TANZIA Dida Shaibu, mtangazaji wa Wasafi FM afariki Dunia

TANZIA Dida Shaibu, mtangazaji wa Wasafi FM afariki Dunia

Siyo sawa kuandika vitu kama hivi, mtu anapokufa anakuwa amefunga kitabu chake cha hapa duniani mengine tumuachie mungu, siyo sawa kumsema mtu ambaye hawezi kujitetea, na unajisikiaje kusema mambo kama haya kwa marehemu, hivi angekuwa dada yako unheandika vitu kama hivi? Hii mitandao isotutoe utu wetu ,hata sisi tutakufa
 
Kwanza uelewa Millard Ayo na Wasafi ni redio shindani kwahiyo sio suala la kusikia na kuandika, ataandika baada ya kupata details hata kama tyr ana uhakika! Apumzike kwa amani Dida
 
Siyo sawa kuandika vitu kama hivi, mtu anapokufa anakuwa amefunga kitabu chake cha hapa duniani mengine tumuachie mungu, siyo sawa kumsema mtu ambaye hawezi kujitetea, na unajisikiaje kusema mambo kama haya kwa marehemu, hivi angekuwa dada yako unheandika vitu kama hivi? Hii mitandao isotutoe utu wetu ,hata sisi tutakufa
Woteeee tutakufaaa, na Didaa ameniumaa mnoo.
Msibanii nitaendaaa, [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Kupitia Dida magazeti ya udaku nakumbuka yaliuza sana hasa magazeti ya kiu, ijumaa wikienda na ijumaa.

Ni msiba mkubwa.
Kwaheri Dida
 
Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha WasafiFM Khadija Shaibu maarufu kama Didah, amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa.

Didah ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 42, kifo chake kimetokea siku kumi na sita (16) toka Wafuasi wake washuhudie ukimya wake katika mitandao ya kijamii ambapo chapisho lake la mwisho mtandaoni lilikuwa September 19 2024 ambapo aliweka picha yake akiwa kwenye gari ikisindikizwa na wimbo wa Martha Mwaipaja “amenitengeneza’.

#AyoTV na millardayo.com tunatoa pole kwa wenzetu wa #WasafiMEDIA , Wafanyakazi wenzake, Ndugu, Jamaa na Marafiki na wengine wote walioguswa na msiba huu, Mungu amlaze pema Ndugu yetu Didah. 🙏🏿
 
Attachments

  • FB_IMG_1728069302139.jpg
    FB_IMG_1728069302139.jpg
    44.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom