JULIUS NYERERE, hakufa kifo cha kawaida.Aliuawa kwa sumu iliyopandikizwa ndani ya mwili wake.Siri hiyo anaijua Daktari wake na baadhi ya maofisa na wasaidizi wake.Alilazimishwa kwenda "kuangaliwa" afya yake na mara baada ya kutoka katika hospitali kwa "checking" hiyo na kuwasili alipofikia Guest wing London alianza kujisikia vibaya na hatimaye alianguka ghafla na kudakwa na mlinzi wake aitwaye Mkanzabi.Ndipo yalipofanyika mawasiliano ya haraka ili kumuwahisha hospitali.cha ajabu wakati anaondoka Tanzania, Mkapa alikuwa akijiandaa kwenda katika mkutano mmoja huko ulaya.alipozidiwa Mwalimu,Mkapa alipitia london kutokea Zurich,lakini kwa mujibu wa madai yake huyu bwana alidai hakuweza kumwona kwa karibu,ila alimwona kwa mbaaali.Hii inadhihirisha wazi kwamba alienda kumsanifu mzee huyo wa miaka 77 akiwa kitandani hoi.Aliporudi Tanzania alikutana na waandishi wa habari na kudai ikulu itakuwa ikitoa taarifa za maendeleo ya Mwalimu huku akisema kwa maneno ya mafumbo kuwa "Mwalimu is recovering slowly"(Dying slowly!).Wakaona mtu wa kumtuma kudhibiti yanayoendelea London ni Kingunge Ngombale Mwiru.Mzee huyu alipewa cheo kuwa mshauri wa Mkapa kuhusu siasa na mbunge wa kuteuliwa.
Mwalimu alifariki dunia na kuzikwa kwao butiama.
Mwaka mmoja baadaye (2000),mkapa alienda Butiama kuhani katika kaburi la Mwalimu.Yaliyotokea pale ni mauza uza ya ajabu ikiwa ni pamoja na kuvunjika kimaajabu kwa msalaba katika kaburi la Mwalimu!!.Yaliandikwa katika magazeti,lakini yalifichwa na kufunikwa.Toka Musoma,Mkapa alienda Mwanza na pale mnakumbuka palitokea ajali mbaya ya basi lililoacha njia na likawa linafuata gari alilopanda Mkapa.Walikufa watu wengi!
Miezi kadhaa baadaye Mkapa alianza kuugua maradhi yaliyomfanya akae nje ya Tanzania kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kurudi akitembelea magongo!!
Ikumbukwe kwamba baada tu ya Nkapa kwenda ulaya kwa matibabu ,nyumba ya Rais ikulu iliungua.Majanga haya ni matokeo ya aliyoyasimamia Nkapa juu ya kifo cha Mwalimu.
Yapo mengi wanayojua watanzania ila kwa hili tuishie hapa kwanza.