Diamond Platnumz na manunuzi makubwa anayofanya

Chuki kaka.Sisi waswahili wengi wetu tuna roho mbaya mno kiasi kwamba mafanikio ya mtu mwingine yantuumiza roho mpaka kutetemeka.
Usikute kuna watu wanaogopa hata kugusa simu zao toka jana kisa dogo kanunua gari kali.
Huyu ananiponda management yake bila hata kujua imemfanyia mangapi msanii wake.
 
Mkuu Extrovert hapo kwenye biashara umegusa penyewe kabisa, me nafikiri ni kwakua wabongo wengi hawana elimu ya kibiashara hivyo wanaishia tu kuwaza biashara za mboga.

Mungu anibariki, ipo siku watu watanielewa.
 
Yaani kama kwa mkwanya na ukwasi alionao Mond,ana management mbaya na msongo wa Mawazo,basi hebu onesha hao wenye management nzuri na furaha.
Mi hapa nashauri wote wawe na "management mbaya na msongo,maana utapata pesa,
Pesa yake,katafuta kwa nguvu zake,wewe kinakuuma nini?kapambane na madaladala yako
 
We jamaa ina maana huwezi hata kujiongeza kidogo tu. Unafikiria ni watu wangapi wameajiriwa na Mond na wanalipwa kiasi gani kwa ujumla wao?

Fanya tour Marekani kaweke Kambi uhangaikie kukutana na masupastaa wa kule uone itakugharimu kiasi gani boss
 
Mwacheni mtoto wa watu mmemkalia kooni sana mpk mnatuambukiza na sisi tuanze kuchunguza vitu vyake. Mpk naona kama amekonda ameisha kabisa nuru imepotea ama kweli maneno yanaumiza sana yawe ya kweli aau uongo.
 
Kalale kijana unajua maana ya DIAMOND [emoji184] au unalia boya sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
pale mwanadamu anapojaribu kuaminisha akili yake iwe kwenye uhalisia. Tunajua kabisa kuwa snoop Dogg kitambo anajulikana afrika kama si ulimwengu mzima at the same kwa Alicia key, anachokifanya Diamond its not bad, jamaa anajaribu kumove kule ambapo wasanii wengi bongo wanataka wafike.

unamtaja jamaa anadrepression yea uenda ni kweli lakini nadhani imekaa zaidi kwenye kiu ya kuvuka hapo alipofika. Hizi social media ndo zinatufanya tuongeze chuki sababu ukinunua ka vitz wewe hapo tutaiona kwenye status. kikubwa jamaa anajiproud himself. Everyone needs the good things, stop hate...tutajipa mastress kwa ndinga za wenzetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…