Maisha popote au warudi bongo?
Excuse me Sir, but you are contradicting yourself. Kama maisha popote usiwaambie warudi Bongo!
Msemo maarufu sana wa diaspora huo, "maisha popote," msemo wa kukata tamaa na wa uongo, masikini ya Mungu.
Sasa kama huyu Copenhagen yuko humu bila aibu anasema anaishi kwa kulipiwa renti na kanisa! Nani Tanzania analipiwa renti na kanisa zaidi ya Mzee wa Upako na Mama Rwakatare?
Namfahamu ni mchangiaji maarufu kwenye thread za immigration, anasema yuko Scandinavian countries lakini siku moja alianzisha mada hapa tukakuta hajui kuandika maneno Denmark wala Finland, yani yuko Scandinavia na darasa la saba la Afrika, he is definatelly gonna be shut out of even touching the bottom rung of the economic ladder. Mtu kama huyo atakueleza nini kuhusu maisha ya Ulaya zaidi ya kukushauri ukawe omba-omba wa makanisani?
Halafu anakuja mtu hapa anasema diaspora wakirudi wanataka kuishi standard za juu, nimemuuliza standard gani hizo ambazo walizoea Ulaya, kunywa Heineken? Kakimbia.
off course I am right, I know what I am talking about. Si wapo humu, kama naongopa watasema.
Na hilo la "kama huna shughuli ya kufanya ughaibuni..." hapo pia unawapotosha.
A more helpful question is "Ulaya na Marekani unafanya shughuli gani?" Sio shughuli mradi shughuli. Na kama ni odd job, "kazi za ajabu ajabu," mustakabali wako na hiyo kazi ni nini, utalea wazee mpaka lini, uta stock Wallmart aisles mpaka lini, utakaa kwenye kibanda cha security nje kwenye sub zero degrees mpaka lini? Au kama hujioni ukitoka humo, okay, unapata nini out of that job, umefanya miaka 5, 10, do you have anything to show for it? Au unapokea tu subsistence paycheck, umelala umeamka, maisha popote!
Vast majority of the diaspora wana exist on subsistence compensation, mdomo uende kinywani. Na hii sio wao tu "...approximately 62% of Americans have less than $1,000 in their savings accounts and 21% don't even have a savings account..." Nenda google andika "USA Savings..."
Hawa ndugu zetu msiwadanganye eti wakija bongo tatizo wanapenda kuishi standard za juu, standard za juu zipi?
Fikiria mtanzania ambae katoka Tanzania akiwa maskini. Ana paspoti ya Marekani popote atakapo duniani anaenda. Hasumbuliwi visa labda za Iraq na North Korea. Ni uamuzi tu kwenda Jamaica au Hawaii kwa wikiendi. Au aungane na marafiki wachukue livu ndani ya boti kubwa (cruise) wazurure visiwa vyote vya Caribbean wiki nzima au wiki mbili. Ni kula, kunywa, muziki, wanawake na kulala.
Mtanzania huyo ana miliki mjengo wa gorofa tatu. Anachagua alale chumba kipi. Hata kama ana mkopo wa nyumba lakini nyumba ina jina lake. Na ikipanda bei anaweza kuuza na kuchukua cha juu.
Mtanzania huyu ashindwe mwenyewe akitaka kusoma atasoma mpaka Phd kumi kwa mkopo wa serikali.
Familia yake ina uhakika wa kwenda shule, huduma za matibabu. Kula sio ishu. Mataifa yaliyoendelea hayajui bei za sembe na sukari kwa sababu vyakula ni vyingi na vya aina nyingi.
Umezungumzia savings. Wengi hawana savings kwa sababu hawana nidhamu ya kusevu. Wana ma credit card mpaka ya laki. Wengi wakiwa na shida ya pesa hawafikiri kumtapeli mtu wanachaji credit card.
Hizo kazi hovyo ulizozitaja ni za kuanzia kwa wanafunzi na ni kazi za pili za kuongeza kipato.
Sasa basi katika huu mjengo wa gorofa tatu. Mtanzania kaweka viflat screen mpaka jikoni. Akipika kaugali anamcheki mzee Majuto na Senga kwenye Youtube. Na anatumia internet ambayo haina cha bando la kuchacha. Ni high speed ya ukweli haina chenga wala nini.
Wakiitwa wenye magari huyu jamaa anakwenda na ushangingi mrefu kushinda Prado. What the hell? Kwanza hakuna Prado. Ni mwendo wa ma escalade, tahoe, yukon denali, lexus, benz, infinity, bmw nk. Ni magari yaliyojaa ma gps na bluetooth. Unaliambia gari piga cd, piga mwimbo wa tatu. piga youtube, piga simu mpigie nanihii. Wabunge wa Tanzania wanayo hiyo? Hata kina Manji hoi hapo. Wana viyoyozi tu.
Barabara ndio usiseme mpaka mlangoni. Unaweza kukaa mwaka hujaona mchanga. Ni lami, pavement, bustani na majani. Sio Bongo hata nyumbani kwa waziri nje kuna makorongo na mazalia ya mbu na vyura.
Mtanzania ana pension atalipwa mpaka siku anaingia kaburini. Na atalipwa hata akiwa Tanzania. Kuna Mkenya karitaya kila January anaenda Kenya mpaka mwezi wa nne anarudi Marekani. Anakimbia baridi. Wenzetu Kenya wana uraia wa nchi mbili basi mambo ni mswano zaidi.
Na hayo yote unayapata kwa mshahara halali wa kawaida tu au kwa kuunga kazi mbili au kushirikiana na mkeo. Huhitaji kuwa mbunge, hakimu, daktari wala loya.
Kwa mwendo huo unarudi nyumbani Mungu akupe nini. Mbu wa maleria kali?
Ni hivi maisha ni kupanga. Mungu katupa akili tuzitumie. Kama umeenda nje na malengo yako ya elimu au pesa. Ukikamilisha rudi nyumbani. Ila kama umeenda nje kuishi. Jichanganye na mfumo wao wa maisha. Sio urudi nyumbani eti maisha magumu. Yakikushinda nje hasa Marekani na Tanzania yatakushinda. Wewe ni mshindwaji. Kama unakumbuka yalikushinda Tanzania kabla hujakimbilia nje.
Hao diaspora wanaoshindwa maisha hasa Marekani ni wale wasiojua wameenda kufanya nini. Mtu anakaa nyumba ya kupanga miaka 30. Akiulizwa niko kwa muda hapa. Lakini anazeekea nje. Hawajui kujiunga na mfumo wa Marekani.
BWEGE YOYOTE KUTOKA TANZANIA AKIINGIA MAREKANI ANAWEZA KUISHI HAYO MAISHA NILIYOYAELEZA HAPO NDANI YA MIAKA MITANO TU!