Diamond Ushakosa Tuzo, Jua Nafasi yako. Achana na Washamba

Diamond Ushakosa Tuzo, Jua Nafasi yako. Achana na Washamba

Nafikiri mshamba wa kwanza ni huyo kaka Yako. Mtu ukikosa ulichotaka alaf ukaanza kuhamaki pia NI u shamba.
 
DIAMOND ACHANA NA WASHAMBA/MALIMBUKENI. TAMBUA NAFASI YAKO.

Na, Robert Heriel

Kitu ambacho kinakwamisha Watanzania tuliowengi ni USHAMBA/ULIMBUKENI.

Ulimbukeni ni like kitendo cha mtu kupata kitu Kwa kizuri au cha thamani Kwa mara ya kwanza, kitu kile kikamfanya atende kinyume na desturi na maadili yanayomzunguka mtu huyo.

Kwa Kiswahili cha kisasa neno Limbukeni ni USHAMBA.

Watanzania wengi ni MALIMBUKENI.
Wengi hatuna Exposure ya mambo yalivyo.

Tuna ulimbukeni karibu kwenye kila Nyanja za maisha.

Yapo malimbukeni ya Madaraka, unakuta jitu likipata uongozi tuu linafanya mambo ya hovyo kabisa. Tumeshayaona hayo malimbukeni, Washamba wa Madaraka.

Wapo Malimbukeni wa Michezo Kama mpira, hayo tumeyaona hata kwenye mashindano ya Club bingwa.
Maneno mengi uwezo mdogo, sifa moja wapo ya Limbukeni au mshamba utaiona kwenye maneno.
Limbukeni hujiinua zaidi kwenye mdomo kuliko vitendo.

Yapo malimbukeni wa Muziki na Umaarufu, haya mengi tunayaona kwa hawa Wasanii WA muziki na maigizo.
Kwa vile mtu hajawahi kuwa Maarufu haya alipokuwa shuleni basi akiwa mkubwa akiwa Maarufu sio ajabu akafanya mambo ya ajabu.

Sio ajabu jitu kuonyesha uchi wake mitandaoni, huo ndio ushamba WA umaarufu, sio ajabu mtu kuvujisha video za uchi au akinyonya denda akiwa anajirekodi. Huo ni Ulimbukeni.

Yapo Malimbukeni ya Fasheni, hawa wengi wao ni Wale waliotoka kijijini kwenda mjini, au waliotoka Tanzania wakaenda ng'ambo huko Ughaibuni.
Hawa wanajikuta wakitoboa masikio na pua ilhali wao ni wanaume.
Wengine wakitoa Marinda Kama Fasheni.

Diamond ni Msanii wa kawaida Kwa wanaoijua Dunia. Ila hapa Nchini ni Msanii Mkubwa.
Diamond ili awe Msanii Mkubwa Duniani lazima aache Ulimbukeni na ushamba.

Asifuate maneno ya Malimbukeni na Washamba ambao Kwa hapa TANZANIA ni zaidi ya 80% ambao ni Washamba.

Ogopa kushabikiwa au kufuata maneno ya watu ambao wanaona kuwa na simu Janja kamaiPhone ndio ujanja.

Ogopa kuwasikiliza watu wanaoona kuwa na Ghetto lenye Flat screen ya inchi 32 ndio kutusua maisha.

Ogopa kushabikiwa na kusikiliza maneno ya washabiki ambao kuwa na Gari ndio kutusua maisha.

Ogopa kushabikiwa na Mashabiki ambao hawataki kununua kazi zako Kwa njia Halali isipokuwa wanaenda Kuburn CD au kurushiwa kwenye muziki library ambazo hazijasajiliwa.

Ukitaka ujue Watanzania wengi ni Limbukeni ni siku uonekane kwenye TV utashangaa ndugu zako na marafiki watakavyokupigia simu na kukusifu.

Ulimbukeni unaitesa nchi hii karibu kwenye kila Nyanja za maisha.
Kiongozi akijenga Ka-Flyover utaona atakavyopiga kelele. Ulimbukeni mtupu!

Limbukeni hatajuagi nafasi zao ndani ya jamii.

DIamond huenda alikuwa hana interest za kutetea Haki za watu ndani ya jamii lakini Nafasi aliyonayo kimuziki ndani ya nchi unanilazimisha kutetea Haki za jamii Apende asipende.

Sasa unakuta jitu Limbukeni linakuambia sio lazima Diamond ajiingize kwenye mambo ya Siasa na uanaharakati hapo ndio unajua mtu huyo Hana Uelewa wowote wa jinsi Dunia inavyoenda.

Mtu unaweza usiwe na interest ya mambo ya Siasa lakini Nafasi yako ndani ya jamii ikakulazimisha kuingia huko.

DIamond wewe ni Msanii Mkubwa hapa Afrika Mashariki, bado unatakiwa ujitahidi uwe Msanii Mkubwa Afrika, ndipo uende Duniani.

Diamond ulichofanikiwa ni katika Propaganda Kwa Limbukeni wa TANZANIA kuwaaminisha kuwa wewe ni Msanii Mkubwa Duniani nao wanaamini hivyo.

Lakini unaowaaminisha ni watu ambao hata hawajui Duniani ni wapi licha ya kuwa wanaishi sehemu ya Dunia.

Hata hivyo sitaacha kukupongeza Kwa hatua uliyoipiga kimuziki kwani sio haba. Ila zingatia kuwa bado unasafari ndefu kuwa Msanii Mkubwa wa Afrika na hatimaye Msanii wa Dunia.

Ulimbukeni ndio kikwazo kikubwa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Mvomero, Morogoro
Dogo kakosa tuzo achaneni naye.....mwacheni apambane na maisha yake halisi ya Tandale ya kupiga watu majungu. Watanzania hawakutaka ashinde, yeye akabisha akaenda Marekani baada ya kufanyiwa kafara na Mama yake ili ashinde.
 
ipo hivi, hakuna anaye furahia anguko la mwenzake, na walla diamond bado hajaanguka, tena mondi bado ni kijana mdogo hivyo bado ana nafasi ya kujisahihisha pale alipo jikwaa, wakosoaji wake tunamlaumu kwa kushinda kwake kukosoa maovuna mabaya yanayo tendeka na yaliyo tendekeka ktk jamii ambayo yeye anaishi na alipo tokea, yeye kama msanii aliyechomoza na kutokea ktk familia / jamii ya kimaskini ameshindwa kupaza sauti yake nzuri tuu ktk kuitetea jamii aliyotoka kama walivyo fanya manguli wezake kama vile Bob Marley, Luck Dube, Snoopy, Fella Kuti, etc tena yeye alikuwa na nafasi ya kuuwa ndege wawili kwa jiwe mmoja maana bado anakumbatiwa na watawala madhalimu hivyo angeweza kuwatupia jiwe mmoja tuu jepesi japesi ktk kukemea mateso /manyanyaso wanayo / waliyo pata pata hata wasanii wenzake au hata jamii aliyotokea ya tandale kwa mtogole n.k………………….
 
👏👏👏👏

Kujifunza ndio kufanikiwa.

Hakuna mwisho wa kujifunza
 
Watu hawakupangii maisha Ila interest na position ya mtu ndio humpangia maisha mtu
Interest yes (mtu anafanya kile anachopenda ili mradi asivunje sheria)..., Position inategemea kama unaomba position yenye sheria fulani (mfano ya sheikh, padri n.k.) inabidi ufuate hizo sheria sababu position requires it na hutaki kufuata hizo sheria unaachia position.

Tukija kwenye huyu dogo ni msanii / muimbaji (first and far most ni kutoa kazi zake) na sababu watu wanazinunua basi he is doing something right..., anakidhi matakwa yake (ambayo ni kupeleka mkono kinywani na kuwahudumia jamii yake) hayo mengine ni extras ambayo sio obligation yake (anaweza akafanya au asifanye)...

Hizi pressure na life of stress (kuishi maisha ya watu wanataka nini na sio unataka nini) ndio yanapelekea stars wengi worldwide kuwa na maisha yenye stress na wanaishia kwenye addiction and sadness
 
Dogo kakosa tuzo achaneni naye.....mwacheni apambane na maisha yake halisi ya Tandale ya kupiga watu majungu. Watanzania hawakutaka ashinde, yeye akabisha akaenda Marekani baada ya kufanyiwa kafara na Mama yake ili ashinde.

Kwenye maisha kuna makundi mawili;
Maadui na Marafiki

Maadui hukuimarisha

Marafiki wapo Aina mbili;
Rafiki mnafiki
Rafiki WA kweli.

Rafiki mnafiki huyu ni Kama informer WA maadui ambaye kazi yake ni kutoa taarifa zako Kwa maadui ili ukwame.

Maadui mara nyingi huwa Real
Ila marafiki huwa wanafiki.

Hata hivyo washindi wote hujichunga wawapo mbele za Rafiki zao kuliko wawapo mbele za adui zao
 
Interest yes (mtu anafanya kile anachopenda ili mradi asivunje sheria)..., Position inategemea kama unaomba position yenye sheria fulani (mfano ya sheikh, padri n.k.) inabidi ufuate hizo sheria sababu position requires it na hutaki kufuata hizo sheria unaachia position.

Tukija kwenye huyu dogo ni msanii / muimbaji (first and far most ni kutoa kazi zake) na sababu watu wanazinunua basi he is doing something right..., anakidhi matakwa yake (ambayo ni kupeleka mkono kinywani na kuwahudumia jamii yake) hayo mengine ni extras ambayo sio obligation yake (anaweza akafanya au asifanye)...

Hizi pressure na life of stress (kuishi maisha ya watu wanataka nini na sio unataka nini) ndio yanapelekea stars wengi worldwide kuwa na maisha yenye stress na wanaishia kwenye addiction and sadness

DIamond position yake unaijua kwenye Muziki Mkuu?
 
DIamond position yake unaijua kwenye Muziki Mkuu?
Yeye mwenyewe ndio anaijua kuliko hata mimi na wewe..., Let the Boy enjoy his time in the limelight.... It will come the time when he will be yesterdays news..., And the best consolation will be I did enjoy the ride....

Watanzania tupunguze kuwavika mizigo watu.., mfano Samatta amekwenda England kila mtu anamvika matarajio yake...., tuwaache hawa wasanii wa-enjoy maisha yao (its hard enough bila kuwaongezea matarajio yetu)
 
Kuna almasi ilijidai kua juu ya mungu, ika try kuwa juu kizungu

Mwisho wa siku ikaja kubebwa kama nyanya iliyo juu ya fungu
 
Burna boy yuko ndani mond ni mlinzi, ingia kwenye BET mond mshindani burna boy ndo mshindi.../

ukimuona burna sizi usimchukulie kipimbi, Wakati niger master anaheshimika kama dingi.../
 
Yeye yupo taifa la mvomero kule USA ya turiani
ana fanya nini sasa shughuli ishaeleweka sio yake?

Ama kweli ningelua mtoa tuzo wa hiyo tuzo ningemchagua diamond ndo amkabidhi burna boy tuzo yake

Yap naye angalau hata aishike aone ni namna gani inavutia ikowezekana hata picha apigie
 
Back
Top Bottom