Diamond: Saida Karoli ana 25% kila pesa 'Salome' itakayoingiza

Diamond: Saida Karoli ana 25% kila pesa 'Salome' itakayoingiza

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Saida Karoli atanufaika na ‘Salome’ wimbo mpya wa Diamond ambao una vionjo kutoka kwenye wimbo wake wa ‘Chambua kama karanga’

Diamond amesema kuwa mwanamuziki huyo mwongwe wa nyimbo za asili ana asilimia 25 kwenye pesa ambazo wimbo huo utakuwa unaingiza,

“Kitu tulichokifanya kabla ya kurealise wimbo,tulizungumza na uongozi wake tukawaambia tunafanya ichi,ichi na ichi, kuna kiasi pia tukakitoaili kiende kwake alafu tukampa 25 percent ya publishing kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent” Diamond ameiambia Perfect 255.

Saida Karoli alipata mafanikio makubwa kupitia wimbo huo ikiwa ni pamoja na kutumika kwenye filamu ya muandaji maarufu wa Hollywood, Tyler Perry.

1474363288714.jpg
 
Huyo mzee Mutta ni mpigaji kinoma hapo Saida anaweza asipate hata shilling 10, maana nina uhakika hata hiyo nyimbo kutumika kwenye movie ya hollywood chini ya muandaaji Tyler Perry nasikia hakupata hata 100 na ukitaka kujua upigaji wa huyu mzee soma kitabu cha Mr II aka Sugu cha kutoka mtaani mpaka bungeni ndio utajua Sugu amefunguka sana kuna kipindi alipiga kopi kibao za Album ya Sugu afu akampa hela kidogo sana mpaka jamaa akataka kukata tamaa ya kufanya mziki kwa kifupi mzee ni dalali wa siku nyingi na anaweza akasema kuwa Saida alimuuzia rights zote za wimbo.
NB: Tusizani kasaidiwa Saida Karoli hiyo ni hela ya mzee Muta, Saida Karoli halambi hata 100 hapo.
 
Saida hana chake hapo kama Diamond angetaka kumsaidia angemfata Bukoba huko huko ampe achake mkononi ila huyo Mzee Mutta atampiga chenga ya mwili Saida ampi hata Sumni
 
Huyu Saida yupo wapi kwa sasa, na kwanini hawakuwa pamoja na Mutta siku ya makubakiano?
Yupo Mwanza hua anaimba kwenye harusi, na ubarikio wa watoto wadogo na shughuli nyingine za vijijini za kisanaa ndani kabisa(source mtu wake wa karibu). Kifupi amechoka sana kwa sasa hata huyo meneja akimpa laki 2 kwenye huo muamala wa diamond atamshukuru sana tena kwa kupiga magoti.. Acha mzee apige pesa mjini shule..
 
Aisee, Mutta ni konyo.
Mpaka Saida amefikia kupiga show za hivyo, serious inatia huruma.
 
Aisee, Mutta ni konyo.
Mpaka Saida amefikia kupiga show za hivyo, serious inatia huruma.
year.. M.r that is how life is.. ukipata fursa itumie kisawasawa (saida karoli enzi hizo) ukiwa kwenye fufsa itumie kisawasawa(mzee wetu)
 
Back
Top Bottom