Diana Bundala aka Mfalme Zumaridi, afikishwa Mahakamani akikabiliwa na kesi tatu ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu

Diana Bundala aka Mfalme Zumaridi, afikishwa Mahakamani akikabiliwa na kesi tatu ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu

Kosa lake ni nini?

Kosa Ni kuzuia polisi wasitekeleze summons waliyopewa na mahakama kwenda kumchukua mtoto ambaye mama yake amaekatalia huko kwa Zumaridi na wanaishi huko pamoja na Zumaridi, naa kusoma hasomi.

Hivyo baba wa mtoto kaamua kufile application kwaajili ya custody ya mtoto atoke huko kwa Zumaridi, maana hasomi wapo tu huko na mama yake na mama yake amegoma kuondoka kwa zumaridi na kuamua kuvunja ndoa.

Shida ilikija pale ambapo polisi wameenda wakafukizwa na makerubi au malaika wa zumaridi na kushindwa kumchukua mtoto. Hivyo polisi waliamua kuja Mara ya pili ndipo walipopata uhalifu mwingine unafanyika.
 
Sid
Kufuatia kukamatwa kisha kufikishwa mahakamani leo kwa kwa Diana Bundala maarufu mfalme Zumaridi yeye na wenzake 93 , imebainika kuwa wafuasi wake wengine wamekimbilia mkoa wa Tabora kata ya Kitete mtaa wa Kariakoo na kuanzisha kanisa liitwalo Bethel na kulijenga katikati ya barabara , kufunga maturubai na kuendesha ibada bila usajili wa kanisa , kuendesha ibada bila kibali cha muda kutoka mamlaka husika , kujenga bila kibali cha ujenzi kutoka manispaa , kufunguliwa muziki kutwa kucha kwa sauti ya juu sana , kutoa mahubiri ya uchochezi wa kidini na kisiasa , kudai wanatoa rushwa hadharani kwenye spika kuwa viongozi wa mkoa mzima wa Tabora wameuweka mfukoni , wadai wanalindwa na diwani wa kata ya Kitete msukuma mwenzao na mchungaji mwenzao , haya viongozi wa Tabora , Mwanza kuna watu wenu huko Tabora wafuatilieni kwa kina .

Sidhani Kama wana ukaribu na Zumaridi Hawa no wengine tofauti.
 
Mchungaji Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayokabili.

Msafara wa magari matatu aina ya difenda zilizolindwa na askari waliojihami kwa silaha umewasili katika mahakama hiyo saa 9:00 mchana kisha watuhumiwa hao kuamuriwa kuingia ndani ya mahakama hiyo.

Akishuka katika gari ya polisi iliyokuwa imembeba, Zumaridi amesikika akisema "Mimi ndiyo Mfalme’ huku huku akionyesha ishara ya kuomba.

Miongoni mwa waliofanikishwa mahakamani hapo wakiwa na mhubiri huyo ni vijana wanaokadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 45 na wazee wa jinsia zote wanaodhaniwa kuwa na umri kuanzia miaka 45 hadi 65.


Source: Mwananchi

View attachment 2137530
Hivi hayo Magari ni Defender na sio Land cruisers?¿
 
Macho ya rohoni yanahitajika katika hili sijasikia lolote kutoka kwa Mitume na Manabii wa nchi hii juu ya mwenendo tofauti wa dada ZUMARIDI
 
Mleta mada mwongo mkubwa hilo kanisa limekuwepo muda mrefu na mleta mada amekuwa mkorofi muda mrefu dhidi ya hilo kanisa amekuwa akijaza mifitina kibao kuibusu hilo kanisa muda mrefu hum Jamii forums

Ana pepo mchafu kaanza.muda mrefu sana kulipakazia hill kanisa la Bethel sasa kaamua kutunga uongo kuwa hao wa Zumaridi
 
Waacheni waabudu Kwa Amani ,hzi ni fitina za kidini tuu , wakat dini karbia zote zimejaa upigaji
 
Acheni watu waabudu kwa amani.


Uhuru wa kuabudu ulitafutwa kwa damu nyingi sana.

Tuvumiliane, imani ni kitu kipana sana...

Wengine wanapakwa majivu wanaaminishwa

Wengine wanapigia magoti sanamu

Wengine wanaongea lugha zisizoeleweka.

Wengine wanawafundisha waumini wao mambo ya kijeshi.

Tuvumiliane!!!!!!
 
Back
Top Bottom