Did you marry the right person? If asked to remarry, would you still choose the same person?

Did you marry the right person? If asked to remarry, would you still choose the same person?

There's no fomular in these matters of r/ships or marriages.
No one is perfect,even if you'll marry a 100 times you'll still not hit your target.
 
Mke wangu siwezi badilishana nae labda nitabadili tu style ya kumtongoza ili niwe nae. Kwenye maisha kwa ninavyoamini mimi ni kama unavyochonga kinyago ww ndio unataka kiweje ili jamii ikione na ipate funzo au ipate ule muonekano unaotaka wewe. Nimeshamtengeneza mke wangu kiasi kwamba navutiwa nae kila siku kutamani kuwa na mwingine zaidi yake ni ngumu bado hajanipa sababu za kuwa na tamaa japo napiga nje ila ni kishkaji tu nahisi nimemtengeneza awe sahihi kwangu na mimi niwe sahihi kwake alafu ni mama bora kwanini nipoteze 50 nilionayo mkononi kisa 100 ninayoahidiwa na sijui itakua 100 kweli au uongo.


Tengenezeni maisha yenu ili kuepuka kujiuliza maishani
 
Mke wangu sijui kama ni mtu sahihi au la ila tunashare vitu vingi sana,chemistry yetu ipo high sana.

Hata nikipata mcheouko,utakuta mchepuko yupo poa sehem moja tu,lakini sehemu nyingi anaachwa.kuna muda wife ananikera sana lakini mwisho wa siku yeye ndio mtu pekee huwa ananijulia na kunipa furaha ya juu sana.

Wife tunachambua nae hip hop vizuri kabisa,anamkubali dizasta,conboi,p mawenge, na nash mc,mimi ndio nipo addicted na hip hop kabisa. Sasa hiki kitu kinamfanya credit iwe juu sana kwangu hasa akiwa ananichania ngoma ya kanisa by dizasta

Ana gud positive interaction anapokutana na watu wangu,anawapenda ndugu zangu,she cares for me and love me so much,

Kero yake ipo kwenye kudeal na simu yangu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom