwa sana ila baada ya kuachana amekumbatia waswahili akaonekana hopeless kabisa!
 
Kwa hiyo akitaka kutoa nyimbo aombe ruhusa kwa wanamuziki wengine?
Konde boy naye alitoa mbona isiwe kwamba naye anamharibia kibakuli au mondi?
 
Crimea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…