Diana Bundala aka Mfalme Zumaridi, afikishwa Mahakamani akikabiliwa na kesi tatu ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu

Diana Bundala aka Mfalme Zumaridi, afikishwa Mahakamani akikabiliwa na kesi tatu ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mchungaji Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayokabili.

Msafara wa magari matatu aina ya difenda zilizolindwa na askari waliojihami kwa silaha umewasili katika mahakama hiyo saa 9:00 mchana kisha watuhumiwa hao kuamuriwa kuingia ndani ya mahakama hiyo.

Akishuka katika gari ya polisi iliyokuwa imembeba, Zumaridi amesikika akisema "Mimi ndiyo Mfalme’ huku akionyesha ishara ya kuomba.

Miongoni mwa waliofanikishwa mahakamani hapo wakiwa na mhubiri huyo ni vijana wanaokadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 45 na wazee wa jinsia zote wanaodhaniwa kuwa na umri kuanzia miaka 45 hadi 65.


Source: Mwananchi

zuma-pic.jpg

=====

Mfalme’ Zumaridi, waumini wake kizimbani, wakataa dhamana

Mwanza. Diana Bundala maarufu kama ‘mfalme Zumaridi na wenzake 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na kesi tatu ikiwemo usafirishaji haramu wa binada, shambulio la kudhuru mwili na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu.

Mwendesha mashtaka wa serikali amesema katika kesi namba 10/2022 inayomkabili Zumaridi peke yake akidaiwa kusafirisha binadamu wakiwemo watoto wenye umri chini ya miaka 18 kinyume cha kifungu namba 4(1) (A) na 6(2) (A) cha sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu namba 6 ya mwaka 2008.

Katika kesi namba 11/2022, Luvinga amesema Zumaridi na nwenzake wanane wanadaiwa kufanya shambulio la kudhuru mwili askari wa Jeshi la Polisi waliofika nyumbani kwake kutekeleza wajibu wao kinyume cha kifungu namba 241 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa kuwazuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao kinyume cha kifungu namba 114(A) kifungu kidogo B cha Kanuni ya Adhabu.

Katika kesi namba 12/2022, mwendesha mashataka huyo aliiambia Mahakama mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Monica Ndyekubora kuwa Zumaridi na wenzake 92 wanadaiwa kufanya kusanyiko lisilo halali kinyume cha kifungu cha 74(1) na 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Washatkiwa walikana mashtaka yao katika shauri namba 11 na 12 huku upande wa Jamhuri ukiieleza Mahakama kuwa upeleleza kuhusu mashauri hayo mawili umekamilika na kuomba kupagiwa siku ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Kuhusu shauri namba 10 la usafirishaji haramu wa binadamu linalomkabili Zumaridi, mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Licha ya mashtaka namba 11 na 12 kuwa na dhamana huku baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamejitokeza kuwadhamini, washtaki wote wanaowakilishwa na Wakili Erick Mutta walikataa dhamana wakisisitiza kuwa wako tayari kwenda mahabusu kuungana na kiongozi wao anayekabiliwa na kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu isiyo na dhamana.

Kutokana na uamuzi huo, Hakimu Ndyekubora ameamuru washtakiwa wote kupelekwa mahabusu hadi Machi 17, shauri hilo litakapotakwa kwa ajili ya washatakiwa kusomewa maelezo ya awali katika shauri namba 11 na 12.

Pia, soma;

1). Mwanza: Polisi yamkamata Mfalme Zumaridi. Anatuhumiwa kwa kosa la usafirishaji haramu wa watu wapatao 149

2). Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

3). Mfalme Zumaridi ni nani haswa?

IMG-20220303-WA0010.jpg
Mfalme Zumaridi (Mwenye sweta la bluu)na wenzake 92 wakitoka kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza kusomewa mashtaka yanayowakabili.
 
Kufuatia kukamatwa kisha kufikishwa mahakamani leo kwa kwa Diana Bundala maarufu mfalme Zumaridi yeye na wenzake 93, imebainika kuwa wafuasi wake wengine wamekimbilia mkoa wa Tabora kata ya Kitete mtaa wa Kariakoo na kuanzisha kanisa liitwalo Bethel na kulijenga katikati ya barabara, kufunga maturubai na kuendesha ibada bila usajili wa kanisa, kuendesha ibada bila kibali cha muda kutoka mamlaka husika, kujenga bila kibali cha ujenzi kutoka manispaa, kufunguliwa muziki kutwa kucha kwa sauti ya juu sana, kutoa mahubiri ya uchochezi wa kidini na kisiasa, kudai wanatoa rushwa hadharani kwenye spika kuwa viongozi wa mkoa mzima wa Tabora wameuweka mfukoni, wadai wanalindwa na diwani wa kata ya Kitete msukuma mwenzao na mchungaji mwenzao, haya viongozi wa Tabora, Mwanza kuna watu wenu huko Tabora wafuatilieni kwa kina.
 
Back
Top Bottom