Diamond Platnumz ashangaa mwili wake kuendelea kupungua

Nobunaga

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Posts
1,205
Reaction score
5,121
Kutokana na baadhi ya mashabiki na Watanzania kwa ujumla kushangazwa na muonekano wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnum, kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu muonekano wa mwili wake akisema kuwa hata yeye haelewi sababu za kupungua.

Diamond Platnumz ameyasema hayo katika mtandao wa Instagram huku akionesha kushangazwa kutokana na kuendelea kupungua mwili wake kadiri siku zinavyokwenda. Alieleza kuwa si yeye pekee anayeshangazwa na mwili
wake kuendelea kupungua bali hata Watanzania wote wamekuwa wakiibua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.

"Halafu nimekuwa mdogo kila siku nazidi kuwa mdogomdogo. Hilo suala linawachanganya Watanzania wengi," aliandika Diamond Platnumz.

 
Atuambie ana urefu gani na kilo ngapi ili tumtafutie Body Mass Index, BMI.

Na anatakiwa ajue tofauti ya kukonda na kuwa mwembamba.

Inashangaza mtu kama Diamond kuishangaa afya yake badala ya kutumia fedha alizonazo kupata ushauri wa kiafya.

Bora ukose mali upate akili maana ukiwa na hizo mali kama akili huna, basi ni bure!
 
Mangi acha porojo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…