Nyie watu mnamuandama sana huyu kijana, aandamane na fikra zenu. Kwani hajaingia kwenye siasa, si kaingia na kachagua upande anaotaka.
Hata marekani kipindi cha vuguvugu la uchaguzi wasanii wengi walichagua pande zao, weusi wengi walimpinga trump lakini wapo baadhi yao waliomuunga mkono pia, haijarishi ni upande mbaya kwako ama ni mzuri kwa maono yake kaona hivyo.
Jamii imegawanyika mkuu, tukio moja linaweza kuonekana tofauti kwenye macho ya kila mtu eidha kutokana na uelewa au matakwa ya mtu binafsi. Kwahiyo huwezi kuiridhisha jamii yote. Nikupe mfano Ney wa mitego nae anaimbaga sana nyimbo uzipendazo(za kiharakati) angalia mapokeo ya nyimbo izo kwenye jamii, sia ajabu hata wewe huzifatilii na ile ni biashara so inabidi nae amix kidogo apate chochote.