Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mbona wenzenu wanasema Tz ni kuzuri Ulaya/US/Japan waTz wanateseka!
Tanzania kuzuri wewe!
Tanzania watu hawaishi kwenye vi apartments!
Tanzania watu hawaishi paycheck to paycheck!
Tanzania watu wana disposable income ya kumwaga.
Tanzania watu hawana mortgage za miaka 30. Wanamilikia ‘majumba’ yao free and clear!
Tanzania watu wanavaa luxury brands kila sehemu. Yaani hata ukienda pale Mwenge madukani unakuta Moschino, Gucci, Burberry, Fendi, Chanel, n.k. zinauzwa kwa bei rahisi sana ambazo Watanzania wengi wanazimudu. Ulaya na Marekani hizo kuxury brands ma diaspora wengi wa Kitanzania hawawezi kuzimudu gharama zake. Lakini hapa bongo unakuta zinauzwa nje tena zinaning’inizwa au zimetandazwa kwenye mkeka.
Tanzania watu hawaishi na roommates maana wana majumba mengi mengi tu na hivyo hawana sababu ya kubanana banana.
Maji hayakatiki Tanzania. Umeme haukatiki. Mabarabara ni mazuri.
Yaani kwa ujumla viwango vya maisha Tanzania viko juu sana kuliko Ulaya na Marekani.
Cheki Mwenge hapo...hapo huko luxury brand yoyote ile. You name it, they got it.
Kama mchuchu wako anapenda red bottoms we nenda Mwenge tu...utapata.