Hawataki sema tu mkuu, kule ni balaa, watadai kwetu kwa wadanganyika bure kabisa, ila wakumbuke huku huku ndipo kuliwapa akili ya kwenda kule, wakifika kule wanajifanya wazawa, tatizo hata wafanye nini hawawezi kukubalika, hawajakaa vizuri miaka imeenda, nyumbani alikuwa anapaponda, hajawekeza chochote, ataanza vipi kurudi?! Zaidi ya kupaponda na kusema harudi ng'oo!
Kuanzia kwa Trump, EU mpaka Asia, mwafrika anaipata fresh, kuanzia kuitwa nyani, kuangaliwa kwa jicho la wasiwasi na lakinyaa mpaka kunyimwa ajira, kisa ngozi nyeusi, maisha gani hayo?!
Ila wanasahau nyumbani nyumbani, hawakufukuzwa, TZ itawapokea vizuri kama ilivyowaaga.