Die Glockie: Je, ni kweli chombo hiki chenye nguvu ya ajabu, Hitler alikitumia kuunda silaha za ajabu na kufanya time traveling?

Die Glockie: Je, ni kweli chombo hiki chenye nguvu ya ajabu, Hitler alikitumia kuunda silaha za ajabu na kufanya time traveling?

Hizi ni Ngano kama Ngano nyingine tu. Sema kwa wengine huwa mnazibeba kama zilivyo bila kuchanganya na zenu. Msiwe na akili kama za mbayuwayu. Akili za kuambiwa unachanganya na zako. HAKUNA TIME TRAVELLING. haikuwahi kuwepo na haitakuwepo. Ukiangalia movies wewe unaamini kila kitu. Ukisimuliwa nawe unakuja tafuta wa kuwasimulia. Huchanganyi na akili zako. Hakuna hilo Kengele ya maajabu... NARUDIA. HIZO NI NGANO TU NA VIGANO katika field mbalimbali. Katika sayansi kuna masimulizi yake, katika imani nako utakuta habari za dragons n.k
Wasaalam

Naam,

Miaka fulani hadithi kuhusu ndege zenye umbo la sahani Almaarufu kama UFO (unidentified Flying Object ) zilishamili sana kuliko hata neno lenyewe, na usichokijua ni kwamba hata jina lenyewe lilipatikana kwasababu ya kutokufahamu vyombo hivi vilikuwa vinatoka wapi! Na viko chini ya milki ya nani!

Huku vikihusishwa zaidi na viumbe kutoka anga za mbali kama Alliens na vinginenevyo., Aghalabu visasili kuhusu alliens tunavifahamu sana tushashuhudia vidio na kusimuliwa zaidi hata ya Mara nyingi.

Hapa kwenye alliens kuna Makundi mawili ya watu duniani waaminio kama kweli wapo na ambao tunoamini hizi ni propaganda za USA., na washirika wake.

Si hilo tu zikazuka hadithi za kusafiri kwa wakati (Time travelin) kwenda Future na Past , lakini hata hizi zilihubiriwa sana na wanasayansi nguli na Hata movie zikatufikishia Ujumbe kwa namna moja au nyingine nyingi.

Lakini mpaka sasa dunia na wakazi wake tumebaki kwenye kitendawili kinachoitwa "HOW" au "WHY" hili ni FUMBO.

I honestly think there's more to this world than what we see,.with our own Eyes and I believe they do.

View attachment 2165932
Nikurudishe karibu karne moja iliyopita ambapo Hitler, NAZI na Ujerumani kwa Ujumla walipoitetemesha dunia??

Ulishawahi kujiuliza jeuri ya Hitler, na ndoto za kuisambaratisha dunia na kuiteka kabisa wakati ule alizitoa wapi?? Mpaka katika point ya mwisho kabisa ambayo hitler anapoteza?

Je, ushawahi kufikiria wanasayansi wa NAZI walivyokuwa na hamu ya kutengeneza silaha ambayo ingeweza kuyapoteza na kuyarudisha nyuma majeshi ya Maadui zao yaliyokuwa yakisonga kuja kufanya Uvamizi dhidi yao?

Je, ni kweli hizi fununu zinazotwambia waliunda UFO yao ya ili kushinda Vita vya Pili vya Dunia?? Ndivyo au sivyo.

View attachment 2165934

Walakini, ushawahi kuskia habari za "Die Glocke" (Kengele) hii ilitengengezwa katika mfumo wa kengele na ndiyo maana ikapata jina hilo lakini hii inaelezwa ilitumika zaidi kama zilivyo UFO.

Kuna Video kutoka kwa mwanahistoria wa kijeshi Mark Felton, inayozungumzia kifaa chenye umbo la kengele ambacho shirika la kijeshi la Adolf Hitler la Schutzstaffel (SS) lilidaiwa kutengeneza kwa ustadi wa hali ya juu ambacho kilihusika na kazi nyingi sana.
Hata hivyo kundi lingine lilipinga na kusema waandishi wanaweza kuwa walitengeneza stori juu mashine hiyo, wakieneza sifa zake baada ya vita na kulipamba jopo la wanasayansi wa NAZI.

Lakini hili halituzuii sisi kukubali kwamba wanasayansi wa NAZI walikuwa na uwezo wa hali ya juu sana katika kipindi kile cha vita.
Ingawa WaNAZI walipoteza katika Vita vya Pili vya Dunia, lakini ziliibuka hadithi nyingi sana baada ya vita ,wakiwa na sifa ya kuwa na karibu kila silaha zenye teknolojia ya hali ya juu.

Mizinga ya Nazi mara nyingi ilikuwa bora kitaalam kuliko mizinga ya Maadui zao., Wao walirusha ndege za kivita katika mapigano kabla ya Maadui kufanya hivyo,pia makombora tofauti tofauti ambayo yalikuwa na uwezo wa hali ya juu kuliko kawaida, ingawa habari hizi zina shaka kimkakati.

View attachment 2165946

Maadui walichukulia mafanikio ya wanasayansi na wahandisi wa NAZI, kuwa ya hali ya juu sana, Hata Jeshi la Marekani lilituma timu za upelelezi nchini Ujerumani katika hatua za baadaye za vita ili kuchota kundi la wanasayansi na baadhi ya mbinu za teknolojia za kijeshi kabla ya kutumia nguvu na juhudi zingine.

Juhudi hizo, zilifanikwa kuchota baadhi ya teknolojia kama zakutengeneza makombora na pia kuchota watu wa muhimu kama Wernher von Braun, mhandisi maarufu wa anga ambaye alivumbua V-2 na baadaye akaunda roketi ya Saturn V ambayo ilikuja kutumika katika programu ya NASA ya Apollo.

Turudi kwenye Die Glockie
Kuhusu hii habari Die Glocke iliripotiwa kuwa moja ya Wajerumani kile walichokiita “wunderwaffe” (wonder weapon).

Habari za kifaa hicho zilionekana kwa mara ya kwanza katika kitabu cha 1960 , cha Morning of the Magicians. Die Glocke pia ilielezewa katika kitabu cha Igor Witkowski cha 2000 "Prawda o Wunderwaffe" (Ukweli Kuhusu Silaha ya Ajabu)

Na muda mfupi baadaye, kitabu cha Nick Cook cha The Hunt for Zero Point kikachimba kuhusu silaha hii, huyu ndiye alifunguka zaidi kuhusu zahma za silaha hiyo anasema hii pia ilikuwa machine inayowasafirisha kwenda sehemu mbalimbali au pia hata ilikuwa mashine ya kusafiri kwa wakati kwenda katika nyakati tofauti na kujifunza teknolojia ambayo ilikuwa sehemu ya mpango wa NAZI wa kudhibiti maadui na kuiteka dunia.

ILIWEZEKANAJE?
Hapa nami nikuunganisha doti , inawezekanaje Hitler apate jeuri na kujiamini kuidhibiti dunia hadi pale kibao kilipogeuka huenda basi silaha na teknolojia hizo na hii Die Glockie zilikuwa chachu ya Ujeuri wake.

View attachment 2165937
Bwana Cook hata aliezea uwezekano kwamba kanali maarufu wa NAZI Hans Kammler aliiuza Die Glocke kwa jeshi la U.S ili kubadilishana na uhuru wake. (Kammler alitoweka katika siku za mwisho za Vita dunia vya pili na hakuonekana tena.) inaelezwa Kammler baada ya kuwa chini ya jeshi la Adui , akatoboa siri kuhusu Die Glockie na maadui wakafanikiwa kuichukua huku kammler akipatiwa uhuru wa maisha yake , lakini hakuwahi kuonekana tena mpaka keshokutwa.

View attachment 2165938

HANS KAMMLER

Die glockie inadaiwa... (hakuna uthibitisho juu ya hilo)

-Ilitumika kuwapoteza maboya wanajeshi wa upinzani kutofikia point ambayo walitaka mfano kuvamia kambi mbalimbali za kijerumani

-ilitumika kwenda sayari za mbali kwa kuwa kifaa hiki kilikuwa ni Antgravity inadaiwa kiliweza kukatiza hadi orbit ya Dunia katika zama ambazo mandeleo haya ya sayansi na Teknolojia.
How spiritualy au?

-Ilitumika kusafiri kwa wakati , inaelezwa wanasayansi walitumia Die Glockie kama chombo cha kwenda nyakati tofauti tofauti kuchukua maarifa ya kutengeneza silaha ili kushinda vita.

-Ilisaidia kuwapa uwezo na nguvu za ziada.

Baada ya maadaui wa NAZI kufanikiwa kuwachota baadhi ya watu wataalamu wa NAZI na kufanikiwa kuwashinda Wakati Maadui hawa wa Ujerumani walipokuwa wanarudisha nyumbani silaha zenye teknolojia ya hali ya juu za Kijerumani wakati wa Project Paperclip, ambapo Von Braun aliwachoma wenzie, ikijumuisha ndege, mizinga na makombora, hakuna taarifa ya toleo lolote kuhusu Die Glocke iliyowahi kutoka na haieleweki kifaa hiki kilipelekwa wapi.

View attachment 2165940

Bado, baadhi ya Wanasayansi na wananadharia wa habari na fununu za UFO wanaamini kwamba vikosi vya Marekani viliwakamata wanasayansi wa NAZI, na hata Kammler mwenyewe na kuwaweka katika vitengo mbalimbali vya kuendeleza teknolojia ya Die Glocke ya kusafiri kwenda mbali na nyakati tofauti.

Kama hadithi hizi zinavyoendelea, hii iliishia katika kile kinachoitwa Tukio la Kecksburg, wakati UFO yenye umbo la kengele iliripotiwa kuanguka nje ya Kecksburg, Pennsylvania mnamo Desemba 1965.

View attachment 2165942

JE, UNAFIKIRIA nini?
Marekani anaposema hajavumbua njia yoyote ya kusafiri kwa wakati, lakini mwishowe anatuletea habari Kedekede kuhusu watu mbalimbali waliosafiri kwa wakati na picha zao za maeneo waliyofika,?

Chombo hiki bado ni Fumbo lakini vipi je ikiwa kiliendelea kuboreshwa na kuleta matokeo ambayo wao waliyataka .???

DaVINCI XV
 
Kweli hili ni jukwaa la watu wenye intelijensia ya hali ya juu
Heeeh.... Basi wewe utakuwa ni very abnormal. Kila kilichopo humu ni normal hakuna watu walichovumbua. Wana copy na kuja paste humu. Au wana translate na kuleta humu. Sasa hiyo intellejencia yao ipo wapi? Yaani unakuwa amazed na vitu vidogo sana mpaka you abuse the word intelligence
 
Heeeh.... Basi wewe utakuwa ni very abnormal. Kila kilichopo humu ni normal hakuna watu walichovumbua. Wana copy na kuja paste humu. Au wana translate na kuleta humu. Sasa hiyo intellejencia yao ipo wapi? Yaani unakuwa amazed na vitu vidogo sana mpaka you abuse the word intelligence
Vya kwako vikubwa ulivyogundua hapa duniani ni kipi? Peleka uchoko wako huko
 
Mbona unakuja na kinyume nyume huku unatokwa povu? Hizi IDs zote huwa zinakusaidia nini? Unatoka povu sehemu zako za mwili za wazi zote.....
Vya kwako vikubwa ulivyogundua hapa duniani ni kipi? Peleka uchoko wako huko
 
Wageni wanaweza kuja kwa ajili yakuchungulia na si kuishi!

Wao watakuona, wewe hautawaona.
Mfano mtu aliye time travel miaka 5000 iliyopita na leo ndiyo kawasili, utamuonaje?

Au leo mtu a'time travel miaka 1000 mbele unadhani kinadharia atakaowakuta huko wataweza kumuona?

Time ttaveller ndiye muonaji wa wengine katika safari zake, lakini wengine hawawezi kumuona.
 
Time Travel ni Nini? Na ni kwa namna gani tutasema kwamba time travel imetokea. Na unapo fanya time travel unaifanya kuelekea wapi? Mwisho wa siku mechanism of time travel ni impossible.
 
Wageni wanaweza kuja kwa ajili yakuchungulia na si kuishi!

Wao watakuona, wewe hautawaona.
Mfano mtu aliye time travel miaka 5000 iliyopita na leo ndiyo kawasili, utamuonaje?

Au leo mtu a'time travel miaka 1000 mbele unadhani kinadharia atakaowakuta huko wataweza kumuona?

Time ttaveller ndiye muonaji wa wengine katika safari zake, lakini wengine hawawezi kumuona.
Hapa unanikumbusha Yule jamaa aliyenaswa AirPort za Japana
Akasema anatokea nchi ya Taured, na akapewa Raman kuonyesha Nchi yake Ilipo

Hapa ni kwamba polisi na Hata yeye mwenyewe waliweza kuongea ,na Claims zikawa huenda jamaa kutoka nchi ya Taured ni Traveller kwa maana Hata Nchi ,mahali alipoonyesha hiyo Nchi haikuwepo
 
Time Travel ni Nini? Na ni kwa namna gani tutasema kwamba time travel imetokea. Na unapo fanya time travel unaifanya kuelekea wapi? Mwisho wa siku mechanism of time travel ni impossible.
Uzuri wa Sayansi imejipambanua na Iko dhahiri,.
Hata stephen Hawkin alipoitisha party,kwa ajili ya Matravellers Kutoka nyakati zote (future & Past) kuja pale lakini hakuna hata Mmoja Aliefika
Kikawaida mechanism zote za kufanya Time Travellin .,hazijapata Proof

Nakumbuka siku mboja Proffesa wangu wa Fizikia aliniuliza, ikiwa Physically kutoka nyakati moja kwenda nyingine haiwezekani je ushawaza kuhusu kufanya hivyo Spiritually.
 
Hapa unanikumbusha Yule jamaa aliyenaswa AirPort za Japana
Akasema anatokea nchi ya Taured, na akapewa Raman kuonyesha Nchi yake Ilipo

Hapa ni kwamba polisi na Hata yeye mwenyewe waliweza kuongea ,na Claims zikawa huenda jamaa kutoka nchi ya Taured ni Traveller kwa maana Hata Nchi ,mahali alipoonyesha hiyo Nchi haikuwepo
Embu elezea kwa upana hiki kisa
 
Kuhusu haya mambo vitu vinasemwa vingi sana ukweli unabaki kuwa fumbo isipokuwa kwa wachache wenye dhamana ya kufahamu ndio hufahamu!.
Kwanza katika maisha ya mwanadamu kuna tabaka za watu kuna elites na wakati na wachini kabisa sasa hawa wa juu hufanya vyovyote ili wawatawale wengine!. Kuna mambo ya hadaa na yasiyo hadaa!.
Taarifa zozote unazozipata kuhusu mambo ya uongozi nadharia n.k itabidi Kwanza uhangaike ujue hii ni hadaa ama sio hadaa!.

Kuhusu UFO,najua kuhusu hizi habari kitambo hata mimi nilishawahi shuhudia UFO nishasimulia humu mpaka leo sijaweza tambua kitu kile ni nini! Nachokumbuka kilitoa mwanga wa kijani na mahali hapo palimulikwa mwanga wa kijani yani pakawa kama mchana ila kwa mwanga wa kijani!.. then kitu hicho kikatokomea angani huko, Ilishangaza na kuogopesha!.
Wanasayansi wa mashirika makubwa walionekana kukataa kuhusu hizi vitu ila sahivi wameanza kukubali kuwa UFO zipo!,kuhusu zinatokea wapi ndio hawasemi ni aidha binadamu au viumbe wengine. Yote haya yanawezakuwa majibu sahihi!.

Kuhusu Hitler na tekinolojia za anga ni ukweli usiopingika kuwa bwana huyu alijidhatiti vizuri kijeshi,hata picha mbalimbali zimekuwa zikionyesha vyombo hivyo vya anga zenye muundo kama sahani toka zamani na zaidi ktk nyakati za utawala wake!..
Chombo ulichokizungumzia kinawezakuwa kweli kilikuwepo ila taarifa zisiwe sahihi! I mean wanaweza kuongeza madikodiko ili kutupoteza maboya! Hizi ndo hadaa!.
Pia inawezekana taarifa zikawa sahihi ila zikawa zimevuja kama ulivyoelezea katika hivyo vyanzo vya hivyo vitabu ambavyo waliandika hao waandishi!.

Kwanini niseme hadaa..?
Napata walakini chombo hicho kikihusishwa na time traveling na hapohapo nikiangalia matokeo ambayo Hitler aliyapata!.. Kama chombo hicho kilikuwa kweli kinaweza ku time travel kwanini walishindwa kupata tekinolojia ya nuclear..?
Katika historia inaonyesha marekani ndo alianza kuitumia nuclear pale Hiroshima na nagasaki na moja ya wanasayansi nguli Albert Einstein formula yake ndio iliyotumika kutengeneza bomu la nuclear na alikuwa mwenye asili ya German na Jew!!!.

Sidhani kama Hitler angekuwa na uwezo wa nuclear angesita kuitumia kwa pale alipokuwa amefikia!,kivyovyote hakuamini ktk kushindwa!.
Kwenye hili nafikiri yapo mambo ya kweli na mengine ni hadaa!.

Time traveling hii nadharia ni kweli ipo maana laws of nature zinakubali mazingira haya,Sasa hizi movie nyingi tunazoangalia ni tofauti na inavyoelezwa kiuhalisia!. Mtu unatoka huko umejazwa fiction tofauti na vile uhalisia ulivyo! Kwanza ni kitu kinachohitaji nguvu sana maana kwanza ili uweze kufanya time traveling kwa njia ya speed itakubidi usafiri walau hata nusu spidi ya mwanga au spidi ya mwanga kabisa kitu hichi ukweli bado hatuna tekinolojia hii!!.. kwanza sidhani Kama
Mwili wa mwanadamu unaweza kuhimili spidi hii kama spidi tu za kwenye maroketi tu ya kwenda huko juu mpaka wavae pressure suit,vipi spidi ya mwanga..?

Kuhusu wormholes still ni nadharia sijui bado zipo ila inabainika kuwa gravity can slow time!,nakubaliana na hili so hata black holes zenye massive gravity sina pingamizi na hili!,ila hicho kifaa cha Hitler ku time travel nafikiri kitahitaji spidi ya mwanga!.. hapo ndo tujiulize je,kwa wakati huo waliweza hili ama tunapigana kamba..?
Na Kama waliweza waliweza kwa njia gani ku time travel au kuna kauchawi..😂 something which I don't believe!.

Maono yangu yawezakuwa kifaa au vifaa hivyo vipo kweli isipokuwa vinaongezewa chumvi tofauti na uhalisia,we angalia hata ndege kadhaa za Vita huwa zikitolewa huwa zinapigiwa chapuo sana sifa kedekede ila zikiingizwa vitani zinakutana na mashambulizi zinadunguliwa!,ndio ni hatari lakini sifa huwa zinazidishwa!.
Tazama hizi Mkuu





 
Hivi mna uhakika Wazungu ni binadamu wenzetu wa kawaida? I dont think so, imagine haya mavitu hawa jamaa waliyatengeneza miaka hiyo wakati sisi kipindi hiki bado tunafikiria habari za mashimo ya vyo vya shule, aise!
Vitu vigani walitengeneza wakati wamevipata hapo. Part kubwa ya Historia shuleni ni kwenye runinga ni uongo mtupu.
Ramani za 1500-1750 zinaonyesha Africa imejaa miji mikubwa Tena bila jangwa la Kalahari, Namib na Sahara. Jangwa Kwa kawaida huletwa na nukes/nyuklia bombs na other high energy weapons.
Je uko na picha za kuundwa Kwa Reli ya Tanzania Zambia na Mabeberu?
 
Vitu vigani walitengeneza wakati wamevipata hapo. Part kubwa ya Historia shuleni ni kwenye runinga ni uongo mtupu.
Ramani za 1500-1750 zinaonyesha Africa imejaa miji mikubwa Tena bila jangwa la Kalahari, Namib na Sahara. Jangwa Kwa kawaida huletwa na nukes/nyuklia bombs na other high energy weapons.
Je uko na picha za kuundwa Kwa Reli ya Tanzania Zambia na Mabeberu?
images (1).jpeg
images (1).jpeg
images.jpeg
 
Vitu vigani walitengeneza wakati wamevipata hapo. Part kubwa ya Historia shuleni ni kwenye runinga ni uongo mtupu.
Ramani za 1500-1750 zinaonyesha Africa imejaa miji mikubwa Tena bila jangwa la Kalahari, Namib na Sahara. Jangwa Kwa kawaida huletwa na nukes/nyuklia bombs na other high energy weapons.
Je uko na picha za kuundwa Kwa Reli ya Tanzania Zambia na Mabeberu?
Ubishi mwingine wala huaga hauna maana yeyote; chombo tunacho tumia kuwasilia hapa kimetengenezwa na wao, chupi uliovaa imetengenezwa na wao, miwani (kama una vaa miwani ) imetengenezwa na wao, ugonjwa wa malaria, typhod nk kule kwao hakuna, yapo huku kwetu lakini dawa wanatengeneza wao. Unaanza kuleta story za kabla ya ukoloni ukijua hata wewe huna uwezo wa kuzithibitisha kama kweli au uongo. Anyway, kwani kabla ya ukoloni kuja, hawa jamaa waliwezaje kututawala? Walitumia bunduki na mabomu wakati sisi tulitumia mikuki, huoni hadi hapo wao walikua mbele ya muda mbali zaidi kuliko sisi!? Enzi za Yesu (kama unaamini katika Biblia) walikua wanalima mashamba yao kwa kutumia ng'ombe, wakati sisi hadi sasa hivi tunatumia jembe la mkono, umeufikiria huo muda wa enzi za Yesu todate ni miaka mingapi imepita mkuu? Haya, bado unapinga kwamba sisi bado tunajadiri kuhusu mashimo ya vyoo mashuleni? Hapo ulipo, una nini ambacho kimetengezwa na sisi? Shati, soksi, chupi/boksa, simu etc vyote vimetoka kwao; but you know what? Raw materials za hivyo vyote tunavyo vitumia vimetoka Africa; why tumeshindwa kubadiri hizo raw materials into reality? Bado nina mashaka kama weusi tupo sawa na watu wa rangi nyingine.
 
Back
Top Bottom