Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

This is fact
Kuna bwana mi natumia gharama zangu kudownload movies na series ye ashanigeuza mi studio kila weekend a nakuja Kwang kunyonya
Halafu Anafanya kazi sehem yenye WiFi

Namuelekeza jins ya kudownload et anasema inachukua muda mrefu

Hiyo shida ya Mtanzania mnayejuana.......
 
Hapa ukifika reception tu unakaribishwa na glasi ya juice ya entertainment, hawa jamaa wako vizuri.
 
Tema cheche mkuu, tema cheche...
Eti standard za juu?! Standard za juu utazipata hapa TZ na elimu yako (kama unayo)..
Kama ni swala la maji kutiririka ndani hata hapa lipo, kama umeme upo, hata kama ni mangumashi, kama vyakula wanavyotaka vipo TZ, tena fresh, sio vile vya kupiga sindano na viko frozen miezi 6..
Standard za juu wanazozungumzia labda ni uhakika wa elimu, malazi na afya, na kwa watoto wao, ambalo wengine watasema kweli, maana hakuna utajiri mzuri na wa uhakika utakaomuachia mtoto kama elimu...Hapo tumekubali kwa hilo...
Ila ukumbuke mpaka umefika huko ina maana hata wewe ulipata elimu fulani huku, je haikutosha kwa wewe kuajiriwa kwenye fanu yako? Je ulijiendeleza tena uwe sawa na standard zao za elimu?..
Haya , baada ya watoto kukuwa itakuaje? Maana unazeeka, unalinda magodown, factories etc, labda unafanya kazi za Care, mpaka lini? Au umeajiriwa kwenye Food Factories, kuna baridi kufa, kwa kazi za usiku mwili lazima uchoke tu...
Bado mbishi, je utaendelea kuwepo huko na ulipwe Pension kwenye nyumba kama za NHC huku kila wiki au ungependa uwe hapa na kajumba kako, kagari kako, mradi wako, uwape ajira Watz wafaidike na Mtz mwenzao aliyepata ujuzi huko..
Kwa kweli ni uamuzi wa mtu kweli, ila lazima ufike muda useme, tayari future ya watoto iko sorted, ya kwako je?!

Wanaotaka kurudi jipangeni, anza na sehemu ya kufikia, lete usafiri wako, njoo na ujuzi wako uliosomea huko, kama bado somea sasa, njoo na kamtaji, mambo swafi tu..
 
Dar stinks[emoji16] [emoji16] [emoji16] siku moja nikawa Moshi, nkaona si mbaya nikanyooshe miguu. Sasa nkaenda mpaka maeneo ya kiwanda cha ngozi, nkakuta siku hiyo walikuwa wanatoa maji ya kulowekea ngozi. Palikuwa na harufu kali mbaya ambayo unaisikia kutokea kama kilometa 3. Ajabu watu wanaishi pembeni ya kiwanda hata hawana shida.
Bongo wengi tunaishi na uchafu hata hatuoni shida
 
I’d say true....

Dar stinks....Mwenge smells like sewage. Vingunguti has a nasty smell too. The whole city is dirty. The airport is dirty. A lot of people are dirty. Hahahaaa
Aisee...mbona unatutukana?
 
Babu ushawahi kwenda Mwenge hususan mle wanapotengenezea kucha wadada?

Wana diaspora Leo mmeamua aiseee...hahahahahahshaaha . Ila mtu ukisoma huu uzi tofauti ya exposure iko dhahiri Kabisa!

Kuna Watu bongo wameshazoea uchafu kiasi kwamba (especially pubs) hawawezi kutofautisha uchafu na usafi tena. Bongo ni kawaida bia kuinywea pembeni ya choo na nzi WA kutosha wakiwa wanarukaruka.....kwanza Mimi nadhani wabongo tuna immunity Kali sana.

Maana kuna uchafu mwingine ni beyond imagination ya kawaida.
 
Wewe ni kichwa, tapeli mjanja 😛
 

Yaani uagize kiti moto halafu nzi wasikidandie? Uagize chipsi vumbi halafu usifukize nzi?

Na ni kweli. Watanzania wengi wana immunity kali sana.

Vi ‘groceries’ na vi ‘pubs’ vilivyopo karibu na uchafu ni vingi mno. Ngoja nitapiga picha nizirushe humu.
 
Ukisema na kuwaza tofauti na wanavyowaza, wanakuona una maringo, oh, unajifanya mzungu n.k.!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…