Diamond Platnumz ashangaa mwili wake kuendelea kupungua

Diamond Platnumz ashangaa mwili wake kuendelea kupungua

wala sibahatishi ninachoongea,nina experience na hii kitu na watu wanaonizunguka wanaotumia marijuana,bangi inakondesha mkuu acha kabisa.ninawafahamu watu kama wanne walikuwa na miili iliyonawili ila walipoanza kutumia bangi wamebaki skeleton
Ila diamond hajawahi kunenepa au kuwa na mwili mnene tangu aanza mziki ingekuwa kama alikuwa na mwili mkubwa gafla akaanza kuisha ningekubaliana na wewe
 
Kwamtazamo wangu diamondi kinacho mbeba Sana kwenye mziki nikucheza huenda take mazoezi ya kucheza ikawa sababu
 
Kutokana na baadhi ya mashabiki na Watanzania kwa ujumla kushangazwa na muonekano wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnum, kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu muonekano wa mwili wake akisema kuwa hata yeye haelewi sababu za kupungua.

Diamond Platnumz ameyasema hayo katika mtandao wa Instagram huku akionesha kushangazwa kutokana na kuendelea kupungua mwili wake kadiri siku zinavyokwenda. Alieleza kuwa si yeye pekee anayeshangazwa na mwili
wake kuendelea kupungua bali hata Watanzania wote wamekuwa wakiibua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.

"Halafu nimekuwa mdogo kila siku nazidi kuwa mdogomdogo. Hilo suala linawachanganya Watanzania wengi," aliandika Diamond Platnumz.

View attachment 2424879
Celine Dion!

Stress zinazomfanya abugie madawa ya kulevya!

Stress za muda umefika wa kulipa baada ya kupewa taji na kupandishwa kimaisha yaani kutoka kimaisha!!

Nasikia aliwahi lopoka mwenyewe kuwa atakufa mwaka fulani sijui ni huu au mwakani!

Nahisi hizo ndizo Zina mmaliza kimya kimya moyoni!!

Maisha ya utafutaji na mikataba ya kiroho sio mchezo!!!

Huwezi toboa na kuwa na maisha kama ya jamaa bila mipango ya wenyewe wenye mwanga wao wa kumulikia watu wao!!

Wa kwenda deep wamenielewa!!
 
Back
Top Bottom