Diamond Platnumz apata shavu kutoka kwenye movie ya Coming 2 America

Umesema vema, hata mimi sipingani na uwepo wa Label wala mmiliki wake kupata faida Kwasababu ule ni uwekezaji na lengo ni faida.

Ila sikubaliani msanii kuuza kwa asilimia 100 hatimiliki ya kazi zake za ubunifu.

Huo ujinga ndio mpaka leo umemfanya Saida Karoli kuendelea kuwa masikini siku zote wakati kazi zake mpaka sasa watu wanapiga pesa.

Hata bongo movie, movie za Kanumba zipo na zinarushwa kwenye TV lakini siyo mali yake tena.

Kumbuka ubunifu siyo kitu cha milele. Leo hata Ferooz, Mb doggy au Pfunk hawawezi kutengeneza hits tena.
 
Una roho ya tamaa diamond angekua star hajasaidia hao watu na akawa kafika hii hatua sijui mngesemaje?? Wote aliowaashika diamond ni east africa stars na wamefikia hatua ya kulisha familia zao kwani angewaacha wangekua wapi? Leo ? Haya maisha ni kushukuru kwa kila utakachopata.
 
Hii movie trailer lake tu ni shida, lazima wapige pesa mingi. Ni bahati mbaya tu inatoka kipindi cha Corona, lakini walitakiwa warudishe gharama zao zote siku mbili tu
 
Hilo jamaa ndio kilivyo muda wote lina frustration ya ajira.hasira hua anazimalizia kwa mondii au magufuli.
Nisivyopenda mijitu negative ni kupiga ignore tu
 
kunta kinte
Hii movie niliiona 2005 au 2006 ITV.

Alipigwa mijeledi kisa alikataa kubadili jina alilopewa na master wake. Anapewa majina John, Toby na mengine ili achague jina mojawapo. Mwamba anakataa yeye ni black na jina lake ni Kunta Kinte.

Ila mwishoni ali-give up! Mijeledi ilimzidi.
 
Hilo jamaa ndio kilivyo muda wote lina frustration ya ajira.hasira hua anazimalizia kwa mondii au magufuli.
Nisivyopenda mijitu negative ni kupiga ignore tu
Kumbe na wewe unalijua jamaa sijui ana shida gani kichwani?
 
Mbona huu utaratibu ni universal (label au management kumiliki masters ya kazi za msanii)
 
Hivi huu wimbo wa Halelujah si ndio ulipigwa marufuku na BASATA huku Tz!?

Ama kweli kama imo imo tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…