Diaspora wengi wa Tanzania hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kuturingishia picha

Hakuna watu wanatoa maneno ya kimzaha na kejel kama shirika la umeme kuhusu kukatika katika ovyo kwa umeme .

Mtoa mada mpka sasa sijaelewa tatzo lake ni nin 🤔

Mara ukame. Mara maji mengi. Mara mitambo mibovu ni danadana mwanzo mwisho.
 
Hakuna tatizo kabisa hapo. By the way, kwani kuchunga wazee Sio kazi halali!?
ni kazi kama kazi zingine tu, watite ukawasafishe, watapike uwasafishe fresh tu, si sawa tu na manesi na madoctor wanachofanya. ndio kazi zenu hizo.
 
Yote Heri kuliko kuozea kwenye hii nchi inayoendelewa kuharibiwa na ccm.
hii nchi utaiona mbaya kama hujatoboa, ila ukitoboa hapa kuna maisha bora kuliko ulaya na america. ukiona unajutajuta jua haujatoboa na kama hautatoboa hapa hata ukienda ulaya utapata shida sana na ukifanya mchezo utaolewa. kwasababu hapa ukiwa na pesa kuna fursa nyingi na wajinga wengi wa kuwatumikisha ili uendelee kukaa kileleni, kuna uwanda mkubwa sana pia kukwepa kodi (pamoja na kwamba sishabikii hilo), ulaya ukienda jua utatakiwa kulipa kodi, na kila mtu hata yule uliyemwajiri ana sauti na humfanyi lolote, maisha yapo juu sana, ndio maana kama hauna kisomo kizuri cha kupata kazi ya kuajiriwa yenye mshahara mzuri, utapata shida sana wala msidanganyike kwenda huko. utaishia kuwa mfagizi, mzibua mitaro, osha makalio ya vibibi na vibabu, dereva, kibarua kwenye ujenzi n.k kazi ambazo bado unaishi kama mtumwa tu na kila unapogeukia ni kodi ambayo huwezi kukwepa.
 
ni kazi kama kazi zingine tu, watite ukawasafishe, watapike uwasafishe fresh tu, si sawa tu na manesi na madoctor wanachofanya. ndio kazi zenu hizo.
Of course ndio kazi zetu hizi, ulitaka wote tufanane, au!?
 
Wewe uliyetoboa sidhani kama ni kazi Yako kuwashauri waliotoboa. Just Live your life, na usiwe mshauri saana hata kama hujaombwa ushauri .
 
Yaani hata mange kimambi hafanyi la maana....hebu acha wivu basi
 

😂😂😂

Kuna Watu machizi kweli humu.

Lakini akihoji uwepo wa Mungu si anahoja?

Ila kwenye huu mjadala naona Diaspora wameshindwa kujitetea kwa hoja zaidi naona Mihemko imetawala.

Walipaswa wajibu hoja za mtoa mada kwa hoja aidha kwa kukubali kuwa huko mambo bado magumu na ndio maana wanashindwa kung'ara kama wenzao. Au wanaweza kusema wanang'ata kwenye sekta fulani zisizo na wafuatiliaji wengi na kutoa mifano ya Diaspora wanaong'ara.

Simple tuu
 

Angalau huu utetezi unahoja kidogo
 
Wewe uliyetoboa sidhani kama ni kazi Yako kuwashauri waliotoboa. Just Live your life, na usiwe mshauri saana hata kama hujaombwa ushauri .
pole. pambana kuna siku utatoka tu ndugu.
 
Hatuwezi kusubiri kumtathmini 3rd and 4th generation migrant. Huyo hatakuwa Mtanzania tena! Na wala hataulizwa umeifanyia nini nchi yako ya zamani.

Mnaulizwa nyinyi! First generation immigrants mliotoka huku, mkakimbia shida, mna meaningful impact gani kwa TZ nyinyi watu ?????

Mama yake Donald Trump hakuzaliwa US, wala baba ya baba yake hakuzaliwa US, hivyo Trump ni second generation citizen. Watakaokuwa 3rd and 4th ni wajukuu wa Trump. Sasa wajukuu wa Trump wataulizwa umeifanyia nini nchi waliotoka babu zako wakati Trump mwenyewe (second generation) haulizwi kuhusu nchi ya mama yake ???? Wanaulizwa first generation tu, mnaulizwa nyinyi! First generation migrants.

Sasa msitoke mapovu. Na sikutegemea diaspora mwenye exposure, umekaa nje miaka kibao, unajibu hoja ya mchango wenu na mafanikio yenu, hoja inayoandikiwa mpaka thesis za PhD kwa kusema "wewe mchawi, unawashwa na pilipili ya shamba, tulipoondoka hatukukuaga, mnakula nyanya chungu Nanjilinji, una kijiba cha roho." Ningedhani mmeshasahau mambo ya uchawi na vijiba vya roho! hahahahahaaaaaa!
 
😂😂😂wabongo nuksi sana
 
Ngoja nikwambie wewe, 1st generation hawezi kuingia ughaibuni kuipambania nchi badala ya kujipambania yeye kwanza na familia yake. li nchi lenyewe limejaa wala rushwa kuanzia viongozi huko juu hadi chini watoa huduma, halafu mie nimeingia kwa mnyamwezi kwa kupambana mwenyewe nianze kuwaza kulipambania li nchi la wala rushwa NEVER. Pambaneni na hali zenu banaa diaspora nao waacheni na life yao, kingine wengine hatukuondoka bongo ili baadae turudi, tuliondoka kwenda mamtoni kuishi na kutengeneza familia zetu, kuja huko ni holidays tu! Hakuna cha kuwasaidia zaidi ya kuwaachia ndugu mijengo waishi kwa nafasi bila kulipa kodi. Yaambieni Ma CCM yawetengenezee nchi kwanza; jana tumeona mlivyokua mnaogelea kama samaki huko jangwani na ununio sijui mnakosema wanaishi washua, sio kujifanya kuwapelekea lawama diaspora fyuuu.
 
Mfano diaspora wa nigeria wanavyofanya mambo yenye impact ya kuitangaza nchi yao sio lazima uisaidie hapana

Lakini wengi wao maisha yao binafsi yanawashinda wanabangaiza huko ughaibuni sasa wataidaidie nchi
 
DIASPORA wa Tanzania wamefungwa mikono kwenye mambo mengi sana. Nigeria, Kenya na Ghana kwa mfano, mtu hata akichukua uraia wa nje, bado wanamtambua, bado ni raia wao kama akitaka, anaweza kumiliki ardhi na kufanya kila kitu kama raia wao. kwa Tanzania, pamoja na kwamba hao vijana wetu wameenda huko kwa ajili ya kutafuta maisha tu, akipata uraia mwingine ili ndoto zake huko zitimie/awe na haki huko ili apate alichofuata, sisi huku tunamdisqualify kama raia, amefungwa mikono kuja Tanzania, atakuja kwa visa, hamiliki ardhi ama la kama mwekezaji, wakati mtu kaacha mama yake baba yake na ndugu kibao huku. ni sisi wenyewe tunajifanya hii dunia ni milki yetu kumbe wapo walioikuta na wameiacha. mtu atakuwaje mzalendo kwenye nchi inayomkana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…