Dikteta Captain Traore wa Burkina Faso ana maajabu gani kumfanya kukubalika sana na Waafrika wengi?

Dikteta Captain Traore wa Burkina Faso ana maajabu gani kumfanya kukubalika sana na Waafrika wengi?

Kwa nini huyu Rais dikteta wa Burkina Faso Waafrika wanapenda kumpamba sana kwa taarifa za uongo na propaganda? Ana maajabu gani?
Hapa wanasema alialikwa katika uapisho wa Trump akakataa!🤣
View attachment 3208451
Unafikiri kufukuza wanajeshi wa Kifaransa kwenda kwao ni kazi rahisi. Hujui jinsi Mfaransa alivyokuwa akiendeleza ukolonui katika nchi makoloni yake. Kimsingi hazikuwa huru na ndio kwanza zinajitambua.
 
Imetumika vigezo gani kumuita dikteta?
Tuelekeze
 
Usikute na wewe mtoa mada ni wale wimbi kubwa waliofaulu sana mwaka huu form 4.
 
Kwa nini huyu Rais dikteta wa Burkina Faso Waafrika wanapenda kumpamba sana kwa taarifa za uongo na propaganda? Ana maajabu gani?
Hapa wanasema alialikwa katika uapisho wa Trump akakataa!🤣
View attachment 3208451
Madikteta wengi sana hapa duniani huwa wanatawala nchi zao kwa njia za kueneza Propaganda za Vitisho, Ghiriba na Ulaghai. Hiyo ni kawaida kabisa.
 
Jamaa kapambana kuwaondoa waxeng£ wote wanaojifanya wanajihadi na waasi wa msituni.. Dhahabu ya burkinafaso haichakachuliwi tena na france hivyo kupelekea mapato kuongezeka maradufu kupitia sekta ya madini. Nafasi za watu kuajiriwa zinaongezeka ukilinganisha na huko nyuma... amani ilitoweka kwa kipindi kirefu sana burkinafaso lakini sasa imerejea. Alaf anakuja **** la mbweha km mleta huu uzi analeta usomi wa university of mburahati anasemaa....... dah nitakupiga kibao wewee
Endeleeni kumeza propoganda za kipuuzi na kijuha, mwaka jana huko kwenye mji Barsalogho magaidi walifanya shambulizi na kuua watu 600, mashambulizi ya kigaidi yameshika kasi zaidi mwaka 2024, nusu ya nchi ya Burkina Faso haina udhibiti wa serikali mpaka sasa, maelfu ya shule zimefungwa na malaki ya watoto wako wamejifungia makwao kwa kukosekana usalama.
 
Madikteta wengi sana hapa duniani huwa wanatawala nchi zao kwa njia za kueneza Propaganda za Vitisho, Ghiriba na Ulaghai. Hiyo ni kawaida kabisa.
Ni mambo ya hovyo sana, mamilioni ya Waafrika vilaza wameaminishwa Burkina Faso sasa hivi mambo ni mazuri sana wakati ni kinyume chake.
 
Eleza amefanya kipi au hajafanya nini ili aitwe dikteta. Usiongee kiujumla taja matukio amefanya yenye hivyo vigezo
Mimi siwezi kusema Yoda ni mwizi bila kutaja ameiba vitu gani, nikiambiwa nieleze kwanini namuita mwizi najibu sababu ameiba bila kutaja vitu alivyo iba.
Vigezo vya demokrasia
 
Back
Top Bottom