Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

Hapo kwenye "nchi ngumu hii"

nakuunga mkono asilimia mia sijui tufanye nini watoto wetu wasiishi hivi wazee wetu walivyotuachia
Njooni tubadili katiba wote ili tuishi nchi ya asali na maziwa kama muishivyo.
Mukituachia sisi tuwe wahanga nyie muje kuishi kwenye barabara za vioo hamtaishi ndoto yenu.
 
Aisee mie naogopa kuumwa,ningekua mzima na sina hayo maradhi niliyonayo ningerudi.Tanzania kuna fursa nyingi za mtu kujiendeleza kwa sababu nchi yetu bado inakua,a lot of opportunities ,Tanzania ukiwa broke utalima nje viazi,utakula,ulaya ukiwa broke ni hadithi nyingine,lol
ARV huku zipo,na ni bure wala siyo zile za Madabida,njoo tu.
 
Tatizo wanalokosea ni ku loos touch na tz mm binafsi nimeishi mbele miaka ya kutosha ila nina mpango 2020 nirudi hme nilichofanya nimenunua mashamba
mifugo pia nimeanzisha kilimo nataka pia nifungue shebeen/bar/hotel moja ya wastan very classic nadhani nitakuwa vema kimtindo siwezi kufia nchi za wazungu hilo nimekataa nimeisha tengeneza connection ya kuuza nyama SA na Congo kuna uhitaji mkubwa wa nyama ya ng'ombe
Natamani niombe kazi kwako, kazi ya kumanage shamba/ranch, nina ka uzoefu[emoji28] [emoji28] [emoji28]
Mkuu sijui upo nchi gani lakini nisaidie kutafuta nafasi katika kampuni za kutengeneza tofali/clay soil bricks au zinazofanya tyre retreading, katika nchi za Canada, USA, England, Australia. Nataka nijifunze hizo kazi katika kiwango bora sana. Nakutumia e-mail yangu kwenye inbox tafadhari.
 
611a96f9ecc918bcfec228e070de43a6.jpg
65c138f2b4cbe08773c90e603f01255e.jpg

Huu ndio ujinga wa diaspora. Jamaa wa Nebraska hawana hamu na mwaka mpya. Baridi ni nyuzi -12 F kwa bongo ni nyuzi -24.44 c. Yaani ni sawa na kuishi ndani ya friji.
 
Aisee sasa kama Bongo ni nyuzi -24 si ndio balaa zaidi?! Natumaini ulimaanisha 24c
 
Aisee sasa kama Bongo ni nyuzi -24 si ndio balaa zaidi?! Natumaini ulimaanisha 24c

-12 degrees fahrenheit =
-24.444 degrees celsius

Hiyo ishirini na nne iwe negative. Geuza ukali wa joto uwe ukali wa baridi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo kubwa linalokatisha tamaa kurudi Bongo ni institutionalised ‘petty’ corruption, na huduma mbovu za kijamii kama vile maji, umeme, afya, elimu, mfumo wa usafiri na usafirishaji.

Mpaka pale CCM itakapotoka madarakani, na kuingia watu wasio masalia ya CCM, ndipo Tanzania inaweza kutatua hizo changamoto.

Until then, kurudi ni vigumu
Halafu unakutana na mjinga anafananisha standard ya maisha Tz na first world!
 
Kurudi na kuishi na Tanzania ni sawa kujihukumu kifo chako mwenyewe huku ukiwa selo ukingoja utekelezaji wa hukumu yako.....

Tanzania hakuna tumaini la maisha unless umetokea kwenye familia zilizo kwenye system other wise kila kitu kwako ni kamari

Ni kama msituni ambapo kila mnyama anaangalia namna yake ya ku survive.....

Nchi haipo organized kwenye mambo mengi sana ya msingi........

Kuishi Tanzania ni gharama kubwa ambapo hiyo inaweza kuku gharimu hata maisha yako.....

Just imagine

Unajibana bana unajenga nyumba nzuri ya kuishi ambapo unatakiwa utafute kampuni ya ulinzi kwa ajili ya usalama wako.....unatakiwa uwe na generator kwa ajili ya kujihakikishia upatikani wa nishati ya umeme au solar power.....unatakiwa uchimbe kisima kwa ajili kujihakikishia upatikanaji wa maji hapo kwako......bila ya kusahau unatakiwa uwe na usafiri kwa ajili kurahisisha mambo yako....vile vile unatakiwa uepukane na shughuli za usiku zisizo na ulazima kwa ajili ya usalama wako......ukitoa hela kwenye ATM machine unatakiwa ujifiche kwa usalama wako......

Kumbuka kuwa unayafanya yote huku ukiwa unalipa au kukatwa kodi katika huduma au bidhaa unayo nunua.........

Tanzania kubadilika ni mpaka lije gharika na kuangamiza uzao wote wa wanasiasa wa sasa....na kuanza upya.......
Mbona wenzenu wanasema Tz ni kuzuri Ulaya/US/Japan waTz wanateseka!
 
Mimi nilivyoondoka Tanzania nilishaamua kuondoka kimoja na kurudi Tanzania likizo tu. Kwa hiyo ushauri kutoka kwangu ni vigumu.

Nilipoondoka Bongo kuna mzee wa busara aliishi sana Sweden. Aliniambia wewe nenda tu lakini utakumbuka uchafu wetu huu.
Nimemuamini. Yaani kinachonirudisha Bongo ni misele ya jogoo. Namisi purukushani za jogoo akifukuza kuku. Kuna haja ya jogoo kushtakiwa kwa ubakaji wa hadharani. Amini usiamini raha ya kula kuku inaweza kukutoka kama kuku wenyewe huwaoni.
 
Angalia tu jogoo asije kukula mpaka wewe.
 
Maisha ya nje yana ufeki fulani. Sasa rafiki yako mnigeria rafiki yako mchina. Mtabishana vipi Simba na Yanga?
Ukipita mtaa wa Samora hukosi kukutana na classmates. Panda treni nje mchana kutwa hutakutana na mtu unaemjua. Labda uende Reading Uingereza.
 
Unaweza kuwa unajifunga mawazo katika mambo makubwa kwa sababu ya mambo ya kijinga tu.

Si kila mtu anaendekwza unayoona ya muhimu wewe.

Na hata kama anaendekeza, si lazima aendekeze kama unavyoendekeza wewe.

Classmates mbona wamejaa Whatsapp na mtu anaweza kuwa nje akawa anakutana na classmates wengi kuliko aliye Tanzania.

Na wengine ni mizinguo tu.

Ushabiki wa Simba na Yanga si kila mtu anataka. Na ukitaka hukosi watu wa kushabikia nao mitandaoni.

Kila mtu aamue anavyotaka kukaa.

Ukiamua kukaa nchi ambayo Magufuli anaweza kukutaifisha mpaka mkeo azae naye utakuwa umeamua kitu kilicho ndani ya uhuru wako wa kuamua.
 
Ndio ufeki wenyewe huo kukutana kwenye what’s up. Mpira taifa unakurupuka tu unaenda hakuna cha season tickets, sijui ununue online aaagh!
 
Ndio ufeki wenyewe huo kukutana kwenye what’s up.
Hapana. Inawezekana ni kwenda na wakati tu. Wewe mwenyewe upo mtandaoni hapa. Ina maana unaishi maisha feki hapa?

Pia. Hata mtu akisema hataki kusikia habari za classmates, anataka kuishi maisha mapya Marekani, akaenda kuishi huko, huo ni uamuzi wake hamna ufeki hapo.

Labda katika ma ckassmates ndio kuna maisha feki sana watu wanataka kuishi maisha wasiyo na uwezo nayo, kuishi kitaoeli tapeli etc. Na kuondokana na vikundi vya ma classmates ndiyo kuondokana na maisha feki.

Na inawezekana mtu anayeamua abaki Tanzania wakati kirohoni haishi kusujudia kila kitu cha Marekani anaweza kuwa anaishi maisha feki sana.

Ufeki hauji kutokana na sehemu unayoishi. Unakuja kutokana na kuishi maisha ya uongo.
 
Back
Top Bottom