Wakuu,
Naona ndugu zetu washaanza kutoa milio huko 😂
Tuliwaambia waachane na siasa wasimame na wananchi wakakaza shingo. Sasa hivi wameshatumika wanatoa milio.
Malipo ni hapa hapa duniani!
-------
Msanii Diamond Platnumz, akizungumza leo, Machi 31, 2026, katika mahojiano maalum na kituo cha redio cha Wasafi FM, Diamond ameeleza kusikitishwa kwake na namna serikali inavyomwaga rasilimali nyingi kwenye mchezo wa mpira wa miguu, wakati muziki ukipewa kipaumbele wakati wa kampeni za kisiasa pekee.
"Wanaweka nguvu sana kwenye mpira ila kwenye mziki wanadharau sana mshikaji wangu. Sisi tunaonekana tu kwenye kampeni, yaani hapo tupo 'serious', ila baada ya hapo miundombinu aaah!"