Diamond umemsifia Rais Samia kwa Mafanikio yaliyotoka kwa Magufuli

Diamond umemsifia Rais Samia kwa Mafanikio yaliyotoka kwa Magufuli

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Msanii Diamond karibia hayo Mafanikio yote uliyoyaonyesha katika Video ya huo Wimbo wako (Kichupa Chako) ambayo kama kawaida ya Mr. Kiherehere Gerson Msigwa (Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo) kaishea Mitandaoni akidhani Mama atafurahi na Kumrejesha tena Ikulu anakokupenda kweli kweli yameletwa na Hayati John Pombe Magufuli.

Kwa Mimi GENTAMYCINE nitaanza kupima Mafanikio ya Rais Samia na Kuyahesabu pale tu kama akibahatika tena kuwa Rais kwa mwaka 2025 hadi mwaka 2030 lakini kwa sasa wenye Akili timamu wote (siyo Wendawazimu, Wanafiki na Chawa) kama Msanii wenu huyu tunajua kuwa Maendeleo ya sasa ni ya Magufuli tu.

Yanayotekelezwa sasa na Rais Samia yalikuwa ndani ya Ilani ya CCM ya mwaka 2020 iliyokuwa chini ya Mbunifu na Mwerevu John Pombe Magufuli huku Makamu wake akiwa ni Samia Suluhu Hassan hivyo Logically tu (labda kwa Mpumbavu) ndiyo hatojua kuwa Maendeleo ya sasa yalikuwa ni Maono yake Magufuli.

Diamond Wimbo wako huu wa Kichawachawa kwake Rais Samia ili nae akiupenda basi uombe kuonana naye ili ukamwombe akusaidie Kupunguziwa Kodi unayodaiwa na akupe Favor katika Mgodi Mmoja au auchune ukiingiza Mzigo wako kutoka Copa Cabana Brazil ungependeza kama ungetoa mwaka 2029, ila siyo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom