Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
15,052
Reaction score
36,866
Mke wa ndugu yetu amefariki baada ya kuumwa kansa kwa muda mrefu, kabla hajafariki amefichua siri kwa mumewe kwamba mtoto wao wa mwisho si mwanae bali ni mtoto wa shemeji (rafiki wa mumewe) ambaye alishafariki kwa ajali miaka 5 iliyopita.

Kabla ya usaliti, huyo shemeji alikua ni mtu wa karibu sana na mumewe kama kaka mkubwa na ndiye alitumika kuwapatanisha baada ya mumewe kukiri kuwa na mchepuko na kuuzalisha watoto mapacha miaka michache tu baada ya wao kuoana. Mke aliwapokea hao watoto, wakakubaliana kutowaambia watu kwamba si wanae na akawalea kama watoto wake wa kwanza. Baadaye na wao wakajaliwa watoto watatu (ikijumuisha huyo wa mwisho ambaye kibaiolojia si wake)

Siku mbili baada ya kutoa hiyo siri, mke alifariki. Imepita miezi 3 sasa ila ndugu yetu anashindwa kuachilia na kusamehe, amejawa na hasira na uchungu na amekua mtu wa pombe na ulevi kupitiliza.

Mtoto wao wa mwisho ambaye ana miaka 7, ndiye mtoto aliyekua karibu naye sana kama baba, ni mtoto wao pekee wa kike na mtoto ambaye wamekua wanaishi naye nyumbani kwa sababu watoto wengine ni wakubwa na wako mashuleni.

Tatizo jingine ni kwamba; sasa kila akimuangalia mtoto anajisikia chuki na hasira ya kusalitiwa na ameanza kupoteza upendo kwa mtoto. Ni kama mwezi hivi umepita tangu ajihakikishie kwa DNA kwamba yule si mtoto wake wa kumzaa ila hana cha kufanya wala pa kumpeleka kwa sababu mkewe na rafiki yake ambao ndiyo wazazi wa mtoto wote wameshafariki na hawana ndugu wa kueleweka ambao anaweza kwenda kumuacha mtoto kwao.

Mshaurini, atapitaje pitaje hapa? kama kuna ushauri mzuri nitascreenshot nimfikishie.

Shukrani!
 
Sad Tears GIF by Big Brother Naija (1).gif
 
Mke wa

Mshaurini, atapitaje pitaje hapa? kama kuna ushauri mzuri nitascreenshot nimfikishie.

Shukrani!
Mungu niepushe mbali na majaribu ya hivi.
Ampeleke Kwa ndugu wa rafiki yake aliefariki na awaeleze Kila kitu.
Ila ndy hvy atakuwa amekili hadharani kuwa mkewe alipigwa fimbo.
Dunia simama nishuke
 
Mke wa ndugu yetu amefariki baada ya kuumwa kansa kwa muda mrefu, kabla hajafariki amefichua siri kwa mumewe kwamba mtoto wao wa mwisho si mwanae bali ni mtoto wa shemeji (rafiki wa mumewe) ambaye alishafariki kwa ajali miaka 5 iliyopita.
binti kiziwi huyu anahitaji kwanza kutenganisha makosa ya wazazi na mtoto. Mtoto hana kosa lolote, wala hakuchagua kuzaliwa hivyo. Miaka 7 amemjua huyo mtu kama baba yake, hivyo kumkataa ghafla kunaweza kumuacha na jeraha kubwa la maisha.

Kwa sasa asifanye uamuzi wa hasira wala kutumia pombe kama njia ya kukabiliana na maumivu. Aongee na mshauri wa familia/saikolojia na ndugu anayemuamini, hasa kabla hajamwambia mtoto kuhusu DNA.

Kumsamehe marehemu si lazima iwe leo; uponyaji unachukua muda. Lakini mtoto huyu anahitaji baba yake sasa kuliko wakati mwingine wowote.
 
Wanaume tunapenda kusaliti, lakini sio wake zetu wasaliti

Mimi huwa nachukia hata mchepuko wangu akinisaliti (imagine), tunaweza tukaachana kabisa yaani

Mwambie atumie busara zetu Wazee wa mwaka 47 "Kitanda hakizai haramu"

Yeye alileta mapacha, mke kaleta mmoja

Watoto ni baraka, ampokee na kumlea kama mwanaye wa damu
 
Wanaume tunapenda kusaliti, lakini sio wake zetu wasaliti
Mimi huwa nachukia hata mchepuko wangu akinisaliti (imagine), tunaweza tukaachana kabisa yaani
Hebu nielezee mzee mwenzangu, huwa sielewi, kwanini mnakua hivi?
Mwambie atumie busara zetu Wazee wa mwaka 47 "Kitanda hakizai haramu"
Yeye alileta mapacha, mke kaleta mmoja
Watoto ni baraka, ampokee na kumlea kama mwanaye wa damu
Nimeupokea ushauri.
 
Mke wa ndugu yetu amefariki baada ya kuumwa kansa kwa muda mrefu, kabla hajafariki amefichua siri kwa mumewe kwamba mtoto wao eleweka ambao anaweza kwenda kumuacha mtoto kwao.

Mshaurini, atapitaje pitaje hapa? kama kuna ushauri mzuri nitascreenshot nimfikishie.

Shukrani!
Amlee tu, kuna ushahidi upi watakaoutumia wale wa upande wa shemeji kumdai mtoto? Kitamaduni watoto atakaozaa mwanamke ni wangu kama nitakuwa nimemtolea mahari ikiwa nitaridhia. Pia mtoto mwenye changamoto ni wa kike, atakuwa na kuolewa ataenda kwake. Tatizo lingekuwa kubwa endapo angekuwa wa kiume
 
Anapaswa kushukuru kwa kufahamu ukweli mapema, mshauri alee watoto wote ni wake tena huyo wa kike anaweza kumfaa kuliko wanae anaomini kuwa ni wake.

Nilijifunza jambo moja kwa Wakurya, wachaga na Wamasai wao wamewafundisha watoto wao wa kiume sio watoto wote watazaliwa ndoani kwake ni wake, ukipata na ukawa unaamini mmoja au wawili kati ya hao ni wako ni jambo la kushukuru maana hata wanaume wana watoto wengine nje ya ndoa zao. Lea wote ni wako
 
Mungu niepushe mbali na majaribu ya hivi.
Ampeleke Kwa ndugu wa rafiki yake aliefariki na awaeleze Kila kitu.
Ila ndy hvy atakuwa amekili hadharani kuwa mkewe alipigwa fimbo.
Dunia simama nishuke
Alisema ndugu wa rafiki yake na familia ya mkewe wote ni maisha duni, akimpeleka mtoto huko vijijii atateseka sana, na anapata ugumu maana huyo mtoto anampenda sana baba yake na baada ya mama yake kufariki amebaki naye kama mzazi pekee.
 
Akapige miti mdogo mdogo ...DevilKazini

😂😂 Hapo mkuu umempeleka mbali sana. Mtoto hana kosa na si lazima kumsubiri afike Form One ndiyo aanze maisha yake. Mlee kwa upendo kwanza, mambo mengine yatafuata kwa hekima.
Kaka hii isikie tu kwa mwenzio inaumaaa sana bora angekuwepo wa kumpa lawama sasa yote yamekufaaa
 
Kwa vile msaliti (Marehemu mkewe) amesha fariki,basi amlee tu huyo mtoto ambaye hana makosa,
Kama yeye alisamehewa na mkewe kwa kuzaa nje ya ndoa huku akiwa ndani ya ndoa,halafu mkewe akakubali kuwalea hao watoto,basi na yeye amlee huyo mtoto wa marehemu mkewe coz hata Baba wa huyo mtoto alisha fariki pia,

Huyo jamaa nae ni msaliti pia,kupunguza hasira zake akumbuke kua hata yeye alimsaliti mkewe,

Nina wasiwasi na hiyo issue ya DNA,aliipimia wapi? Mahakama gani ilimpa ruhusa ya kufanya hiyo DNA? coz DNA ina taratibu zake,sio kama kwenda kupima Malaria tu.,

Labda swali langu niwaulize tu wana jamii,Je marehemu alikua sahihi kutoa hiyo siri kua huyo mtoto hakua mtoto wa mumewe?
 
Back
Top Bottom